Chonde! Chonde! Mh.JK jibu hoja usifanye mzaha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chonde! Chonde! Mh.JK jibu hoja usifanye mzaha!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mmaroroi, Nov 19, 2010.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Katika hotuba yake kwa Bunge Rais JK alisema mimi ni Rais tu anayeondoka atarudi tu.Sasa kwa Rais makini ni vema ujiulize kwanini unakataliwa?Jibu pekee ni kukaa na wahusika ujue sababu ya kukukataa la sivyo unakuza jambo hilo na si muda mrefu utajutia maamuzi ya mzaha.Wananchi kwa sasa wanakupima busara ya kutatua suala hilo.Ziba ufa kabla ukuta haujaanguka.Hayo ndio yangu,Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  sijawahi kuona watu wamekaa mahari raisi anaongea wanazomea, japo walikuwa wanaangalia TV , basi jana kila mtu alikuwa anabeza kila alichoongea............ Kuna mahari akasema Tanzania tunauza zaidi kenya-kuna jama likasema mtoeni huyo
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mi natamani nilie nashindwa siku hizi ninatabu kweli kwenye kuangalia tv zoote zinzonyesha hotuba ya jk basi remote inakazi ya ziada!
   
 4. K

  Kagasheki Member

  #4
  Nov 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hotuba yake jana ilikuwa na mapungufu mengi sana haswa suala la udini ambalo wameliongea sana kipindi cha kampeni.Kimsingi sioni Udini unatokea wapi maana yeye mwenyewe juzi ameteua wabunge watatu wote waislamu,sijui tulitafsiri vipi?.Suala hili wamelifanya ajenda ili kumpunguza makali Dr.Slaa na wanachama na mashabiki wa CHADEMA lakini wanapotosha umma na matokeo yake ni mwanzo wa kuchochea udini ambao kimsingi haupo.
  Kauli ya kwamba Rais ni mmoja na wengine hawana mbadala nafikiri ni mwanzo wa kujenga mgogoro mpya mfano wa uliodumu Zanzibar kwa miaka kumi na tano.Tuna tatizo la msingi la katiba na Tume ya Uchaguzi ambayo kimamlaka inaingiliwa sana na watawala ambao ndio wateuzi wa viongozi wa tume hiyo.Hivyo wanaweza kujiona washindi kwa hivi sasa ila mbele ya safari hali inaweza kuwawia ngumu kutawala nchi hii.Ni suala la muda tu,tusubiri tuone
   
 5. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Heshima kwako mkuu umenikuna,Mungu yuu nasi tushirikiane kuikomboa nchi yetu.
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  Alisema amepunguza mfumuko wa bei kutoka asilimia 12 hadi asilimia 4 mwezi wa septemba
  .
   
 7. m

  mbezibeach Senior Member

  #7
  Nov 19, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi alinifurahisha sana jana alivyotoa ulimi.....hakuamini kama makamanda wa Chadema wanatoka nje...Nikapata hofu mkwere wetu asije tena akaanguka.
   
 8. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Usitegemee kwenye watu wa Tanzania ambao ni zaidi ya 40m wakukubali wote. Na hakuna duniani kiongozi ambae anakubaliwa na watu wake wote, haipo. Hakuna hoja hapo, mnalotaka la uchaguzi kurudiwa HALIPO jipangeni tu kwa 2015, Suala la katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi mahali pake ni kuonana na yeye kwa njia ya kiistaarabu ili apeleke mambo hayo bungeni, lakini so far hakuna hoja ndio maana anaendelea kutandika mzigo kama kawaida na si muda mrefu ataunda serikali. Yeye ndio RAIS na hakuna rais wa Tanzania mwingine zaidi yake.
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  c.r.a.p
   
 10. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  KATIKA SIKU NILIZOKUA DISGUSTED NA JK BASI JANA ZAIDI KILA KITU KWAKE MZAHA TU MARA HOO MZEE YUSUPH! MARA HOO FILAMU ZA BONGO...NCHI INA ISSUES NZITO ZA KUONGELEA YE ANAWAZA STAREHE TU...MSURA NAO MTABASAMU MPAAAAANA ULIMI NJE KILAA SAA....:laser:
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Aliniacha hoi kuna sehemu alisema najua waliotoka humu bungeni najua wananiangalia na kunisikiliza kwenye luninga......ama kweli Mkwere hamnazo
   
 12. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  yatamtokea puani
   
 13. Omukuru

  Omukuru JF-Expert Member

  #13
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  I'm not sure you think twice before you write. Hakuna anayedai uchaguzi urudiwe. Kinachodaiwa ni kubadili zile taratibu zilizopo zinazoibaka demokrasia. Baadhi ya vipengere vya katiba vinahitaji mabadiliko ili kukuza uhuru wa wabunge na wananchi kwa ujumla kwa maslahi ya umma. Tume inatakiwa kuwa huru zaidi ili iweze kufanya kazi yake kwa uwazi pasipo mshinikizo wa baadhi ya viongozi wa vyama au serikali. Lengo ni kwamba mabadiliko haya yausaidie umma wa Tanzania kuwachagua viongozi wake hiyo 2015 na kuendelea, kwa uhuru na haki na waongozwe na viongozi waliojichagulia wao wenyewe, na sio viongozi wa kulazimishwa kama ilivyo sasa katika baadhi ya maeneo.
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Nikaona TBC yule mtangazaji alikuwa anamkatili yule mama mwanaharakati kuongea .mtangazaji anataka mama asifie hotuba ya mheshimiwa ,Mama nae ameshikiri msimamo wake wa kukosoa hotuba ...
   
 15. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #15
  Nov 19, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Hivi Mkwere baada ya chuo kikuu hiyo miaka ya sabini amesoma mahali pengine au ndiyo anatumia nondo zilezile tu za miaka hiyo!!
   
 16. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #16
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Hakuna kitu namiss siku hizi za usoni kama maneno ya hekhima kutoka kwa rais.

  Nasikitika miaka mitano itapita nikiwa sina Rais wa kumsikiliza

  INANIUMA SANA KWA KWELI
   
 17. T

  Tofty JF-Expert Member

  #17
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 6, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yaani we acha tu........
   
 18. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #18
  Nov 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  bado kidogo tu ataanza kutangaza kumbi gani mzee yusufu ana piga!
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Nov 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hajawahi hata kwenda kwenye kwenye academic seminar na PASS degree yake
   
 20. Lenana

  Lenana JF-Expert Member

  #20
  Nov 19, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 422
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  ujinga na upumbavu wa kifisadi umakini hamna zama za mafisadi kufisidi nchi appointment ya meghji kurudi bungeni inajieleza tusitegemee mema katika ngwe hii watanzania tumezoea kuambiwa fungeni mikanda this time around ni zaidi ya kufunga hiyo mikanda!
   
Loading...