Chombezo: Chachandu za Beka wa Tanga

Chombezo: Chachandu za Beka wa Tanga

SEHEMU YA 11

sehemu iliyopita niliishia pale
mzee Kibandiko aliyekuwa akifuatilia
mazungumzo kati ya kijana wake na Rhoda
binti aliyeonesha kumpenda Beka lakini Beka
hakuwa na habari naye jambo lililomkera
sana mzazi wake na kumwita ----- . Je ,
kilifuatia nini? Songa mbele na uhondo huu. . .
ale kibarazani , Beka alimuaga Rhoda lakini
msichana huyo aliyekuwa na shepu tata na
kila alipotabasamu vishimo vilitokea kila
upande wa mashavu yake , aliendelea
kumbembeleza amsindikize japo kidogo .
“ Rhoda kama nilivyokuambia nataka
kumsaidia mama kuchota maji wewe nenda
tu ila nashukuru kwa kunitembelea maana
haijawahi kutokea , ” Beka alimwambia Rhoda.
“ Haijawahi tokea nini?” Rhoda alimuuliza.
“ Si kupiga stori na msichana kwa muda wote
huo, tena kama mama ametusikia tukiongea
lazima ataniuliza , ” Beka alimwambia Rhoda .
“ Atakuuliza nini, kwani yeye hapendi
wakamwana?” Rhoda alimuuliza Beka .
Kufuatia msichana huyo kumuuliza hivyo
Beka , mzee Kibandiko aliyekuwa akisikiliza
kila walichoongea alitabasamu na kumfagilia
sana Rhoda . “ Huyu binti ana akili na
kampenda sana mwanangu , sema Beka
mwenyewe haelewi chochote , waliosema
penye miti hapana wajenzi hawakukosea , ”
mzee huyo aliwaza .
“ Rhoda, suala la mama kuhitaji wakamwana
halipo na kwa upande wangu sihitaji kuwa na
msichana , mimi ni mwendo wa kujisomea tu
mpaka kieleweke, ” Beka alimwambia .
Kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda na
msichana huyo kuhitajika kwenda kupika
kwao , akiwa mnyonge alimuaga Beka na
kuahidi wangekutana siku nyingine,
akaondoka.
Njiani Rhoda alijisemea kwamba kwa jinsi
vijana wenye rika la Beka walivyokuwa
wakimsumbua kumtaka kimapenzi na licha
ya kumuonesha dalili za kumpenda Beka na
kijana huyo kuwa na domo zege, alikuwa na
tatizo tu !
“ Si bure, yaani nimemfuata mpaka kwao na
kumuonesha hisia zangu lakini kashindwa
kunitokea , yule atakuwa mgonjwa ila
nitafanya kila njia kujua kama yupo fiti au la, ”
Rhoda alijisemea moyoni .
Huku nyuma baada ya msichana huyo
kuondoka, Beka aliingia ndani na kukutana
koridoni na baba yake ambaye alimkata jicho
na kwenda kukaa sebuleni.
Beka aliyemjua vizuri mzazi wake
anavyokuwa akikerwa na jambo akawa
anajiuliza alikuwa kaharibu wapi bila
mafanikio.
“ Mbona sikumbuki kama kuna kazi alinipatia
sijaifanya, nitakuwa nimekosea wapi ?” Beka
aliyekuwa ameketi chumbani kwake alijiuliza .
Akiwa anatafakari hivyo , aliona mlango wa
chumba chake ukifunguliwa kisha baba yake
aliingia na kusimama katikati ya kitanda na
mlango .
Kwa jinsi mzee huyo alivyokuwa, moyo wa
Beka ukapiga paa kwani alijua alikuwa
kaharibu tu mahala na kwa akili ya fasta
alijua baba yake hakupendezwa na ujio wa
Rhoda pale nyumbani kwao .
“ Baba nahisi nimekukosea naomba
unisamehe , ” Beka alimuwahi mzazi wake .
“ Umenikosea nini?” mzazi wake alimuuliza.
Beka alimwambia kitendo cha kumkuta
akizungumza na Rhoda pale kibarazani ,
mzazi wake akamwambia hakuwa na tatizo
na Rhoda isipokuwa alikuwa anataka kujua
kwa nini alikuwa hasafishi banda la mbwa .
Kufuatia kuulizwa hivyo , Beka aligundua ni
kweli alipitisha siku moja bila kusafisha
banda hilo lakini kabla hajajitetea mzazi
wake alimdaka na kwenda naye sebuleni.
Alipofika sebule alichukuwa fimbo aliyoificha
chini ya kiti na kuanza kumtandika Beka ,
Beka akaanza kulia .
“ Leo utanitambua, sipendi kijana
mzembemzembe hata kidogo, ” mzee
Kibandiko aliendelea kumtandika Beka bila
kijana wake kujua kama sababu haikuwa
kutofagia banda la mbwa isipokuwa
kushindwa kumtokea Rhoda aliyejileta
nyumbani kwao bila kuitwa.
Huku akimtandika moyoni alikuwa akisema :
“ Wewe mtoto mjinga sana , binti mzuri kama
Rhoda kajileta mwenyewe wewe unashindwa
kumpa maneno matamu unamwambia
unataka kumsaidia mama yako kuchota maji,
si upuuzi huo?”
ITAENDELEA HAPA HAPA

