Chris Lukosi katoa ushauri mzuri jinsi TRA wanavyokosa mapato

t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
3,501
2,000
Mkuu tuseme umeagiza gari jipya la thamani ya milion 60 tzs ushuru wake utakuwa shilling ngapi?
inategemea na aina ya gari, kama ni private au commercial, private mara nyingi inakuwa juu kwenye kodi kuliko commercial, japo kwenye commercial pia kuna configuration inakuwa nafuu
volvo used trucks ya mwaka 2001 kwa mfano, ikiwa tractor unit 4x2 kodi ni ml 13, ikiwa 6x2 ni mil kama mil 17 , ila Volvo hiyo hiyo ya mwaka huo huo ikiwa rigid , kodi ni kama mil 38.
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
43,084
2,000
Yeereeeeeh!

Chris Lukosi Mfanyabiashara Mtanzania maarufu Uingereza ametoa ushauri mzuri kwa TRA na kusikitika jinsi wanavyokosa mapato mengi kupitia bandarini.

Anasema alitoka bandarini huko Uingereza akahesabu magari 250 kwenye meli yaliyokuwa yanaletwa bandari ya Dar na Mombasa.

Kati ya hayo magari 250 zaidi ya magari 180 pamoja na malori yalikuwa yanaenda Kenya, magari 10 Uganda na magari 22 Tanzania.

Cha kushangaza magari yote yanayoenda kenya ni kuanzia mwaka wa 2014 kuja juu halafu makali kichizi lakini yaliyoagizwa na wabongo ni ya miaka 2004 huko ya kawaida.

Chris anasikitika sana si eti wabongo hawana nia na uwezo wa kutuma bali ushuru ni mkubwa mno.

Kwa mfano yeye alikuwa anauza ford ranger ya 2017 milion saba tu watu walishindwa kukununua kwasababu ushuru wake kuitoa Dar port milion 22 mara tatu.

Aliendelea kushauri iwapo TRA wangeshusha ushuru watu wengi wangeagiza magari mengi sana na TRA kupata ushuru, masheli yangepata mapato mengi, magereji yangenufaika, ma car wash n. K.

Ushauri wa jamaa mzuri sana na nimeukubali.

Ila nimecheka kwenye koments jamaa mmoja kamuuliza mbona haya ukuyasema mwendazake alipokuwa hai?

Wangari Maathai RRONDO

Chris Lukosi ni mpuuzi ,enzi za JIWE alikuwa anasifia tu muda wote ,aache unafiki angeshauri kipindi kile cha JIWE apunguze kodi sio awamu hii ndio anajifanya kuleta unafiki wake ,Aendelee kula chips na Chilisosi aliyoletewa na wanawe.
 

Glenn

JF-Expert Member
May 22, 2018
12,251
2,000
Mkuu tuseme umeagiza gari jipya la thamani ya milion 60 tzs ushuru wake utakuwa shilling ngapi?
Huyu mnyama ni wa 2013, bei ya kununulia ni 91ml, ushuru 24ml
Screenshot_20210418-131830_Chrome.jpg
Screenshot_20210418-132248_Chrome.jpg
 

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
14,929
2,000
Ukipita kampala ukaona mikwaju wanayosukuma waganda, ukipita Nai city magari ya maana yapo road ukifuatilia ushuru wao ni wa kawaida kabisa yaani TRA ni watu wa ajabu hawajui wanataka nini kwa wakati gani, importation ya magari ikowa kubwa hata mafuta yatauzika sana, na kulikua na uwezekano hata nchi jirani kununua magari hapo hapo Bongo, ninadhani wanaweka viwango vikubwa vya kodi wakihisi ni kuongeza mapato kumbe wanayapunguza bila wao kufahamu
Wakishusha kodi watu wa nchi jirani watafuata magari hapa Bongo. Yard zitaibuka kotekote mipakani na kujuza uchumi. TRA bado wanafikiri kijamaa kuwa gari ni anasa.
 

ipyax

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
3,166
2,000
inategemea na aina ya gari, kama ni private au commercial, private mara nyingi inakuwa juu kwenye kodi kuliko commercial, japo kwenye commercial pia kuna configuration inakuwa nafuu
volvo used trucks ya mwaka 2001 kwa mfano, ikiwa tractor unit 4x2 kodi ni ml 13, ikiwa 6x2 ni mil kama mil 17 , ila Volvo hiyo hiyo ya mwaka huo huo ikiwa rigid , kodi ni kama mil 38.
Nasikia klm anafanya modification hapo hapo Dar ili kupunguza kibano cha import duty.
 

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,946
2,000
Shida ya hii nchi Magari yanaonekana kama kitu cha anasa na sio kitu muhimu..ila baskeli na pikipiki sio anasa ila nikitu cha lazama..
Nenda Zanzibar watu wanaendesha magari mpya bado sababu ya ushuru kuwa mdogo.. gari unanunua laki 7 Zanzibar na bado linatembea..
Umaskini mwingine huwa ni wakujitakia wenyewe.Wenye madaraka wanaona fahari kuendelea kunyenyekewa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom