Nanren
JF-Expert Member
- May 11, 2009
- 2,440
- 2,142
mwenye maamuzi ya kukataa ni mwanamke,ni wanaume wachache sana wenye uwezo wa kusema NO mbele ya mwanamke (ndio maana siku zote sisi wanaume tunwafuata nyinyi wanawake na kuwatongoza) hiyo ni nature na ndivyo ilivyo leo hii yule ambaye ukimuhitaji lazime uonyeshe nia kwa zaidi ya miezi miwili mfululizo,unamkuta tayari yupo barabarani ni wewe tu na pochi yako...mtu anayetumia mwili wake kupambana na hali ngumu ya maisha badala ya ubongo ni hasara kubwa...sasa kama yeye mwenye elimu anafanya hivyo yule ambaye hajaenda shule kabisa afanye nini?...Na infact sio kwamba wana hali ngumu ni tamaa tu na kuendekeza starehe (kupenda vya bure mchezo),so ladies wakiamua kuanzia leo hatuuzi tena wala hatutoi bure,na hatumuonjeshi mtu mpaka tuolewe...aaah tutaskia labda kesi ya kubaka na bila shaka muhusika atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria
Kwa hiyo kwako wewe, huwezi kubaka kwa vile unaogopa sheria.
Ila unaweza kununua ngono kwa vile sheria ya kuzuia biashara ya ngono labda haipo au haina nguvu, si ndio?
It is being naive na nikujiendekeza tamaa zako za mwili, ni uchovu wa akili na kukosa ujasiri, unapo-conclude kuwa mwanaume hawezi kumkataa mwanamke. Urijali ni pamoja na ujasiri wa kupambana na tamaa za ngono, sio kupigisha pigisha tu fimbo yako.
Bado msimamo wangu ni kuwa hao wasichana wanaouza miili pamoja na wanaume wanaonunua wote wanatakiwa kulaumiwa. Nchi za wenzetu, ukikamatwa unanunua ngono nje ya eneo linalohusika, wote mnapelekwa kortini. Na nchi zingine, ni marufuku kabisa suala la kuuza mwili kwa ajili ya ngono. Ningekusifia ungekuwa unapendekeza kuwa sheria ziongozewe nguvu zaidi kuwazuia wanunuaji na wauzaji. Kuuza bangi na kununua bangi, yote ni makosa. Sasa iweje kuuza ngono ndio kosa saana halafu eti mnunuaji hana kosa na asilaumiwe?... holy crap!