WABALLA Inc miss nuru Lmntrix
 
Haya saaa, mission one ya kujua kama beka ni mzima imetick! duuuh...
.
.
Ila paliponifurahisha ni pale mzee kibandiko anamtandika beka na kusingizia kwanini hajasafisha ka Dogie..kumbe kakasirika kuwa BEKA ni DOMO ZEGE ,,aiseee its so funny two in one!!
.
.
Hapo nabaki nikijiuliza , Je mzee kibandiko atatafuta suluhu ya huo UDOMO ZEGE wa mwanae!!??
Na je chachandu zitahusika katika jambo hilo!!?
Am just curious nijue kwanini beka ana chachandu .....
Mkuu VAN HEIST keep it up.. Hadithi nzuri hii!!!
 
Last edited by a moderator:
Nilipofika sehemu ya mzee Kibandiko anamchapa Beka,nimejikuta nacheka mwenyewe kwa sauti mpaka watu wakanishangaa,
 
SEHEMU YA 12

Mpenzi msomaji ,sehemu iliyopita niliishia pale
mzee Kibandiko alipomsifia mkewe kwamba
alikuwa mwanamke mrembo asiyechuja . Je ,
mama huyo aliposifiwa alisemaje ?
Songa nayo …
“ Asante , hata wewe ni mwaume wa shoka ,
unajua kunitunza na kunifikisha pale
ninapopataka, ” mama Beka alimwambia
mumewe . “ Nashukuru mke wangu kama
umeligundua hilo, hata hivyo nisipokupa raha
mimi akupe nani?” Mzee Kibandiko
alimwambia mkewe na kuweka kikombe cha
tangawizi mezani .
“ Umeona eh ?” mkewe alimsapoti ,
wakacheka . Mzee Kibandiko aliyekuwa
kamaliza tangawizi iliyokuwa kwenye
kikombe, alinyanyua miguu na kulala chali
kitandani , wakaendelea kupiga stori.
“ Mama Beka nikuulize kitu ?” mzee huyo
alimwambia mkewe.
“ Uliza hata maswali mia yakiwa ndani ya
uwezo wangu nitakujibu , ” alimwambia .
Mzee Kibandiko alipoambiwa hivyo , alicheka
na kumweleza mkewe atupie macho dirishani
kulikuwa na mtu alikuwa akiwachungulia.
Mkewe alipofanya hivyo hakumuona mtu na
alipogeuza macho kumtazama mumewe
alishangaa alipomuona kafungua taulo na
kubaki mweupe pee !
Mama Beka alicheka na kumfuata mumewe
akampiga kibao chepesi kwenye paja na kwa
sauti nyororo alimuuliza ndilo swali alilotaka
kumuuliza!
“ Kwani wewe ni dada yangu, upo hapa kwa
ajili ya kunifurahisha nami nikufurahishe ,”
mzee huyo mpenda mahabati alimwambia
mkewe kisha alimvutia kifuani kwake .
Mama huyo akiwa kajaa tele kifuani kwa
mzee huyo wa mjini, mumewe akaanza
kuuterezesha mkono wake wa kulia maeneo
mbalimbali yenye shoti ya umeme.
Wanandoa hao waliendelea kuleteana fujo
hadi kila mmoja akaiva , mama Beka
alipotupia macho mlangoni alibaini
hawakuufunga, akaamka kichovu kwenda
kuufunga. Wakati akifanya hivyo alikuwa
