Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 414
Shirika la Marekani la Utafiti wa Anga (NASA) limesema ndege yake ya utafiti imefanikiwa kutua katika Sayari ya Mirihi (Mars) imefanikiwa kutua salama na kushusha kifaa cha utafiti kilichopewa jina Perseverance katika sayari hiyo nyekundu.
Hii ni hatua mpya katika utafiti wa anga za juu, ambapo kifaa hicho chenye ukubwa unaolingana na gari dogo kitakusanya sampuli za mawe kutoka katika sayari hiyo na kuyaleta duniani kwa mara ya kwanza katika historia ya mwanadamu.
Lengo la kutuma kifaa hicho cha utafiti ni kuangalia uwezekano wa kuwapo uhai katika sayari hiyo ya nne katika Sayari za Mfumo wa Jua, na kitapeleleza kwa muda wa miaka miwili.
Kwa sasa, wahandisi na wafanyakazi wa NASA wanashusha pumzi ya ahueni baada ya chombo hicho kufanikiwa kutua, kwani ni takriban nusu tu ya vyombo vya anga vilivyowahi kutumwa katika Sayari Nyekundu vimefanikiwa kutua salama!
Matokeo ya utafiti utakaofanywa na chombo Perseverance utamsogeza mwanadamu karibu zaidi na lengo la siku moja kuishi katika Sayari ya Mirihi. Licha ya kutumia gharama kubwa ya zaidi ya dola bilioni 3 (Sawa na zaidi ya Tsh. trilioni 6 na bilioni 900), NASA ina matumaini ya kupata matokeo yenye kulingana au zaidi ya thamani hiyo ya fedha kutokana na utafiti huo.
Chombo hicho kimetua karibu na eneo lililopewa jina Kreta ya Jezero, bonde lenye upana wa kilomita 12 lililopo karibu na Ikweta ya sayari hiyo. Eneo hilo linaaminika kuwahi kuwa na mto uliotengeneza delta zaidi ya miaka bilioni 3.6 iliyopita, hivyo kufanya uwezekano wa kuwapo viumbe hai au masalia ya viumbe hai kuwa mkubwa.
Marekani inapewa changamoto na mataifa ya China na Umoja wa Falme za Kiarabu ambao pia wametuma vyombo vyao vya anga katika Sayari hiyo Nyekundu kupeleleza uwezekano wa uwepo wa uhai. Wingi wa shughuli za anga katika sayari hiyo kunaifanya kuwa kitovu cha utafiti wa anga za juu kwa takriban kipindi cha karne ijayo.