Chuma Ulete: Ni kweli ipo? Ipi dawa ya kuidhibiti? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuma Ulete: Ni kweli ipo? Ipi dawa ya kuidhibiti?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mtego wa Noti, Feb 5, 2012.

 1. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Siku hizi inashangaza sana huku kwetu uswazi...
  Unakuta hela zilizo nyingi zimechanwa pembeni kidogo hasa kwenye pembe za noti......ukiwauliza kwa nn wanachana kdogo wanasema eti ni kudhibiti hela zao zisichukuliwe na chuma ulete.

  Inasemekana kuwa chuma ulete ni watu wanaotumia njia za hali ya juu zaidi za kimazingara kuchukua hela maeneo mbalimbali. Akikupa hela yake ukachanganya na za kwako basi hela zako zitapotea ktk mazingira yasiyoeleweka...

  Wenine wanasema kuna watu huwa hawana kazi yoyote lkn wanaishi tu huku mjini. Inasemekana baadhi yao hutumia chuma ulete...

  Ukifungua genge uswazi mara utasikia watu wenyeji wa hapo hasa wafanyabiashara wenzako wakisema...''Jiangalie sana yule mzee ni chuma ulete''......

  Haya maneno kuna wengine wanayaamini?

  =========
  Kwa hisani ya wanaojua:

  [​IMG]

  Jini wa Chuma Ulete

  Kwa muda mrefu nimekuwa nikipokea simu na barua pepe kutoka kwa watu mbalimbali wakiniomba niwaelezee jinsi ya kudhibiti chuma ulete.
  Chuma ulete ni uchawi ambao unarudisha nyuma jitihada za maendeleo ya watu wengi sana.

  Kwa ufupi Chuma ulete ni wizi wa kimazingara ama wizi wa kichawi au wizi wa kiini macho.

  Macho anayefanya wizi kwa kutumia chuma ulete anakuwa ameingia mkataba wa kiroho na jinni au majini wanao husika na wizi wa vitu na mali za watu.

  Chuma ulete zimegawanyika katika makundi makuu mawili. Ya kwanza, ni Chuma Ulete katika mapenzi na mahusiano na ya pili Chuma Ulete ambayo haihusiani na masuala ya mapenzi.

  Watu wengi hawafahamu kuhusu Chuma Ulete ya Mapenzi, bali wanafahamu kuhusu Chuma Ulete hii iliyo zoeleka kwa watu wengi.

  Chuma ulete katika mapenzi ni pale ambapo mwanamke anamfanyia uchawi wa mapenzi mwanaume mwenye kipato na kumfanya mwanaume huyo awe anampa mwanamke huyo pesa na mali zake zote. Zoezi hilo litaendelea mpaka mwanaume huyo atakapo filisika.

  Chuma ulete hii hufanywa zaidi na wanawake, lakini wapo pia wanaume wanao jihusisha na chuma ulete ya aina hii.

  Katika makala ya leo sitaielezea sana chuma ulete ya mapenzi, nitajikita zaidi katika chuma ulete iliyo zoeleka ingawa nitagusia kidogo kuhusu Chuma ulete ya mapenzi.

  Chuma ulete za mapenzi zipo za aina nyingi, lakini zenye nguvu, zipo za aina kumi na tatu. Nitaelezea kwa ufupi sana, aina moja tu kati ya hizo kumi na tatu.

  Kuna ndege mmoja anapatikana porini. Ndege huyo ana rangi nyeusi na kahawia, na macho yake huwa yenye ku’gaa. Dume la ndege hawa huwa na umbo dogo zaidi kuliko jike na huatamia na kulalia makinda. Kichali ama kiota cha ndege huyu, hutumika kuhifadhi mayai ya ndege wa aina nyingine ambae pia huishi porini.

  Basi mwanamke akimlisha mwanaume wake nyama ya ndege huyo pamoja na dawa ya mti fulani wa porini ambao matawi yake hutoa manyunyu wakati wa usiku. Mwanaume huyo atakuwa mtumwa wa mwanamke huyo katika siku zote za maisha yake na atakuwa anampatia mwanamke huyo kila anacho chuma.