kabaki na skeni taiti nyeupe , mumewe
alipoangalia hipsi na bambataa la mkewe
lilivyokuwa limenona , akawa anameza
mafunda ya mate mfululizo .
Mama huyo alipofunga mlango alimalizia
kiwalo chake cha mwisho , akajongea kwa
mumewe aliyempokea kwa mikono miwili
kama wakuu wa mikoa wanavyokabidhiana
Mwenge wa Uhuru mpakani mwa mkoa
fulani unapomaliza mbio zake .
Kwa kuwa hakuna kitu alichokipenda kabla
ya kulicheza segere kama kula mua a. k . a
denda , alimpa mumewe nyama ya ulimi naye
bila noma akaipokea. Wawili hao ambao
wakati huo hawakuwa na habari kabisa na
kijana wao Beka zaidi ya kazi iliyokuwa
mbele yao, walipagawishana si kidogo na
mwishowe walizama kwenye kisiwa cha
wapendao na kupeana raha ya dunia .
“ Ila wewe baba Beka wewe!” Mama Beka
ambaye muda huo alikuwa hoi alimwambia
mumewe .
“ Mimi nini?” Baba Beka alimuuliza. “ Si hivi
unavyonifanyia !” alimwambia .
“ Nakufanyia nini?” mkewe alimuuliza.
Kufuatia kuulizwa hivyo alimwambia kuhusu
tabia yake ya kupenda kunaniliu mchana
hata kama kijana wao yupo.
“ Tatizo liko wapi , kwani tunakutana
hadharani… halafu elewa kwamba wewe ni
mke wangu hakuna mtu yeyote hapa duniani
atakayenipangia muda wa mimi kuwa na
wewe, ” mzee huyo alimwambia mkewe.
“ Ni kweli unachosema lakini kumbuka Beka
amekua kitendo cha sisi kujifungia ndani
mapema yote hii atajua kinachoendelea , siyo
vizuri bwana!” mkewe alimwambia .
“ Tena akijua ndiyo safi, itamsaidia
kuchangamka , toto gani wenzake wote wapo
shapu yeye ni kukaa tu hapa nyumbani
utafikiri padri , ” baba Beka alimwambia
mkewe.
“ Baba Beka maneno gani hayo , unaacha
kumshukuru Mungu mwananetu katulia
wewe unataka afanye mambo ya kipuuzi ?”
mama huyo alimwambia mkewe.
“ Kuwa na demu ndiyo upuuzi, kwa taarifa
yako mtoto wa kiume kama yeye kukaa
nyumbani na kuchotachota maji ndiyo upuuzi
mkubwa, mtoto wa kiume hatakiwi kuwa
kama Beka , ” baba Beka alimwambia mkewe.
“ Haya bwana wewe muombee mtoto mambo
yasiyofaa, siku akianza kukuletea kesi za
kuwapa mimba watoto wa watu ndiyo akili
itakaa sawa , ” mama huyo alimweleza
mumewe .
“ Hicho ndicho ninachokitaka , mimi nataka
wajukuu hata wakwe zangu wakifika mia
moja mhusika akiwa Beka nitawalea , ” mzee
huyo alimwambia mkewe.
Kufuatia kauli hiyo , mama Beka aliishia
kucheka kisha alimwambia mumewe kwamba
alishinda waachane na maongezi hayo .
Je , baada ya mama huyo kutoa kauli hiyo
mumewe alijibuje ?
ITAENDELEA HAPA HAPA

