Hii inaitwa flat slab (slab ambayo inaungwa moja kwa moja na nguzo bila uwepo wa mkanda). Kwa hapo, span ya jengo ni kubwa sana, angalau kidogo kungekuwa na nguzo zingine kati kati ili kugawa hiyo span. Hapo slab imeshindwa kujibeba yenyewe (self weight) ikaundergo deflection kabla hata mzigo mwingine kuwepo juu yake
Hiyo ni moja, lakini failure nyingine ya flat slab huwa inatokea kwenye perimeter ya column. Mfano wa flat slab ni sawa na mtu achukue sindano azisimamishe then juu aweke kitambaa cha nguo, muda wowote mzigo ukizidi kiasi kilichopigiwa hesabu, slab inatoboka kwenye nguzo na kushuka chini ndio maana wengine huwa wanaweka drop panel na column capital kwenye nguzo ili angalau kupunguza hiyo risk ya slab kutoboka
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.