  Naomba niishie hapo kwa leo kuhusu chuma ulete ya mapenzi, Nitaelezea aina zote kwa kina katika siku zijazo.

  Sasa tuje kwenye chuma ulete iliyo zoeleka na watu wengi. Kama nilivyo elezea hapo juu, chuma ulete ni wizi wa kichawi, au wizi wa kimazingira au wizi wa kiini macho.

  Anakuja mtu dukani kwako au kwenye eneo lako la biashara, anakupatia noti ya shilingi elfu kumi na kuagiza vitu vya shilingi elfu mbili. Utamrudishia chenji shilingi elfu ishirini na nane badala ya shilingi elfu nane. Tofauti utakuja kuiona wakati wa kupiga mahesabu na mwisho wa siku utaishia kugombana na mfanyakazi na kadhalika.

  Wengine anakuja kwa gia ya kuomba chenji, ukimpa chenji, kiasi fulani cha hela zako, kinahamia kwenye kibubu chake. Anaweza pia kununua vitu, ukimpa chenji, kiasi fulani cha hela kinahamia nyumbani kwako.

  Chuma ulete nyingine ni ya wizi wa vyakula majumbani na madukani. Wachawi wanatumia ndumba kuiba vitu kama vile unga, mchele sukari nakadhalika kwenye maduka na majumba ya watu. Nitaelezea chuma ulete hii katika siku zijazo, leo nitazungumza kuhusu chuma ulete ya hela.

  JINSI CHUMA ULETE INAVYOTENGENEZWA.

  Ili kutengeneza chuma ulete , mchawi huchukua njugu mawe nyeusi na kuimeza nzima nzima bila kuitafuna halafu anainya na kuichukua tena.
  Baada ya hapo atachukua mti unaitwa Kilinda Mgunda, anaunguza pamoja na hiyo njugu mawe nyeusi aliyo imeza na kuitoa kwa njia ya haja kubwa. Vinachomwa kisha vinasagwa na kuwa unga unga.

  Anachanjwa kwenye pembe zote za mwili wake na kupakwa hiyo ndumba halafu ndumba nyingine inawekwa kwenye chungu kisha inapikwa pamoja sarafu halafu anatumia kuoga

  Baada ya hapo ataenda kuwaalika majini wa chuma ulete ulete. Jinsi majini wa chuma ulete wanavyo alikwa. Kinachukuliwa kipande cha ngozi ya hayawani wa mwituni, ngozi ya kinyonga iliyo kaushwa, pamoja na pangaa ya mti. Pangaa ya mti ni mti ulio ota juu ya mti mwingine.

  Vitu vyote hivi vinachomwa pamoja na njugu mawe na kisha kusagwa na kufungwa kwenye kitambaa chekundu pamoja na jinni halafu vinaenda kufungwa kichawi kwenye mti mkubwa kwa muda wa siku tatu usiku na mchana.

  Baada ya hapo, ndumba hiyo itatolewa mahali hapo na kwenda kuwekwa kichawi katika eneo la sokoni vinapo uzwa vitu.

  Baada ya siku tatu ndumba hiyo inachukuliwa inaenda kuzikwa kaburini kwa muda wa siku tatu.

  Siku ya saba, ndumba hiyo inachukuliwa na kupelekwa kwenye chumba maalumu, kwa ajili ya kupikwa kichawi. Basi baada ya hapo, hiyo chuma ulete itakuwa inafuata amri ya mtu huyo na kumpatia chochote anachokitaka.

  JINSI YA KUIDHIBITI CHUMA ULETE

  Zipo njia za kudhibiti chuma ulete, si rahisi kuzielezea zote kwa wakati mmoja, leo nitaelezea njia hii ifuatayo ;

  Chinja kuku mweupe halafu chukua firigisi. Pasua hiyo firigisi halafu weka ndani yake shilingi elfu moja ya noti . Baada ya hapo nenda kaichimbie chini ya ardhi kwa muda wa siku sita. Siku ya saba nenda kafukue hiyo firigisi, chukua shilingi elfu moja yako na uiweke kwenye droo ya biashara yako na ututukanga.

