Chuo kikuu mpaka kuamua kutakaku-apply jeshi..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuo kikuu mpaka kuamua kutakaku-apply jeshi.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rasib, Jul 14, 2012.

 1. Rasib

  Rasib JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Habari jamani wadau wa jukwaa la siasa, Wadau najua yaweza ikawa nimekosea kwa namna moja ama nyingine kupost hii khabari hapa lakini nimefikiria kwa kina wapi niiweke ili nipate msaada stahiki nikaona bora hapa maana jukwaa hili huwa lipo makini hasa kwa hoja na ushauri uliosimama.....
  Mada yangu kama inavyojieleza hapo juu, mimi ni kijana niliyemaliza masomo yangu ya chuo(degree) katika chuo kikuu cha Dodoma mwaka jana, pursuing BA project planning management and community development. Na matokeo yangu yapo vizuri sana ila shida inakuja nimejaribu kuapply kazi ktk nafasi mbalimbali pale zinapotoka na hasa hizi za kimaendeleo bila mafanikio, nimefanyiwa udahili zaidi ya mara 130 bila mafanikio zaidi napoteza hela na muda wangu ulio na dhamani kubwa kwangu. Mimi kutokana na elimu yangu niliyoipata chuon nimefanikiwa kuandika bussiness plan ya kuku na nimefanikiwa kwa 75% na pia kupitia jamiiforum nimepata msaada mkubwa hasa ushauri na mambo mengine nashukuru sana kwa wajasiriamali na wachangiaji wa jukwaa hilo.
  Nini hasa kinanisukuma kutaka kuapply?
  Hasa ni kupata wigo mpana wa kuweza kupata nafasi ya kuimpact nilichosoma kwa jamii kupitia nafasi hiyo please njoo na ushauri ambao ni constructive na wala si destructive please and please, siyo lazima upost kama huna lakunishauri please..
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  By kufanyiwa udahili zaidi ya 130 times unamaanisha interviews?

  Na mie ntakudahili tena. Unataka nini? Sijaelewa ushauri juu ya kujiunga jeshi ama kuendelea kufuga kuku?
   
 3. M

  Magugu Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hebu kaa tena uandike vizuri tujue ni masaada gani unataka maanake hueleweki kabisaaaaa. Inawezekana ndo maana unakosa kupata hizo nafasi kwa sababu kujieleza kwako hakujitoshelezi. Au unaweza kujieleza kwa kiingereza kiswahili ni tabu basi fanya hivyo. Na kama kiingereza nacho ni tabu basi hapo tukusaidie uende tena darasani
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni bora uendelee kukuza biashara yako ya kuku bila ya shaka na mayai ,hakuna kitu bora kama kuweza kujiajiri mwenyewe ,elimu ni ufunguo wa maisha ,tumia elimu hiyo kujiendeleza ,kujiunga na jeshi sio jambo baya ila huko utakuwa umefika na unaweza kupoteza hata biashara ambayo kama sikosei utakuwa umeianza ,ila utakuja kujuta hapo baadae utakapofikia umri wa kuacha kazi ,wapo waliowahi kufanya kazi jeshini wakiwa na vyeo vizuri tu ,lakini hii leo ukiwaona ,nyuso zimewabadilika.

  Nyuso zimewabadilika WAMEZEEKA KULIKO UNAVYOFIKIRIA ,na zaidi maisha yao yamekuwa duni sana ,unajua unapoacha kazi ya jeshi kwa hapa kwetu basi hata thamani yako inapungua ,inakuwa kama ndio unaanza maisha mepya.
  Lakini ukianza leo kujiajiri mwenyewe na ukaitunza kazi na miradi yako basi ujue utafanikiwa sana kimaisha.

  Kuna msemo wa kigeni usemao The real money comes from your own business ,sasa fikiria kwa undani kauli hiyo.
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mwalimu kwa zaidi ya miaka 25 sasa; nimefundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaaama na vyuo vingine mbalimbali duniani katika muda wote huo. Nitakushauri mambo mawili tu kati ya yale ambayo huwa nawashauri wanafunzi wangu.