WABALLA Inc miss nuru Lmntrix
 

Naona ka sehemu ya 10 na 11 zinafanana halafu 12 kama vile kuna part imemis from 11
 
Naona ka sehemu ya 10 na 11 zinafanana halafu 12 kama vile kuna part imemis from 11

nilichanganya sehemu ya 10 kwa 11 nimeshaweka sawa.. part iliyomis ni kwamba baada ya kumchapa beka akamwacha aende kusafisha banda la mbwa na yeye akarudi kwa mkewe kutokana na uzuri wa mkewe hasira zote zikapoa wakajikuta wanafanya majamboz...
 
story nzuri ila inachosha.... inaelekea unajifunza!! watu wawil wakiwa wanaongea weka conversation, sio kila akiongea beka unasema beka aliongea mara baba beka alimjib wakati tunajua watu wako wawil, weka majina panapotakiwa, sio kila sentensi.... ni ushari tu.
 
story nzuri ila inachosha.... inaelekea unajifunza!! watu wawil wakiwa wanaongea weka conversation, sio kila akiongea beka unasema beka aliongea mara baba beka alimjib wakati tunajua watu wako wawil, weka majina panapotakiwa, sio kila sentensi.... ni ushari tu.

nitajaribu kuedit maana mimi sio mtunzi... ni msimuliaji tu
 
SEHEMU YA 13

Mpenzi msomaji , sehemu iliyopita niliishia pale
aliposisitizia mkewe kwamba anahitaji kijana
wake Beka achangamke kisha alimuuliza ‘ wife ’
wake huyo kama alimwambia asante kwa raha
aliyompa.
Je , baada ya kumuuliza hivyo mkewe
alisemaje? Twende mdodomdogo…
Kufuatia mama huyo kuulizwa hivyo alicheka
na kusema :
“ Si tayari umemaliza shida yako kwani
asante ina umuhimu?”
Kufuatia dongo alilorushiwa na mkewe, mzee
huyo alimvutia mkewe maungoni mwake
akambusu na kumwambia asante kwa kumpa
raha.
“ Nami nakushukuru mume wangu kwani
unanipatia sana na kuniacha hoi… kwa hilo
jiandae kupokea zawadi yangu, ” mama Beka
alimwambia mumewe , wakacheka .
“ Zawadi gani mama?” Baba Beka akamuuliza
mkewe.
“ Wewe subiri utaiona siku hiyo , usiwe na
haraka besti , ” mkewe alimwambia mumewe ,
wakacheka .
Baada ya utani wa hapa na pale, mama
Beka aliingia bafuni akaoga kisha akatoka na
kumuacha mumewe akiwa kajipumzisha .
Jioni wakiwa wamemaliza kula wakiwa
wameketi sebuleni, mzee huyo alimuita Beka
aliyekuwa anajisomea na kumwambia
kwamba huwa hapendi kumchapa ila aache
uzembe .
Beka ambaye hakufahamu kama alichapwa
kwa sababu alishindwa kumtokea Rhoda
aliahidi kuwa makini na atahakikisha
anafanya usafi kwenye banda la mbwa kila
siku.
Kufuatia kauli hiyo , baba yake alicheka
kwani alipomsisitiza aache uzembe , moyoni
alimaanisha kuwatokea mademu lakini kijana
wake hakujua hilo.
“ Hivyo ndivyo inatakiwa kufanya , mtoto
akikosea mwelekeze kwa kumuambia lakini
siyo unamchapa, ” mama Beka alimwambia
mumewe .
“ Kama hasikii viboko ndiyo dawa yake , ”
mzee huyo alimuambia mkewe.
Muda wa kulala ulipowadia, Beka alikwenda
