Makanisa Iweni Macho na Walimu wa Neno la Mungu.

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Huduma ya UALIMU wa Neno la MUNGU kwa miaka ya karibuni imedhihiri kuwa na mlipuko wa kuenea kwa kasi ya ajabu kuliko huduma zingine kama Uchungaji, Uinjilisti na Ushuhudiaji.

Kabla ya majira ya mlipuko huo, huduma ya Ualimu wa Neno la MUNGU haikuwa na nafasi kubwa ndani ya Kanisa.

Makanisa mengi yalizuia huduma hii kama ambavyo Huduma (Ministries) zinazoendeshwa na Mitume na Manabii zinavyozuia pia huduma ya Ualimu wa Neno la MUNGU.

Hata hivyo, huduma hii imevamiwa na baadhi ya Watumishi wa kujipachika wasio na vigezo, ambao hata hivyo hawadumu na huduma hii bali wanalenga kutengeneza majina makubwa na baadaye kutamani huduma zingine za Utume na Unabii wanakoweza kumiliki Madhabahu, wafuasi na mapato. Mitume na Manabii wengi wamepatikana kwa njia hii.

Hii ndiyo hali iliyofanya wilaya ya Mbozi kuongoza dunia kwa uwiano wa Makanisa na watu (Church Per Capita).

Mwalimu mmoja wa Neno la MUNGU nilimhoji kuhusiana na madai haya, akajitetea kwamba Kanisa libebe lawama kwa sababu vyuo vya Kanisa havina mtaala wa mafunzo ya huduma ya Ualimu wa Neno la MUNGU.

Hali hii inatoa mwito kwa Makanisa kuja na mpango maalum wa kuwachagua, kuwapima, kuwachuja na kuwapa vibali/leseni Walimu wa Neno la MUNGU wanaojizukia na kutamalaki Madhabahu.

Soli Deo Gloria.
 
Ni kweli hichi pia ni kichaka kingine kinachohitaji macho ya rohoni kupambanua
Wengine wao wakiishapiga semina wanasaini vocha ya malipo kama walialikwa na Kanisa. Kama waliandaa wenyewe semina na kuomba tu Madhabahu basi hugawana mapato na kiongozi/Kanisa husika (Gospel-entrepreneurship)
 
Wilaya ya momba na mbozi kwa Tanzania ndio Brazil ya mitume na manabii,kila baada ya nyumba ka
dhaa unakutana na kanisa mbaya zaidi wengine ni makada wa vyama vya siasa.
Kazi ipo mkuu. Yesu ahairishe kurudi mapema. Injili bado iko chini ya 50%.
 
Back
Top Bottom