Chuki kwa waume zenu kipindi cha ujauzito

Chuki kwa waume zenu kipindi cha ujauzito

Wanaharibu mood za watu hawa sumtyms..Mi wife nae ni mjamzito..Basi karibu deile tunagombana... Jana ameingia home akanikuta nacheki mpira..Kabla hata ajakaa akatoa pesa kwenye pochi yake akanambia "baby naomba ukanichukulie msosi na vocha"..Mi nikamind kimoyomoyo..Mtu ametoka nje,amevipita vibanda kama 10000 huko lakini hajanunua vitu vyake zen anakuja kusumbua watu hapa..

Nikaona isiwe tabu..Nikamwambia poa..Sikuchukua hela yake..Nikaenda fasta kumnunulia nikarudi...Ule msosi kaugusa kidogo akasema haupandi..Akaniomba nikamchukulie mwingine..Nikamwambia avumilie kidogo basi game ikiisha ntaenda..Mtu haelewi anadai njaa inamuuma hawezi kuvumilia..

Mi Nikatoka home nikaenda kukaa bar ya karibu nikaendelea kucheki mpira..Afta one hr baada ya game kuisha nikarudi home na msosi mkononi..Basi hilo zogo lake sasa..Mwanamke aliongea mpka usiku muda wa kulala..Asubuhi pia kaamka na gubu lile la jana basi tafrani tupu

Nimeamua nisitishe zoezi la kugawa mimba aisee..Huyu nadhani ndo atakuwa mtt wangu wa mwisho
Hongera sana Mimi nilishawahi kulazwa kwenye sofa eti Kisa akiguswa na gegedu hata mgongoni atatapika
 
Mkuu na akiwa kwenye period anakuwa sio zake / zako?
Hiyo ni makusudi tu.

Pili ni ishara kwamba huyo mtoto alie tumboni sio wa kwako, hakutaki.

Mtoto akianza kukukataa toka tumboni ujue huyo sio wako.

Wanawake wajanja wanajua mtoto akiwa sio wako wanasingizia mimba sijui nini ila sio kweli.

Alafu hayo mambo yako africa tu, wazungu kipindi cha ujauzito ndio mapenzi huwa yanaongezeka kwa waume zao maana mtoto ni wa baba kweli.

Huu ujinga mimi sitaukubali.
 
Pepo limemkumbaa kemea... Mbona mama yake Yesu akumchukia mumewe au vile hakuwa baba mwenye mimba!
 
sidhani kama kuna wanaofanya makusudi. Wakati wa ujauzito kunatokea mabadiliko makubwa. nakumbuka nlikuwa sensitive sana na utando wa buibui. Kila nikikaa kwenye kochi nikiangalia juu naona umejitokeza. Nikiona namwita house maid aje kutoa. Akija anatoa machooo lakini haoni. naamua kumnyang'ang'anya ufagio kwa hasira huku nikimsema vibaya, natoa mwenyewe. Baada ya kujifungua sikuwa najali kuhusu utando wa buibui. Baadae nilikuja kuhisi hata ule niliokuwa nauona haukuwa halisi maana haiwezekani mahali kila siku patolewe utando wa buibui na buibui kila siku alete utando wake. Pia kuna mtoto wa miaka mitatu nilikuwa nampenda sana. Ilikuwa akiniringia naumia moyo eti naona ananifanyia makusudi kumbe ni mtoto tu.

Siku moja nikaenda hotelini nikaagiza chakula. Nikala vijiko viwili nikahisi mboga imechacha. Wakanibadilishia. Ya pili hivyo hivyo nikawaambia imechacha. Mhudumu akanibishia na tukabadilishana maneno sana. Supervisor akaingilia akasema niletewe aina nyingine. Nayo nikala kidogo nikahisi imechacha. Hapo nikahisi mi ndo mwenye matatizo. Nikalipa nikaondoka kwa aibu.

kitu kingine jamani genye!! uuuuwi sitaki hata kukumbuka. nusura niwe kichaa maana hata baba wa mtoto mwenyewe hakuwepo kwenye picha, tulishaachana kabla hata sijajua nina ujauzito. Angekuwepo nahisi angekimbia nyumba na boxer mkononi! Namshukuru Mungu kipindi kilipita salama, ni miaka 8 sasa.
 
Mlishabeba mimba?kama bado nawaombea mzibebe ili na nyie mfanya hayo maksudi

Tena hawa kungekua na uwezekano wakuzibeba tungewaogeshea kitandani maana hata kunyanyuka sidhani kama wangeweza.
 
Huyo ulomzaa alikuwa mtoto wa kiume au wa kike?!!?
 
Tena hawa kungekua na uwezekano wakuzibeba tungewaogeshea kitandani maana hata kunyanyuka sidhani kama wangeweza.
Mmmh !! wee Nao !! Tungeweza huoni Watu tunabeba wake wanne (mathna,wathulatha wa Rubaa) na watoto wote pamoja na ukoo mzima ktk msafara wa maisha hadi tunaitwa "shaibu" !!!
 
  • Thanks
Reactions: nao
mimba ikikuchukia na mama kufikia hatua kuchukia tendo la ndoa au kukosa hamu mimba inapofikia third trimester huyo ni mtoto wa kiume ikikupenda sana na mwanamke kupenda sana tendo la ndoa ni mtoto wa kike. utafiti wangu mwenyewe
 
Back
Top Bottom