chumbani kwake na wazazi wake walikwenda
chumbani kwao .
Kulipokucha Beka alikwenda shuleni, baba
yake kazini na mama yake ambaye hafanyi
kazi alibaki nyumbani .
Siku hiyo Beka alichelewa kurudi nyumbani
jambo ambalo halikuwa kawaida , na
aliporejea mama yake alimuuliza
alikochelewa .
“ Kuna mwalimu mgeni kaanzisha darasa la
tuisheni , hivyo mimi , Jacob , Jully , Sara na
wanafunzi wengine tulibaki kwa ajili ya
kujifunza, ” Beka alimwambia mama yake .
“ Hapo mwanangu ndipo unaponifurahisha,
soma ipo siku utakuja kuwa mtu mwenye
madaraka makubwa hapa nchini, ” mama
huyo alimwambia mwanaye .
Kwa kuwa Beka alipenda sana kumsaidia
mama yake kazi za nyumbani , alipomaliza
kula alimuuliza mama yake kama kulikuwa
na kazi ya kufanya akamwambia apumzike
tu .
Beka aliyependa kukaa kibarazani kwao ,
alipoambiwa hivyo alizunguka nyuma na
kukaa juu ya ukuta wa kibaraza .
Haukupita muda mrefu , alimuona Rhoda
akiwa amekaribia alipokuwa , akamkaribisha ,
ingawa hakuwa mtu wa mademu alijikuta
akivutiwa na mavazi aliyovaa msichana
huyo.
“ Karibu Rhoda , halafu hizo nguo ulizovaa
zimekupendeza sana, ” kwa mara ya kwanza
Beka akamsifia msichana huyo japo hakuwa
na lengo la kumtaka kimapenzi.
“ Jamani asante Beka , hata hivyo nimevaa
kawaida mbona !” Rhoda alimwambia .
Beka alimwambia Rhoda kwamba hata kama
alivaa kawaida lakini alipendeza , msichana
huyo akasema asante .
Wakati Rhoda na Beka wakipiga stori, mzee
Kibandiko aliyekuwa kazini aliwasili na
kuwakuta pale kibarazani kama ilivyokuwa
siku ya kwanza kumuona Rhoda pale
nyumbani kwake .
“ Shikamoo baba na pole kwa kazi , ” Beka
alimwamkia baba yake .
Kabla yam zee huyo hajaitikia salamu ya
kijana wake , Rhoda naye alimwamkia ndipo
mzee huyo aliitikia salamu zao kwa pamoja .
“ Naona Beka umepata mgeni , safi sana
mnapotembeleana na kubadilishana
mawazo, ” mzee huyo alimwambia kijana
wake .
“ Nashukuru baba , kwani tunataka kujisomea
pamoja kwani mitihani imekaribia , ” Bela
alimwambia mzazi wake .
“ Hilo ndiyo tatizo la mwanangu , yeye kila
wakati anawaza kujisomea badala ya
kuuangasha mbuyu , hebu kaangalie kabinti
kalivyo kazuri , hii ni sheedaaa kweli, ” mzee
huyo alijisemea moyoni.
Akiwa amesimama mlangoni , alimtania
Rhoda kwamba anafaa sana kuwa mkwewe
kwa jinsi walivyopendezana na Beka , Rhoda
aliishia kucheka huku akiangalia chini kwa
aibu.
Mzee Kibandiko alipoingia ndani, Rhoda
aliachia tabasamu pana ndipo Beka
akamuuliza alifurahishwa na nini.
Je , baada ya Rhoda kuulizwa hivyo alijibu
alijibuje?
ITAENDELEA HAPA HAPA

WABALLA Inc Lmntrix miss nuru
 
hahahahaa,huyo mzee Kibandiko anaweza kumtongozea Rhoda kwa Beka,maana anawaza uroda muda wote!
 