  (1) Jambo la kwanza unapokwenda kwenye usaili wowote ule, jitahidi kuonyesha kuwa wewe ni mtu mzuri ambaye wasaili watafurahi sana kufanya kazi nawe. Kuwa na mawasiliano mazuri, usionyeshe majivuno ya kiujua sana, bali onyesha kuwa unaweza kujifunza kwao kirahisi na vile vile wanaweza kujifunza kwako kirahisi. Kushinda kwako mitihani shuleni siyo jambo ambalo waajiri wanataka, bali wanachotaka ni uwezo wako wa kufanya kazi nao.

  (2) Jambo la pili ni kuwa onyesha kuwa wewe ni mtu potential sana ambaye unaona mambo kwa mbali sana. Jitahidi kuwa analytical badala ya kuonyesha kuwa unakariri uliyofundishwa shuleni. Kwa kufanya hivyo utaonyesha kuwa unaweza kuwasaidia wao kufanikisha biashara au shughuli zao zaidi ya wao wanavyofikiri.


  Post yako hapo juu, inaonyesha kuwa yote hayo mawili wewe huna. Katika post hiyo umeonyesha kuwa ni egotist zaidi ukijielezea mwenyewe bila kuonyesha nini unachotaka kutuletea hapa JF.

  -.... kuna kitu kinaitwa Communication Skills ambacho unaelekea kukikosa.
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ni bora uendelee kukuza biashara yako ya kuku bila ya shaka na mayai ,hakuna kitu bora kama kuweza kujiajiri mwenyewe ,elimu ni ufunguo wa maisha ,tumia elimu hiyo kujiendeleza ,kujiunga na jeshi sio jambo baya ila huko utakuwa umefika na unaweza kupoteza hata biashara ambayo kama sikosei utakuwa umeianza ,ila utakuja kujuta hapo baadae utakapofikia umri wa kuacha kazi ,wapo waliowahi kufanya kazi jeshini wakiwa na vyeo vizuri tu ,lakini hii leo ukiwaona ,nyuso zimewabadilika.

  Nyuso zimewabadilika WAMEZEEKA KULIKO UNAVYOFIKIRIA ,na zaidi maisha yao yamekuwa duni sana ,unajua unapoacha kazi ya jeshi kwa hapa kwetu basi hata thamani yako inapungua ,inakuwa kama ndio unaanza maisha mepya.
  Lakini ukianza leo kujiajiri mwenyewe na ukaitunza kazi na miradi yako basi ujue utafanikiwa sana kimaisha.

  Kuna msemo wa kigeni usemao The real money comes from your own business ,sasa fikiria kwa undani kauli hiyo.
   
 7. Rasib

  Rasib JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  nataka kujiunga jeshi mkuu, nsaidie
   
 8. Rasib

  Rasib JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  thnx mkuu, ngoja niendelee kusubiri na wengne waniambie nifanye nin
   
 9. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtazamo wangu wa haraka nimebaini mapungufu mengi tu upande wako,kama umekuwa enterviewed mara 130 na mara zote hujapata kazi basi inaonekana huwa hujipangi vizuri kabla ya kwenda kwenye hizo enterview.kwanza jinoe vizuri na uweze kuongea kiswahili fasaha taratibu na kwa kujiamini,kuwa msafi wa mwili na nguo zako,vaa vizuri kwa namna inayo kutofautisha wewe na mtu wa mtaani,kuwa patient wasikilize kwa makini na tumia kila fursa uipatayo kuwaonesha you can deliver the best,kama unatumia kiswahili basi kiwe fasaha vivyo hivyo kama unatumia kiingereza kiwe sahihi na kinachoeleweka.usitumie maneno usiyo kuwa na uhakika nayo.
  Siku hizi hata jeshini wanataka watu wanao elewa mambo, wabunifu na siyo tu watu wenye vyeti vyenye grades nzuri! umewahi kukaa chini na kujiuliza kwanini hujapata kazi pamoja enterview zote hizo?pengine ni kwasababu unakimbilia kuwaonesha vyeti vyako vizuri na siyo kuwaonesha the finest ujuzi na ubunifu ulionao.onesha kuwa unafahamu mambo kwa vitendo anza na LUGHA YAKO IS IT SMART?
  Kwangu mimi wazo la kujiajiri stands to be the best idea to dwell on.usiwe na haraka na mafanikio kwasababu hata wadau wako wanahitaji kujua mengi kutoka kwako kabla hawaja kuamini kihivyo.watu wa bank mathalani watataka kujiridhisha kama wewe ni mwaminifu unaweza kurudisha fedha zao kwa wakati n.k
   