  Basi hakuna mchawi yoyote Yule atakuja kuiba hela kichawi kwenye biashara yako.

  MAKALA HAYA YAMEANDALIWA NA DOKTA. MUNGWA KABILI, MTAALAMU ALIYE BOBEA KATIKA ULIMWENGU USIOONEKANA.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2013
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,473
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Mmmh sikuwahi kuamini inafanya kazi.

  Mwenzangu amechukua lilizo lwa ajili ya hili ana bucha za samaki sasa ikawa mauzo yanaenda tofauti na mzgo uliouzwa; imewatokea mara sita akaamua kumweka ndugu pesa wanapokea wanaandika anaweka kwenye droo ikifka jion waliochandika kwenye daftar na pesa iliopo tofauti ikawa mara tatu lkwa ndugu sasa jamaa amepga simu baada ya kulkaa mwenyewe siku saba kwamba kuna majini yanachukua h yake nkamwambia hiyo ironleta wala usichoke ;;mm
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2013
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hiyo biashara imekwishamshinda aachane nayo aangalie kitu kingine cha kufanya.
   
 4. m

  mahakama ya kazi JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2013
  Joined: Feb 20, 2013
  Messages: 1,469
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  du,dawa yake kwanza usitoe chenji hovyo,pili ukirudisha chenji weka juu ya meza usimkabidhi mkononi.
   
 5. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2013
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  sawa kabisa
   
 6. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2013
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 630
  Trophy Points: 280
  Mkabidhi Yesu uone.
  This will never happen again
   
 7. High Vampire

  High Vampire JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2013
  Joined: Nov 17, 2012
  Messages: 2,054
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Afunge kwa kusali na kuwasamehe wote aliowakosea
   
 8. Rockcity native

  Rockcity native JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2013
  Joined: Dec 31, 2012
  Messages: 2,087
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
  Mtafute manyaunyau ni bingwa wa kutengua hzo issue
   
 9. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2013
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  Yesu ndie dawa, tena ni bureeee.
   
 10. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2013
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Bangi ni dawa tosha ya chuma ulete!
   
 11. Kijana leo

  Kijana leo JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2013
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 2,872
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  piga maombi hapo, funika kwa damu ya yesu. halafu njoo tena hapa useme kuwa amekutendea.
   
 12. dist111

  dist111 JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2013
  Joined: Nov 29, 2012
  Messages: 2,941
  Likes Received: 1,286
  Trophy Points: 280
  Dawa ni kutozichanganya hela, ukimhisi mtu (aulizie majirani wakora huwa wanajulikana) hela yake weka pembeni! Basi mchezo wake kwishney
   
 13. F

  FUSO JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2013
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,339
  Trophy Points: 280
  bora ya hiyo ya chuma ulete chamtoto -- kuna jamaa mke wake anatembelewa na jini mahaba!! wakiamuka kuwasha taa usiku wanakuta jini limeshafanya kazi yake; yaani ndoa ipo mashakani, kwa waganga imeshindikana; kanisani umeshindikana; yaani balaa tupu.
   
 14. m

  mmasai kilema Member

  #14
  Mar 18, 2013
  Joined: Mar 1, 2013
  Messages: 63
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kama hao chuma ulete wapo kwanini wasiende bank kuchukua hela tena nyingi . Baadala ya hizo elfu elfu za samaki
   
 15. M

  Mponjori JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2013
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 2,210
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  huko benk sijui kuna nini,naskia ndumba zote zmegonga mwamba.
   
 16. F

  Funge JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2013
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 585
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hilo jini kiboko yao walokole. Mwambie aende kwa kanisa la kilokole
   
 17. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2013
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mwambie asalimishe hii biashara na yeye kwa Bwana Yesu ili ale memaya nchi.

  Sent using wireless by wire
   
 18. vanmedy

  vanmedy JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2013
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 2,245
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  aweke kipande cha mkaa kwenye droo la hela
   
 19. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #19
  Mar 18, 2013
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  au mifupa ya NOAH, teh teh teh
   
 20. N

  Nyakwaratony JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2013
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 575
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mh... kweli???
   
Loading...