Chombo cha Marekani chakaribia jua kwa karibu zaidi

Hiki chombo kinazunguka nini hapo kilipo? Huu umbali na hii spidi hata kama ikiwa chai toka kwake beberu kuhakiki mbona shughuli.

Hawa wakisema tujikite kuengelea uchawi unaelewa, siyo wale wachumi uchwara. 🤣🤣

Hiyo ni picha ya kutengenezwa tu, maana hakuna kamera yenye kuweza kupiga picha ya namna hiyo iwe toka duniani au toka ISS
 
Mwaka 2018 Marekani walirusha chombo kuelekea anga za mbali katika harakati za kwenda karibu zaidi na jua , umbali ambao haukuwahi kufikiwa na chombo chochote kile duniani

Umbali wa miles millioni 4 chombo cha Parker solar probe kilisogelea jua na kuanza kuzunguka kwa ukaribu wa eneo hio huku kikifanya chunguzi mbalimbali za kisayansi ambazo zitakuja kutusaidia kuweza kulifahamu jua kwa undani zaidi

Nadhani unaweza ukajiuliza kitu au vitu vingi kuhusu uimara wa chombo na kuweza kuhimili joto kali linalozalishwa na jua letu

Chombo kimetengenezwa na material magumu kwa mbele ambayo yamefungwa madini ya aina ya carbon kwa mbele ambayo yanauwezo wa kuhimili mpaka joto la 2500 c na bado wakaweka mfumo wa kupoza vifaa vingi vilivyopo kwa nyuma na kwa ndani vifaa vyenyewe ni kama.computer na kamera ili zisiweze kupata joto la kuweza kuivisha vyombo hivyo

Baada ya kufika katika umbali huo basi chombo cha parker solar proble kiliongezeka kasi na mpaka kufikia kasi ya 200 kwa sekunde moja au 692,000 kilomita kwa lisaa ambapo kwa kasi hiyo chombo hakikuweza kuvutwa yaani kiliweza kupambana na kani ya uvutano wa jua letu na kama ingetokea kasi hiyo kutokufikiwa basi chombo kingepotea

[emoji625]Moudyswema [emoji625]Tanzaniascienceyetu [emoji625]AsteonomyKiswahiliView attachment 2507368
Hiyo picha imepigwaje?

Vilienda viwili?
 
NASA nao Kuna wakati ,hawaaminiki Kama NATO/marekani .anyway Kama kweli tunasubiri taarifa za huko kwenye jua.
 
Marekani kwa kamba tu, hamjambo
 
Hiyo picha imepigwaje?

Vilienda viwili?
Hiyo picha aliyesema imepigwa ni nani? Ushawahi kukutana na wale watu wanaotoa maelezo kuhusu taswira ya mtu fulani halafu kuna mtaalam anamchora huyo mtu? Maelezo yakikamilika picha ya huyo mtu inaonekana? Ndivyo ilivyo hapo, kwa kutumia calc na data za eneo chombo kilipo kulingana na info wanazopata(manamba namba tu) comp inauwezo wa kutengeneza taswira ya muonekano ambao ndo tunatumiwa ss vilaza wa mambo ya anga.
 
Sijui kwanini ss watanganyika tunapenda mambo mepesi mepesi.

Mfano: Mtanganyika ni rahisi kuamini dunia ni flat, na pale antactika kuna geti kubwa na hiyo siri hawataki tuijue kwa sababu ndicho anachoona siku zote dunia ni flat, na analijua geti. Ukianza mambo magumu yanayothibitika kimahesabu unaitwa muongo.
 
Hiyo picha aliyesema imepigwa ni nani? Ushawahi kukutana na wale watu wanaotoa maelezo kuhusu taswira ya mtu fulani halafu kuna mtaalam anamchora huyo mtu? Maelezo yakikamilika picha ya huyo mtu inaonekana? Ndivyo ilivyo hapo, kwa kutumia calc na data za eneo chombo kilipo kulingana na info wanazopata(manamba namba tu) comp inauwezo wa kutengeneza taswira ya muonekano ambao ndo tunatumiwa ss vilaza wa mambo ya anga.
Mkuu fahamu Msanii anafahamu dhima na deep knowledge ya sanaa pia hajaishi mbali na ulimwengu wa dijitali. Umeongelea zeros and ones yaani binary numbers ambazo ndo tafsiri ya kila tendo, text, picha, sounds ndani ya mfumo wa kompyuta......

Mada imekuja na picha. Picha haijawekwa label kuwa ni illustration au kielelezo sasa ulitaka sisi tutafsiri kuwa ni comp-gen image?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Jinsi unavyo sema hilo neno "uwongo" utadhani unafahamu hata meseji yako imefikaje humu jf.

Hao unao waambia waongo ndio wanao kufanya uongee na mjombaako mkoani wakati wewe upo kimbiji.
Kubali tu kwamba binadamu tunazidiana akili kwa mbali sana mkuu [emoji1787][emoji1787].
 
Mkuu fahamu Msanii anafahamu dhima na deep knowledge ya sanaa pia hajaishi mbali na ulimwengu wa dijitali. Umeongelea zeros and ones yaani binary numbers ambazo ndo tafsiri ya kila tendo, text, picha, sounds ndani ya mfumo wa kompyuta......

Mada imekuja na picha. Picha haijawekwa label kuwa ni illustration au kielelezo sasa ulitaka sisi tutafsiri kuwa ni comp-gen image?
Msanii, unataka kuhitimisha vp?
 
Wataalam watanielimisha ila Picha za space (With exception to hizi za rovers za mars, nadhani ni picha direct zinatumwa.) Nyingine ni comp generated.
Kwa mfano wanasayansi wanaotafiti anga za juu wanatuletea picha za galaxies pamoja na blackhole na milkway na kadhalika wakati tunajua sisi tupo ndani ya mfumo hivyo all are exaggerations.

Kwenye mwezi hawajafika lakini washatudanganya wamefika
 
Naomba kuuliza, hivi hawa wataalamu wanaotengeneza hivi vyombo na kuandaa plan nzima ya safari huwa wanasoma course zipi? hizo course hapa bongo kuna chuo kinafundisha?
 
Kwa mfano wanasayansi wanaotafiti anga za juu wanatuletea picha za galaxies pamoja na blackhole na milkway na kadhalika wakati tunajua sisi tupo ndani ya mfumo hivyo all are exaggerations.

Kwenye mwezi hawajafika lakini washatudanganya wamefika
Tunarudi palepale. Unatumia vigezo gani kusema unadanganywa? Kitu kikiwa comp gen kinakuwa ni uongo? Kwa vigezo vp?
 
Back
Top Bottom