Mzawa_G
JF-Expert Member
- Feb 27, 2014
- 667
- 1,467
Siku ya jana umoja wa ulaya uliweza kurusha chombo anga za mbali ambacho kimepewa jina la Juice space craft kuelekea katika safari ya miaka 7 ya uchunguzi kwenye miezi mbalimbali ya sayari ya Jupiter
Mwanadamu amebaki na maswali mengi sana juu ya miezi kadhaa ya sayari ya Jupiter ambayo mengine ndani yake imejawa na barafu bila kusahau ule mwezi wa Ganymede wenye kiasi kikubwa cha maji kuliko maji yote yanayopatikana duniani
Chombo hicho kilibebwa katika rocke ya umoja wa ulaya inayojulikana kama Ariane 5 ambapo tutahitajika kusubiria kipindi cha miaka 7 kwa chombo hicho kuweza kufika katika miezo hiyo ya Jupiter
Kumbuka sayari ya Jupiter ni sayari namba 2 yenye miezi mingi zaidi katika mfumo wa nyota Jua huku namba moja ikishikwa na sayari ya Saturn
Mwanadamu bado anaendelea kutafuta alama ya miasha ya viumbe hai katika maeneo mbalimbali huku akiwa ana kiasi fulani cha uhakika huenda kwenye mwezi wa Ganymede kukawa na maisha ya viumbe wa majini
Moudyswema
Tanzaniascienceyetu
AstronomyKiswahili