Wanaoichafua UDOM na kui link na CCM hamtutendei haki kabisa,kila chuo kina UVCCM cha ajabu hapa UDOM japokuwa UVCCM ni wachache sana na wanafanya kazi zao kwa kujificha wakiogopa kuzomewa na wanafunzi,lakini cha ajabu kila wakifanyacho wanafiki wanasema UDOM imefanya hiki...huu ni ujinga mkubwa,hata kumchangia kikwete form mwaka 2010 walifanya UVCCM baada ya kupewa pesa na mkuu wa mkoa wa wakati huo wakishirikiana na Katibu mkuu wa wakati huu mzee Makamba,lakini wenye chuki wakasema UDOM imemchangia kikwete! Binafsi habari hizi huwa nazikuta jamii forums tu,nadhani ifikie hatua uwongo huu ukome,,,mbona hamuandiki harakati za CHADEMA? mbona hamuandiki habari za BAVICHA UDOM kujenga ofisi zao? Mbona hamuandiki habari za wanafunzi wa CHADEMA ambao ni wengi zaidi chuon kufanya mikutano ya hadhara vijijini wakati wa weekend kuelimisha umma kuhusu mambo ya msingi? Ufikie wakati upotoshaji huu ukome,uongo na uzandiki dhidi ya UDOM ufikie mwisho,hamuwatendei haki wanafunzi na walimu ambao ni wana mageuzi....mleta mada omba radhi jukwaani,ni tabia mbaya kudanganya umma