Chris Lukosi katoa ushauri mzuri jinsi TRA wanavyokosa mapato

The Mongolian Savage

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
6,191
13,616
Yeereeeeeh!

Chris Lukosi Mfanyabiashara Mtanzania maarufu Uingereza ametoa ushauri mzuri kwa TRA na kusikitika jinsi wanavyokosa mapato mengi kupitia bandarini.

Anasema alitoka bandarini huko Uingereza akahesabu magari 250 kwenye meli yaliyokuwa yanaletwa bandari ya Dar na Mombasa.

Kati ya hayo magari 250 zaidi ya magari 180 pamoja na malori yalikuwa yanaenda Kenya, magari 10 Uganda na magari 22 Tanzania.

Cha kushangaza magari yote yanayoenda Kenya ni kuanzia mwaka wa 2014 kuja juu halafu makali kichizi lakini yaliyoagizwa na wabongo ni ya miaka 2004 huko ya kawaida.

Chris anasikitika sana si eti wabongo hawana nia na uwezo wa kutuma bali ushuru ni mkubwa mno.

Kwa mfano yeye alikuwa anauza ford ranger ya 2017 milion saba tu watu walishindwa kukununua kwasababu ushuru wake kuitoa Dar port milion 22 mara tatu.

Aliendelea kushauri iwapo TRA wangeshusha ushuru watu wengi wangeagiza magari mengi sana na TRA kupata ushuru, masheli yangepata mapato mengi, magereji yangenufaika, ma car wash n. K.

Ushauri wa jamaa mzuri sana na nimeukubali.

Ila nimecheka kwenye koments jamaa mmoja kamuuliza mbona haya hukuyasema mwendazake alipokuwa hai?

Wangari Maathai RRONDO
 
Tatizo la taasisi za nchi hii ni kutokujua wanataka nini hasa ??

Hivi lengo la kuweka kodi kubwa kwenye magari used ni kukusanya kodi kubwa au ku-discourage importation kubwa ya magari used ili watu wanunue magari mapya?????
Mkuu si nadhani ushuru wa magari mapya na used yote asilimia ni sawa tu ama magari mapya ushuru wao ni chini?
 
wangeshusha ushuru wenye Ford ranger wangekuwa zaidi ya 500 na ushuru wangepokea zaidi na zaidi. Pia hapo hapo wauza spear wangeongezeka,
Dah uuze ford 7m ushuru uwe mara 3 .ila Mungu tuzidi kumshukuru kutuondolea majanga yale jamani! Hapa mjini nawaona wenye ranger hawazudi 5
Sheria za Kenya huruhusiwi kuingiza gari lililotengenezwa miaka 7 iliyopita.
Tz wana kodi ya uchakavu tena kubwa sana
 
Ninavyojua magari mapya ushuru wake ni nafuu.
Dah sikujua hili ndo maana nlikuwa na sitasita. Basi sasa nitayaleta kama haya zaidi ya 30.
Screenshot_20210418_125806_com.android.chrome.jpg
 
Hiyo ni nondo na msingi wa kutengeneza pesa na kujenga uchumi wa nchi ila CCM/Serikali wameziba sikio (TRA) yao hawawezi elewa.
Wakipunguza tu ushuru magari mengi yataingia nchini na automatically:
1. Serikali/TRA watapata kodi kubwa zaid.
2. Wauza mafuta watauza sana na serikali itapiga kodi tena kwa mara nyingine kupitia mafuta yanayoingia pamoja na biashara ya kuuza mafuta.
3.Vipuri vya magari vitaingizwa nchini-kodi iko palepale
4. Gereji zitaongezeka-kodi kama kawaida
5. Madreva/leseni za udereva zitaongezeka-pesa iko hapa tena as usual.
6. Gereji na car wash zitaongezeka- pesa iko hapatena
Pesa ipo ila serikali/tra ni kichwa cha mwendawazimu inataka kodi kubwa kwa siku moja matokeo yake haipati na kuanza kubambikia watu kesi kwa kukosa maarifa. Naamini awamu hii ya sita itatumia zaidi akili badala ya nguvu.
 
Ukipita Uampala ukaona mikwaju wanayosukuma waganda, ukipita Nai city magari ya maana yapo road ukifuatilia ushuru wao ni wa kawaida kabisa yaani TRA ni watu wa ajabu hawajui wanataka nini kwa wakati gani, importation ya magari ikowa kubwa hata mafuta yatauzika sana, na kulikua na uwezekano hata nchi jirani kununua magari hapo hapo Bongo, ninadhani wanaweka viwango vikubwa vya kodi wakihisi ni kuongeza mapato kumbe wanayapunguza bila wao kufahamu
 
Tatizo miundombinu, magari yakijaa aipati picha foleni itakwaje, Kenya wapo juu sana kwenye barabara
sio lazima magari yote yajazane dar , mengine yatakwenda mikoani kupunguza tension ya usafiri huko , kilindi basi la kwenda handeni lilitoka asubuhi hamna tena namna ya kusafiri hadi kesho yake , labda ubahatishe private magari yakipoa bei yatasambaa hadi mikoani
 
Back
Top Bottom