Chonde Kanisa Katoliki, historia inatuhukumu

Oct 5, 2015
88
476
CHONDE VIONGOZI WA KANISA KATOLIKI - HISTORIA INAWASUTA.

"Viongozi wa dini kuhamasisha watu kupiga kura wakati huu, ni sawa na kuchochea chuki"

Hali ya maisha katika nchi za mashariki ya kati ndio mfano halisi wa mambo makuu matatu yanayoweza kumfanya binadamu aamue kwa hiari yake kuondoa uhai wa binadamu mwingine; moja Ni chuki za kisiasa, pili ni chuki za kidini na tatu ni visasi (CIA -Assassination manual).

Vibaya zaidi ni pale mambo haya yanapochanganyika pamoja, hapo maujai yatadumu vizazi na vizazi, kama inavyotokea huko mashariki ya kati.

Tanzania ipo mbali sana na nchi za mashariki ya kati, lakini haipo mbali na Rwanda ambayo angalau imeonja joto ya chuki za kisiasa zilizokuzwa na tatizo la ukabila na kupelekea mauaji ya halaiki. Ndio kusema kuwa, sababu kuu ya mauaji ya halaiki ya Aprili 1994 huko nchini Rwanda haikuwa kuuawa kwa Rais wao Juvenal Habyarimana bali chuki kati ya wahutu na watutsi iliyodumu kwa muda mrefu uliopita, huku kanisa KATOLIKI likiwa sehemu ya kuhandisi hisia hizo za chuki. Mauaji ya Rais Habyarimana pamoja na mambo mengine yanayosenwa vilikuwa ni vichocheo vya mauaji, lakini sababu kubwa ni chuki iliyokomaa.
Tanzania imejifunza nini kutoka Rwanda? Kanisa KATOLIKI limejifunza nini kutoka Rwanda.

Mwezi machi mwaka 2017 kiongozi wa kanisa KATOLIKI duniani Papa Francis alimpokea Rais Paul Kagame huko Vatican yalipo makao makuu ya kanisa hilo Kongwe duniani. Dhumuni kubwa alokuwa nalo Papa Ni 'kuomba msamaha' kwa kile alichokiita 'DHAMBI NA KUSHINDWA KWA KANISA' (The sin and the failure of the Church). Dhambi hiyo ya kanisa ni kwa viongozi wake; maaskofu, mapadre, ma-brother, masister na hata viongozi wa 'walei' walioshiriki kwa njia tofauti mauaji ya watutsi nchini Rwanda.

Ushiriki wa kanisa katika mauaji hayo ulikuwa kwa 'MAHUBIRI YA CHUKI DHIDI YA WATUTSI, KUWAELEKEZA WAUAJI MAHALI WALIPOJIFICHA WATUTSI, KUWARUHUSU WAUAJI WAINGIE MAKANISANI NA KUWAUA WATUTSI WALIOJIFICHA HUMO, BAADHI YA MAPADRE NAWO WALISHIKA SILAHA NA KUUA WATUTSI.

Jambo la kusikitisha zaidi baada ya mauaji hayo ya halaiki kanisa liliwaficha na/au kuwatorosha mapadre na maaskofu walioshiriki mauaji ili waepuke mkono wa Sheria. Kanisa liliwasaidia WAUAJI kupata hifadhi katika mataifa ya Ulaya kwa kughushi nyaraka za utambulisho wao ili waonekane ni wakimbizi au wahanga wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Ombi la msamaha la Papa Francis lilipokelewa na Serikali ya Rwanda kwa shingo upande, kwani pamoja na ombi hilo, kanisa halikuwahi kuonesha nia ya kuwarudisha na kuwafichua wauaji ili wahukumiwe inavyostahili, isipokuwa jumuia za kimataifa ndio zimekuwa zikijitutumua kuwatafuta wauaji walikokimbilia.

Padre Athanas Seromba ni mfano mmoja wa viongozi wa kanisa walioshiriki mauaji ya watutsi na kutoroshwa na kanisa. Akiwa paroko (kiongozi wa kanisa ngazi ya parokia) wa parokia ya Nyange ndani ya jimbo la Kibuye, Padre Seromba alishiriki mauaji ya watutsi 2000 waliokuwa wameomba hifadhi ndani ya parokia yake. Inadaiwa kuwa Padre Seromba mwenyewe pia alishiriki mauaji hayo ya tarehe 6 na 25 Aprili 1994. Lakini mwezi Julai 1994, Seromba alitoroshwa na kwenda kuishi nchini Italia ambako alibadili jina na kuitwa Atanansio Sumba Baru, na zaidi aliendelea na huduma ya upadre kwenye kanisa moja pembeni ya mji wa Florence, Italia.

Hata hivyo, madhabahu yalimzomea Bwana Seromba, hakuwa na amani ya nafsi na hatimaye akashindwa kuji-hifadhi na dhambi alizotenda. Februari 2002 Padre Seromba alitoka hadharani na kukubali ashitakiwe, lakini alikana mashitaka. Desemba 2006 alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 15, akakata rufaa. Machi 2008, mahakama ya ICTR ikajiridhisha kuwa makosa ya Seromba ni makubwa kuliko ilivyodhaniwa kabla, na kwahiyo akahukumiwa kifungo cha maisha. Leo, Padre Athanas Seromba anatumikia kifungo cha maisha ndani ya gereza la Akpro-Missérété huko mjini Porto-Novo, Benin.