 10. r

  richone Senior Member

  #10
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nakushauri endelea kukuza ufugaji wako wa kuku. lakini sii kukimbilia kutafuta ajiri ndio maaa ya wewe kusoma tena isitoshe umesoma PPM maanayake wewe unauwezo wa kubuni miradi.
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kichuguu habari za masiku mkuu
  Huyu kijana issue ni issue kubwa kwa vijana wengi wa Kitanzania .Hawasomi alama za nyakati hata kidogo wanadhani watu wana angalia vyeti kama walivyi waafrika wengi u proudish wa kuitwa Pro au Dr badala ya kuitwa Kichuguu tu kawaida na titles zako za kishule ziko lazima zitatambuliwa .Huyu aendelee na kuku for sure maana si rahisi kupata kazi akiwa fresh namna hiyo .Kama kaanza kuku kwa nini anataka kuajiriwa tena ? Anaweza kuwa vyema zaidi kuliko kutaka kutumwa .
   
 12. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,360
  Likes Received: 2,989
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye usaili mara 130 ndiyo penye kuleta wasi wasi. Bora uendelee na kufuga kuku maana elimu ni UJUZI na si CHETI. Kama utakumbuka shirika la HAKIELIMU liliingia ktk mvutano mkubwa na serikali ya awamu ya tatu mpaka kufungiwa. Tatizo likiwa kusema ukweli kuhusu aina ya elimu imejielekeza ktk kupata cheti bila kuweza kufanya chcht kile.
   
 13. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,876
  Likes Received: 2,824
  Trophy Points: 280
  Haki ya nani JF ni kiboko! Unakuja moto unarudi bariiidi! Jamaa anasema kadahiliwa mara 130. Hivi ni udahili au usaili? Hapo lazima akose kazi!
   
 14. papag

  papag JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 688
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  wanafunzi wengi wa kitanzania mara wamalizapo vyuo wanatagemea matokeo yao mazuri kwenye vyeti ndio yatawapa kazi nzuri.Hilo silikatai ila wanasahau kitu kimoja.katika utafutaji wa kazi waajiri wengi pamoja na kuangalia cheti chako ulichotunukiwa kikubwa wanachooangalia ni ule uwezo wako binafsi na muenekano wako kwao.sasa ht km una GPA y a 1st class honours lkn majivuno yako kibao,kichwani hamna kitu,exposure ya nje ya masomo yako huna.unategemea kwenye soko la ajira utafanikiwa kweli?fikiri kaa chini.....chukua hatua
   
 15. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Una kila dalili ya kuanza kukata tamaa.Wazo lako la kutaka kujiunga na jeshi unaliona kama ni jawabu la kukata kwako tamaa sio!Halafu dogo kuwa mkweli kidogo,,,,chuo umemaliza mwaka jana,vyeti vimetoka mwezi mmoja uliopita,ajabu wewe umeshapiga intervew 130!Unafanya usaili mala ngapi kwa siku aisee?Hii inakuingia akilini hata wewe kweli?
   
 16. Karikenye

  Karikenye JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Rafiki yangu hebu jiulize ni kitu gani unataka kufanya hapa duniani...what is your destiny? What are you passionate about? What Job do you think will give you heart satisfaction? Baada ya kupata majibu hayo then unaweza kujua kama kujiunga na Jeshi ndio your ultimate destiny..

  Isipokuwa nafasi za professionals (Graduates) zitatangazwa kuanzia mwezi wa august or September.. kama that is what you are passionately about... you just wait and apply... Isipokuwa siku hizi kama unataka kujiunga na Jeshi kirahisi lazima upitie JKT voluntarily then kutoka hapo ni rahisi kuajiriwa na JWTZ japo JKT ni mtoto wa JWTZ na basically wote military training yao is equally the same... remain blessed!
   
Loading...