Chuo cha IFM kimezingirwa na biashara ya mitumba, chips na mama lishe

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Hakika jiji la Dar es Salaam limevamia na wafanyabiashara wajasiamali maarufu machinga, mama lishe, wauza chips wauza mitumba kila kona. Wametanda pembezoni mwa barabara mbalimbali za jiji wakifanya biashara.

Posta ndio usiseme kila sehemu ni vibanda vya mitumba, mama lishe wakipika vyakula mbalimbali, vibanda vya wauza chips vimeshamiri mpaka imekuwa kero.

Hatukatai machinga kufanya biashara lakini watengewe maeneo rasmi sio barabarani au mbele za maofisi na maduka. Ukifika chuo cha IFM wauza mitumba, wachoma chips wamejaa eneo la chuo mpaka shule ya msingi bunge.

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Hao wamachinga baadhi yao ni wale wahitimu wa vyuo vikuu walioshindwa kuajiriwa na Serikali mara tu baadavya kuhitimu masomo yao!

Hivyo wameamua kujiongeza kwa kujiajiri kama wamachinga. Ukiwachokoza hao ni sawa tu na kuchezea moto jirani na mafuta ya petroli!

Yakilipuka, tutaelewana tu kama Taifa.
 
Wanafunzi hao hao ndio wenye shughuli hizo za machinga, mama lishe, wauza chips wauza mitumba

Wengine wanapata pesa ya kulipia ada kutumia biashara hizo hizo, wanaouza ni wafanya kazi wao
 
Sera ya CCM ni kuchafua jiji kwa namna yoyote Ile. Hata ukiweza kujisaidia haja kubwa Ocean Road yote, unaruhusiwa ili mradi tu uwe na kadi ya 🔰
Wangekuwa wapiga kura CCM wangekuwa wanaiba kura mchana kweupe?

20210822_151734.jpg
 
Hao wamachinga baadhi yao ni wale wahitimu wa vyuo vikuu walioshindwa kuajiriwa na Serikali mara tu baadavya kuhitimu masomo yao!

Hivyo wameamua kujiongeza kwa kujiajiri kama wamachinga. Ukiwachokoza hao ni sawa tu na kuchezea moto jirani na mafuta ya petroli!
Yakilipuka, tutaelewana tu kama Taifa.
Ngoja Waizunguke IKULU ya MAGOGONI tuone kama ni Moto wa Petroli

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
NI chuo kinachosimamia fedha! Hata hivyo, chuo gani cha jengo moja kati ya jiji? Walishambiwa wachane na vyuo vya wizara lakini wao wanaona ni njia ya kupiga pesa tu!
 
Hao wamachinga baadhi yao ni wale wahitimu wa vyuo vikuu walioshindwa kuajiriwa na Serikali mara tu baadavya kuhitimu masomo yao!

Hivyo wameamua kujiongeza kwa kujiajiri kama wamachinga. Ukiwachokoza hao ni sawa tu na kuchezea moto jirani na mafuta ya petroli!
Yakilipuka, tutaelewana tu kama Taifa.
Kwa hiyo nchi isiwe na utaratibu, yani watu wavunje sheria tu alafu tufunge mahakama na magereza
 
Hao wamachinga baadhi yao ni wale wahitimu wa vyuo vikuu walioshindwa kuajiriwa na Serikali mara tu baadavya kuhitimu masomo yao!

Hivyo wameamua kujiongeza kwa kujiajiri kama wamachinga. Ukiwachokoza hao ni sawa tu na kuchezea moto jirani na mafuta ya petroli!
Yakilipuka, tutaelewana tu kama Taifa.
Siyo jukumu la serikali kuwaajiri wahitimu wa vyuo, na kukosa ajira siyo sababu ya kuhalalisha uvunjaji wa sheria na kanuni.
 
Back
Top Bottom