Januari 3, 2023 kutakuwa na kupatwa kwa sayari ya Mars

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
Mwaka mpya wa 2023 unaashiriwa na tukio la kipekee angani la Mwezi kuficha sayari ya Mirihi (Mars) siku ya Jumanne tarehe 03 Januari. Usiku wa siku hiyo sayari angavu nyekundu ya Mirihi itazibwa na Mwezi ulio karibu kwa kiasi masaa mawili kuanzia saa 4:15 usiku. Kuanzia saa 4:24 Mirihi itaanza kufunikwa ma Mwezi kutoka ukingo wake wa chini kulia. Hutaona sayari hiyo hadi baada ya saa moja na nusu hivi saa sita ya manane Mirihi itakapo jitokeza tena kutokea ukingo wa chini kushoto. Yaani tukio hili ni la kupatwa kwa sayari ya Mirihi.

Ramani hii inaonesha sehemu za Dunia ambako tukio hili litaonekana,
hasa bara la Afrika sehemu za mashariki, kati, na kusini.

1672338851873.png


Na picha hizi zinaonesha Mirihi itakavyokuwa jirani kabisa na Mwezi kuanzia saa 4:15 usiku na utakavyoonekana sayari itavyojitokeza mara baada ya saa sita usiku.
1672338944344.png


Tukio kama hili la kupatwa kwa sayari na kufichwa na Mwezi ni la nadra sana na hasa kwa vile linatokea wakati watu bado wapo macho na kulishuhudia.

Hauhitaji darubini au chombo chochote kufurahia tukio hili na halina madhara yoyote. Ni la kusisimua uelewa wa mambo ya angani. Ni rahisi kutambua Mirihi angani kwa sasa kwa vile inang’aa sana kutokana na kuwa jirani zaidi na Dunia na kuangaliana na Jua hivo huwezi kukosa kuona uwekundu wa Mirihi. Pamoja na hiyo siku ya tukio Mwezi utakuwa jirani na nyota hiyo nyekundu.

1672339057165.png


Jioni ya siku ya tukio, mara baada ya magharibi saa moja jioni anga imejaa sayari nne zilizopangika katika mstari mnyofu. Picha ya anga yote inaonesha mpangilo wa sayari na Mwezi katika mstari mmoja. Zuhura (Venus) itakuwa
jirani na upeo wa mahjaribi. Juu yake, angani kati ni sayari ya Zohali (Saturn) inayong’aa kwa ukali tulivu. Juu zaidi utaona karibu na utosi ni sayari angavu sana ya Mshtarii (Jupiter). Ukiendekea zaidi utosini upande wa mashariki
utaona Mwezi ukiwa jirani na Mirihi nyekundu.

Ufuatilie uone hali angani siku ya Jumanne tarehe 03 Januari na uweze kujenga dhana ya hasa kitu gani kinatokea angani wakati uaangilia Mirihi nyekundu inapofichikwa na Mwezi. Kaa macho kwa kuweza kuanglia tukio hili kwa darubini.

Imetolewa na Dr. N.T. Jiwaji, Astronomy and Space Science Association of Tanzania (ASSAT) ntjiwaji@yahoo.com
 
Kwa hiyo mwaka unaanza kwa mirihi na mwezi kufanya mashindano, tuombe isije kuwa jambo baya...
 
Back
Top Bottom