Christopher Ole Sendeka ateuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa Halmashauri Kuu ya CCM

Christopher Ole Sendeka ateuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa Halmashauri Kuu ya CCM

Vyeo vyote vya kichama,ndani ya CCM,ni kwa mujibu wa Katiba,Kanuni na Taratibu za chama. Kuanzia cheo cha Mwenyekiti wa Taifa hadi mjumbe wa shina,vyote vipo kikatiba. Katiba itumikayo sasa ni ile ya mwaka 1977,toleo la 2010.

Katika Katiba ya CCM,hakuna cheo kinachojitegemea na kuitwa Msemaji wa CCM. Kikatiba,msemaji wa CCM wa kitaifa ni Mwenyekiti. Mwenyekiti hukasimu mamlaka yake hayo kwa Katibu Mkuu na Katibu wa Itikadi na Uenezi. Vyeo vyote hivyo vipo kikatiba.

Hakuna cheo cha Msemaji wa CCM alichopewa Ndugu Christopher Ole Sendeka. Ni cheo hewa. Hakipo. Baada ya uwepo wa wafanyakazi na mishahara hewa,sasa ni cheo hewa!

Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam
Mmeanza majungu yenu baada ya Sendeka kupingana na Mwenyekiti wake mtarajiwa na Mkuu wa mkoa Fulani kwenye msiba wa Kabwe kama mwakilishi wa chama kuhusu kutumbuliwa kwa Marehemu Kabwe.
 
Mmeanza majungu yenu baada ya Sendeka kupingana na Mwenyekiti wake mtarajiwa na Mkuu wa mkoa Fulani kwenye msiba wa Kabwe kama mwakilishi wa chama kuhusu kutumbuliwa kwa Marehemu Kabwe.

Aisee kuna katip fulani hapo very interesting. God in the details
 
Sendeka kacheo kake ni ka kuzugia kwa kulamba wakubwa miguu.

Hii inafanana na movie za Kikorea ambapo huwa kuna watu kazi yao ni kuwa maboi wa waheshimiwa, hawatakiwi kupinga kitu
 
Ina maana Bw.Eli sendeka haijui katiba ya CCM? Ana kweli Na ninani aliyempa cheo hewa Huyo Mzee?Mbona alifanya party kujipongeza?
 
Hivi karibuni Bw.Christopher Ole Sendeka alipewa cheo cha kuwa Msemaji wa Chama.Nimetafuta katiba ya TANU Na ya CCM lakini sijaona Cheo hicho.Najiuliza hivi aliyempa cheo hicho Bw.

Sendeka alikuwa Na maana gani? Hivi Bw. Ole Sendeka anaijua katiba ya CCM? Naamini aliyempa Bw.Sendeka cheo hicho alipitiwa kidogo Na Bw. Sendeka alikubali cheo hicho Kwa kuwa hana shughuli baada ya wakwao kumkataa.
 
wewe mlete maada huna kazi zingine za kufanya mpaka unapata muda wa kwenda kupitia kurasa zote za katiba ya chama?
 
Hivi karibuni Bw.Christopher Ole Sendeka alipewa cheo cha kuwa Msemaji wa Chama.Nimetafuta katiba ya TANU Na ya CCM lakini sijaona Cheo hicho.Najiuliza hivi aliyempa cheo hicho Bw.Sendeka alikuwa Na maana gani? Hivi Bw.Ole Sendeka anaijua katiba ya CCM? Naamini aliyempa Bw.Sendeka cheo hicho alipitiwa kidogo Na Bw.Sendeka alikubali cheo hicho Kwa kuwa hana shughuli baada ya wakwao kumkataa.


Heeeeeeeeeeeeeeeh, tayari mmeanza kukanyagana kama alivyowahi kusema DK. Kitine...Duh, makundi ndani ya CCM yameanza figisufigisu....ni hatari...mtauana mwaka huu...lazima utumbuaji uendelee hata ndani ya chama...
 
Walisema ni kumsaidia Nape kwa sababu ana majukumu ya uwaziri hadi hapo uchaguzi mwingine utakapofanyuka
 
wewe mlete maada huna kazi zingine za kufanya mpaka unapata muda wa kwenda kupitia kurasa zote za katiba ya chama?
Ndugu yangu, mtu anapojisomea anaongeza uelewa, anapanua maarifa. Ukiwa huna tabia ya kupenda kujisomea, ya uongo, yenye chumvi utalishwa na kuishia kupotoshwa. Jenga utamaduni wa kujisomea, hata hoja zako zitakuwa imara.

Ila utahitaji kupunguza muda wa mambo mengine ili upate maarifa mapya. Ninakutakia heri.
 
Akakua ana piga jaramba kusubira. Baada magu kupewa chama ndio naye atakasimishwa rasmi cha nape.
 
kwani wewe mbona kama huna kazi. Povu lina kutoka. kwani katiba ya chama ni siri huko ugambani
 
Back
Top Bottom