Hadhi ya Posta Mpya imeharibiwa na biashara za machinga na mama lishe

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Ukweli utawala wa awamu ya 5 kuruhusu wamachinga na mama lishe.

Kufanya biashara popote watakapo na wasibughudhiwe ulikuwa na ushamba wa aina yake. Zamani maeneo ya Posta yalikuwa ni maeneo ya kuvutia sana sio kwa wageni bali hata kwa wenyeji.

Yalikuwa masafi yasiyo na misongamano ya hovyo kama Manzese, Kariakoo, Mwenge, Buguruni na Mbagala. Leo Posta ni kama hayo maeneo.

Wamachinga wamepanga bidhaa zao mpaka barabara, mama lishe na majiko yao wanapika supu chai na chapati bado kidogo kuna mtu ataweka jiko la kuchoma mahindi na viazi kwenye Mnara wa Askari.

Tunaiomba manispaa ya jiji iwaondoe kabisa wamachinga na mama lishe eneo hilo na maeneo ya ofisi za umma ili kulifanya liwe safi na kuvutia.
 
Ndio shida kila mmoja wetu kutaka kuishi Mjini,Shughuli za Kilimo tumeziacha kabisa
 
Ukiona hivyo wanyonge walikuwa wamezidi kujivinjari mitaa ya posta kinyume na hapo awali, ndo maana wanapata wateja....
 
Kwahiyo CCM ni Chama cha Masikini na Wafanyakazi?

Dunia nzima Mkulima ni mtu Tajiri sasa hamuoni kuwa hicho Chama ni Nuksi?

Nimesema ukitaka kuwa maskini nchi HII sijaongelea duniani bali BONGO.
 
Jana nimeona RC makala kasema watasafisha mji soon!?? Inshort Magufuli viatu vya urais havikumtosha
 
Back
Top Bottom