SEHEMU YA 14

Mpenzi msomaji , sehemu iliyopita niliishia pale
Mzee Kibandiko alipoingia ndani baada ya
kumtania Rhoda kwamba anafaa kuwa
mkwewe kwa jinsi walivyopendezana na Beka
ambapo msichana huyo alitoa tabasamu pana
ndipo Beka akamuuliza alifurahishwa na nini?
Songa mbele . ..
Rhoda aliuliza "baba yako , kumbe anapenda utani eh ?
Beka : kama nilivyokuambia siku ya kwanza kwamba
baba yangu anapenda sana mizaha na pia ni mcheshi .
Rhoda :“ Leo nimeamini , si ulimsikia alivyosema
nafaa kuwa mkwewe kwa vile
tunapendezana ?”
beka: “ Wewe utamuweza baba yangu kwa utani ,
tena ilibakia kidogo angekwambia nguo
ulizovaa zimekupendeza sana ,” wote wakacheka .
Kufuatia kauli hiyo ya Beka , Rhoda
alimweleza asingeweza kutoa kauli hiyo kwa
sababu kidesturi mimi naweza kuwa
mkwewe .
beka: “Mkwewe kwa nani ?”
Rhoda: “ Si kwako, kwani wewe huwezi kunioa mimi ?”
Rhoda alimtupia swali Beka bila kujua kama
mzee Kibandiko alikuwa akiwasikiliza kupitia
dirishani.
beka: “ Mimi mambo hayo sitaki kuyasikia kwa kwa
sasa , nataka kusoma kwa kwenda mbele ,”
Beka alimwambia Rhoda ambaye alikosa
raha ghafla.
Kule ndani mzee kibandiko aliposikia kauli hiyo ya
mwanaye alikunja sura na kujisemea moyoni
“ Huyu anataka bakora tena, tena
leo nitamtandika na kumweleza kwa nini
nimemtandika , siwezi kuvumilia upuuzi
wake . ”

Rhoda aliamua kufunguka :Kwani Beka watu wakisoma ndiyo hawaoi au
kuwa na wapenzi , mbona ukiamua tunaweza
kuwa pamoja huku tukiendelea kusoma?”
Kauli ya Rhoda ilimpa raha sana mzee
Kibandiko na kujisema moyoni kwamba
atafanya kila awezalo amtafutie Rhoda
zawadi yoyote .
Beka : “ Mimi mambo hayo hapana tena mama
akikusikia anaweza kukufukuza kabisa hapa
nyumbani , ukitaka afurahi atukute
tunajisomea, ”
Wakati wanaendelea kupiga stori, baba Beka
aliyekuwa amekasirika aliinuka na kwenda
stoo ambako kulikuwa na fimbo za mifagio
ya nje akachukua moja .
Wakati akitafuta fimbo hiyo mkewe
aliyekuwa jikoni ambaye hakujua kama
mumewe alirejea , alisikia kama kuna mtu
alikuwa akitafuta kitu stoo akafikiria ni Beka .
Kutokana na kumpenda sana mwanaye
aliamua kumfuata ili kujua alikuwa akitafuta
nini ili amsaidie , ile anafungua mlango wa
kwenye korido akamuona mumewe kashika
fimbo.
“ Mwenzangu, umerudi saa ngapi na hiyo
fimbo ya ufagio ya nini?” alimwuliza .
ingawa mzee huyo alikuwa na hasira ,
alimdanganya mkewe kwamba alipoingia
chumbani alimuona panya hivyo alitaka
kumsaka na kumuua .
“ Halafu na wewe baba Beka kwa ubishi
ndiyo mwenyewe , kila siku nakuambia ziba
hilo tundu kwenye mlango hunielewi , yaani
chumba kimegeuka uwanja wa panya!”
Aliongea mama huyo bila kujua kama
mwanaye Beka asingemaliza siku hiyo bila
kula bakora .
mzee kibandiko : “ Itabidi kesho nimuite fundi alizibe , ” mzee
huyo alimwambia mkewe.
Baada ya kumaliza mazungumzo kuhusiana
na panya , mkewe alimpa pole ya kazi akashangaa baada ya kujibiwa ilikuwa nzuri kiasi
“ Kwa nini kiasi ?” alimwuliza .
“ Siku hazifanani tu , hivi mwanao kafagia
banda la mbwa ?” mzee huyo badala ya
kumweleza mkewe kilichojiri kazini
akamchomekea swali . “ Nafikiri atakuwa
kasafisha, ngoja nitamuuliza akimaliza
kujisomea, ” mama huyo alimwambia
mumewe .
Kwa kuwa alimdanganya mkewe kwamba
chumbani kwao kulikuwa na panya, aliingia
na kujifanya anamsaka lakini moyoni alisema
lazima Beka atamtambua hata kama
atakuwa kasafisha banda la mbwa
atamtafutia sababu ya kumcharaza bakora
tena.
Mama Beka alimshauri mumewe wakati
akimsaka panya huyo azibe lile tundu ili
asitoke kisha alikwenda jikoni kuandaa
tangawizi ambayo baba Beka alikuwa
akipenda kunywa aliporejea kutoka kazini .
Hata hivyo , hakukaa muda mrefu mle
chumbani alitoka na kwenda kuketi sebuleni
kusikiliza maongezi ya kijana wake na
Rhoda.
“ Vipi umeshindwa kumpata ?” mama Beka
alimwuliza mumewe baada ya kumkuta
ameketi sebuleni.
Kufuatia sauti ya mama huyo kuwafikia akina
Beka , vijana hao walipunguza sauti ambapo
Rhoda alimwuliza Beka kama mama yake
hakuwa na noma .
Beka: Kwa kuwa tupo hapa kwa ajili ya kujisomea
hana shida, yeye hapendi mambo ya kipuuzi
tu ! î
Mambo ya kipuuzi ndiyo mambo gani ? Rhoda
alimwuliza .
Kama ya wanawake na kuwa na marafiki
wasiozingatia maadili , î Beka alimwambia .
ìWewe Beka na huyo mama yako mh ! Hivi
hujui kama hivi sasa umekua unafaa kuwa
na rafiki wa kike kama mimi ?î Rhoda
alifunguka .
ITAENDELEA HAPA HAPA