Kauli ya Padre Alister Makubi.

Kauli ya Padre Alister Makubi wa kanisa la Mt. Petro - DSM na baadhi ya viongozi wa kanisa KATOLIKI nchini Tanzania za kuwashawishi wananchi kupiga kura, ni kauli zinazotafakarisha hasa kuangalia wakati huu ambapo nchi yetu ipo kwenye matishio makuu mawili.

Moja ni chuki za kisiasa zinazokua kwa kasi kutokana na kuminywa kwa uhuru wa kisiasa kwa wanasiasa wa upinzani.

Pili ni tishio la ugaidi kwa kurejea mauaji ya watu 6 huko mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. Taarifa zinasema wauaji hao wanaojitambulisha kuwa na ushirika na kundi la ISIS, wengi wao Ni watanzania waliowahi kutumikia Al-Shabaab na sasa wamerejea Tanzania.

Kwa sababu ya matishio hayo mawili, mtu yeyote mwenye akili timamu anajua - silaha kubwa inayohitajika kwa sasa kuepuka hatati zinazoweza kutokea ni umoja wa kitaifa. Kuhamasisha watu wakapige kura wakati vyama 7 vya siasa vimetangaza kujitoa kwa sababu ya dhuluma ya wazi, ni kutangaza kuwa upande unaoonwa kuwa wa dhuluma. Kanisa KATOLIKI linapaswa kujiepusha kushiriki dhuluma hii na badala yake lijikite kwenye kuhubiri amani na kushawishi kupatikana kwa suluhu baina ya vyama vya siasa.

Haiwezekani kutenganisha dini na siasa, lakini uhusiano wa dini na siasa haupaswi kuwa wa kuchochea chuki. Kuna idadi kubwa ya wakatoliki ambao ni wafuasi wa vyama vya upinzani na wanaunga mkono uamuzi wa vyama vyao kugomea uchaguzi, kuwahamasisha watu hao kupiga kura ni sawa na kuwaambia waunge mkono dhuluma za serikali ya CCM, na kwa maana hiyo kanisa linaunga mkono dhuluma za CCM kama lilivyounga mkono mauaji ya halaiki kule Rwanda.
Waumini wa dini zingine ambao pia ni wafuasi wa vyama vya upinzani wanatafsiri vipi hatua hiyo ya kanisa KATOLIKI ya kuhamasisha waumini wake wakapige kura wakati huu wa hali tete?
Viongozi wa kanisa wawe waangalifu kwa sababu chuki haimuachi aliyeichochea, bali inamrudia. Kule Rwanda, pamoja na baadhi ya viongozi wa kanisa KATOLIKI kuchochea maasi, wapo miongoni mwao waliokataa kushiriki maasi kwa namna tofauti. Wapo waliokemea kwa maneno na wapo waliokataa kuwaruhusu wahutu waingie kanisani na kuua watutsi, na kwahiyo viongozi hao waliuawa. Inakadiriwa mapadre na masister zaidi ya 200 waliuawa kwa kukataa kushirikiana na wauaji. Maana yake nini! Unachochea chuki halafu mambo yakiharibika yanakuathiri na wewe mwenyewe au ndugu na rafiki zako.

Maoni yangu ni kwamba, kama viongozi wa kanisa hawaoni haja ya kushawishi kupatikana kwa suluhu ya kisiasa wakati huu, ni bora wakae kimya. Kama viongozi wa dini wataendelea kuhamasisha watu kupiga kura wakati huu, watakuwa wanachochea chuki kwa kuungana na upande mmoja kati ya pande mbili zinazohasimiana.

Kanisa KATOLIKI lina mchango mkubwa kwenye maendeleo ya Taifa, hiyo ni sifa nzuri ambayo haipaswi kuchafuliwa.
Viongozi wahubiri amani na mshikamano, kama hawawezi basi waendelee kuhubiri dini na mambo mengine. Tayari kuna watu wanaamini Kanisa haliwezi kukemea serikali inapofanya hujuma kwa wapinzani kisa Rais ni mkatoliki, hisia hizo hasipaswi kuchochewa na kanisa.
Nawasilisha.
 
Walimuua Yesu, wamebaki na MARIA, vita ya RWANDA walihuska sana, soma historia ya hii dola ya RUMI.






 
Kwa nini wakiongea kkkt ni vigeregere kwa bavicha na wakiongea rc ni full povu kw bavicha?
 
Kwahiyo kwa akili yako matope unasema.

KKKT -CHADEMA

BAVICHA-CHADEMA.

Ila huleti maudhui yaliyo ongelewa, kweli wewe bora hata amfre polepole na ukilaza wake ila ni muelewa wa mambo
Hiyo ndio akili yako yasema. Mimi nimeandika hapo sijasema hayo kila mtu anaona.
 
Kwa nini wakiongea kkkt ni vigeregere kwa bavicha na wakiongea rc ni full povu kw bavicha?
RC historia yao hapo jirani Rwanda tunaijua. Hili kanisa linanuka damu za Watusi na Wahutu. Kule Songea hili kanisa kina Songea Mbano walikuwa wanabatizwa na padri kisha wananyongwa
 
43 Reactions
Reply
Back
Top Bottom