SEHEMU YA 16
Mpenzi msomaji, sehemu iliyopita niliishia pale
Rhoda alipomuita Beka ambapo kijana huyo
aliduwaa kwa muda kwa kumwagiwa sifa
kibao. Je , kilifuatia nini? Songa nayo mdau
wangu. . .
Nakusikiliza Rhoda , Beka alijibu huku akiwa
na hisia fulani kwa msichana huyo ambazo
hakuwahi kuwa nazo tangu alipoingia katika
umri wa kikubwa a. k . a kubalehe . Hayo ndiyo
yalikuwa yakinisibu moyoni mwangu kwa
muda mrefu , kwa kifupi nakupenda , rafiki
zako akina Saidi, Jafari, Dan na wengine
wamekuwa wakinisumbua lakini nawakataa
kwa sababu moyo wangu umekupenda wewe ,
nipe nafasi moyoni mwako Beka , mtoto wa
kike alijieleza kwa hisia kali...
Kama unavyofahamu katika dunia hii hakuna
mtu asiyependa kusifiwa , Beka
aliyemwagiwa sifa kibao alifurahi sana na
kujitambua kwamba alikuwa handsome boy.
Beka : Nashukuru kwa kuniambia hisia zako ila
naomba kwenye saa moja au mbili kasoro
tuonane pale uwanjani kwenye goli la kusini ,
hata kama nitachelewa nisubiri na kama
nitawahi kufika nitakusubiri,
Msichana huyo alitamani kumrukia kwa
furaha lakini mazingira hayakuwaruhusu
akaishia kuporomosha bonge la tabasamu ,
akamshukuru Beka kwa kumkubalia ombi
lake . Kule ndani , mzee Kibandiko aliyekuwa
kafurahi kupita maelezo , aliinuka na kwenda
chumbani ambako alifungua waleti yake
iliyokuwa juu ya meza akatoa wekundu
mmoja wa msimbazi na kusema "lazima
awapatie Rhoda na Beka ili wagawane elfu
tano tano."
Akiwa na fedha hiyo , alipitia mlango wa uani
na kujifanya hakufahamu chochote kilichojiri
kati ya Rhoda na Beka .
Vijana hao walipomuona , walijifanya
wanajisomea, mzee huyo alitamani kucheka
lakini akapotezea na kusogea pale
kibarazani. Naona mnajisomea ! aliwaambia.
Kama vile waliambiana wajibu kwa pamoja ,
wakasema ndiyo,, ndipo mzee Kibandiko
akasema walimfurahisha sana, akatoa ile
noti ya shilingi 10,000 na kumpatia Beka na
kumwambia wagawane hiyo ilikuwa ofa yake
kwao .
Beka ambaye ilikuwa nadra kupewa fedha
kubwa kiasi kile alipigwa butwaa na
kumshukuru mzazi wake akifuatiwa na
Rhoda aliyepiga magoti na kumshukuru mzee
huyo.
Msijali wanangu , leo mmenifurahisha mno ,
mimi huwa napenda sana watoto
wakielewana na kujisomea pamoja kama
mnavyofanya,
Beka na Rhoda ambao hawakujua mzee huyo
alimaanisha nini walifurahi, lakini kabla mzee
Kibandiko hajaondoa alimtania Rhoda "aangaliaBeka asimpunje hela yako"
Rhoda alicheka na kusema :
"Beka hawezi kufanya hivyo kwani
ni kijana mzuri"
Mzee kibandiko : "aaahh nakutania mwanangu"
Kitendo cha Rhoda aliyekuwa na akili za
ziada kutoa kauli hiyo , Beka hakujua alichomaanisha Rhoda badala yake alifurahi mno
kufagiliwa kwa mzazi wake kwamba
mzee Kibandiko aliwaacha Beka na
Rhoda wakiendelea kupiga stori akaingia
ndani huku akiimba wimbo wa Lucy Bandawe
uliopigwa na Ottu Jazz Band ambao moja ya
shairi lake linasema Lucy Bandawe. . . Lucy
wangu nampenda !
Mkewe aliyemfahamu vizuri mumewe
alipofurahi alikuwa na kawaida ya kuimba
hasa wimbo huo,
Mama beka : "eeehh bab umefurahishwa na nin..!??"
Mzee huyo alicheka na kumwambia kuna
jambo lilimfurahisha sana muda ule angemwambi baadaye .
Kwa kuwa mkewe alikuwa bize na mapishi
na shughuli zingine za jikoni , aliishia
kutabasamu kisha alimwita Beka ili amtume
dukani.
Beka alipoitika na kutaka kwenda kumsikiliza
mama yake , mzee Kibandiko alimuuliza
mkewe alimuitia nini mtoto aliyekuwa
akijisomea na mwenzake?
Nataka nimtume hapo dukani mara moja ,
mama huyo alimwambia mumewe .
Kufuatia mkewe kutoa kauli hiyo , mzee huyo
alimwambia Beka aendelee kujisomea kisha
alimuuliza mkewe alitaka kumtuma nini ili
aende yeye kwa sababu hakuwa na kazi
yoyote.
Mkewe alicheka na kumwambia mumewe
kwamba kweli siku hiyo alifurahi mpaka
kuamua kwenda dukani kununua chumvi na
dawa ya meno !
Wewe lete hiyo hela niende, kwanza ni moja
ya mazoezi si unaona kitambi
kinaninyemelea? alimwambia mkewe.
Alipotoa kauli hiyo mkewe aliendelea
kucheka na kumwambia atumie hela
aliyokuwanayo mfukoni mwake, baba Beka
akamwambia anataka ampe hela ya bajeti
aliyomuachia , huku mkewe akicheka
alimpatia shingili elfu mbili ndipo mzee huyo
akaelekea dukani.
Mh! Hii furaha siyo bure, huenda atakuwa
kapandishwa cheo kazini au kuna dili lao
limekwenda vizuri, na ninavyomfahamu
anavyopenda kufinyana anapokuwa kafurahi ,
leo usiku mbona shughuli ninayo mie!
mkewe aliwaza na kuachia tabasamu.
Kule nje Rhoda alimwambia Beka kwamba
hakutegemea kama baba yake alikuwa mtu
poa namna ile ; Yaani katupatia ten moja
kwa sababu ya kujisomea tu , hivi akisikia
umefaulu si atakufanyia mambo makubwa
zaidi ?
Si nilikuambia siku ile , ila akichukia ni balaa ,
juzi kanilamba bakora sina hamu naye ,
Beka alimwambia Rhoda.
Eh ? Ulifanya kosa gani ? Kwanza siamini
kama unachosema kina ukweli mbona mshua
wako mpole , mcheshi na mpenda utani ?
Rhoda alimwambia Beka .
Tukikutana baadaye nitakuambia sababu ila
elewa akichukia kaa naye mbali , Beka
alimwambia Rhoda, wakacheka .
Rhoda aliyekuwa amemuweka sawa Beka
ambaye awali hakuwa kabisa na hisia za
mapenzi juu yake , alimuaga kijana huyo na
kumwambia kwamba anakwenda kupika
hivyo wangeonana uwanjani kama
walivyokubaliana.
I TAENDELEA HAPA HAPA
WABALLA Inc miss nuru manju Lmntrix belie MO11