Christopher Ole Sendeka ateuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa Halmashauri Kuu ya CCM

Christopher Ole Sendeka ateuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa Halmashauri Kuu ya CCM

Vyeo vyote vya kichama,ndani ya CCM,ni kwa mujibu wa Katiba,Kanuni na Taratibu za chama. Kuanzia cheo cha Mwenyekiti wa Taifa hadi mjumbe wa shina,vyote vipo kikatiba. Katiba itumikayo sasa ni ile ya mwaka 1977,toleo la 2010.

Katika Katiba ya CCM,hakuna cheo kinachojitegemea na kuitwa Msemaji wa CCM. Kikatiba,msemaji wa CCM wa kitaifa ni Mwenyekiti. Mwenyekiti hukasimu mamlaka yake hayo kwa Katibu Mkuu na Katibu wa Itikadi na Uenezi. Vyeo vyote hivyo vipo kikatiba.

Hakuna cheo cha Msemaji wa CCM alichopewa Ndugu Christopher Ole Sendeka. Ni cheo hewa. Hakipo. Baada ya uwepo wa wafanyakazi na mishahara hewa,sasa ni cheo hewa!

Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam
 
heeeeeee! kweli au umemkumbuka huyu mzeee duuuuuh! hahahaaaaa nicheke kidogo CCM sasa imekuwa kama simba na yanga.

Au wanamuogopa MAGUFULI atawatumbua hadhalani kwenye mambo yao?
 
endelea na mambo yako hapo chuoni achana na mambo ya ccm

Kwani CCM ni mali yako wewe?Aachane na mambo ya CCM kwa uongo upi aliouandika au kwa kuwa huna ukijuacho kuhusu katiba?

Cheo cha Sendeka na alichowahi pewa A.Mrema cha makamu waziri mkuu vipo kwenye katiba ipi?.
 
Nilijua tu ! Ukiona mtu yeyote anaanza kuzurura baada ya kupewa cheo basi haraka sana kitilie shaka cheo chenyewe , nilishamuuliza humu , wee sendeka unafanya ziara zote hizi kama nani ?
 
Sendeka tunakupenda ccm wenzako sana achana na shombo za wapinzani,sendeka mpiganaji hodari na safi sana
 
chama chetu pendwa kiko mbele kwa kila jambo baya,mzee tupatupa asante kutufumnbua macho.
 
Mbona cheo cha itikadi na uenezi ndicho anachokitumikia Ole Sendeka
 
Aya ukimalize kajipongeze na kiroba saaf huku unazungusha mikono
 
Mimi siyo gamba ila namsif ole sendeka kuchangamkia fursa. Cheo ni hela bana kikubwa hapo ni hela tuu. Hata mm ningekipata ningefanya mabos
 
Back
Top Bottom