WABALLA Inc miss nuru belie Lmntrix
 
SEHEMU YA 15


Sehemu iliyopita ;Mambo ya kipuuzi ndiyo mambo gani ?”
Rhoda alimuuliza.
“ Kama ya wanawake na kuwa na marafiki
wasiozingatia maadili , ” Beka alimuambia.
“ Wewe Beka na huyo mama yako mh! Hivi
hujui kama hivi sasa umekua unafaa kuwa
na rafiki wa kike kama mimi ?” Rhoda
alifunguka . songa nayo sasa...
Licha ya Rhoda kujitahidi kumshawishi Beka
lakini kijana huyo hakuonesha dalili kama
alikuwa na hisia za mapenzi na msichana
huyo, akamuambia wakati ukifika ataoa
kabisa siyo kurukaruka kama chura na kila
msichana .
Kufuatia kauli hiyo , Rhoda alicheka na
kumuambia Beka kwamba dunia ya sasa
imebadilika siyo kama ya wazazi wetu
ambao waliogopa kujaribu baadhi ya mambo .
beka :“ Kujaribu mambo gani?”
Rhoda aliangua kicheko na kusema :
“ Mfano unapoambiwa usijihusishe na
masuala ya mapenzi sasa utayafahamu vipi
bila kujihusisha nayo?”
Msichana huyo huku akiwa hajui kama
kulikuwa na mtu alikuwa akiwasikia ,
alimuambia Beka kwamba hakuona kikwazo
cha wao kuwa wapenzi kikubwa ni kuwa
makini.
beka: “ Kuwa makini kivipi, yaani Rhoda hujatulia
kabisa wewe !”
Wakati wakiendelea na stori hizo , mzee
Kibandiko aliyekuwa amekaa kwenye sofa
lililokuwa dirishani kwa ndani, alimfagilia
sana Rhoda .
“ Huyu binti ana akili sana, anakoelekea
atamuweka sawa tu huyu ----- wangu,
kijana gani anashindwa kumuelewa
mwenzake mpaka amuambie kabisa kwamba
wakananiliu ndiyo atamuelewa?” mzee huyo
aliwaza.
“ Beka nimevumilia muda mrefu nikifikiri
utanielewa na kucheza na hisia zangu lakini
mwenzangu huoneshi dalili zozote za
kunihitaji, ngoja nikuambie la moyoni ,” Rhoda
aliendelea kufunguka,
Kule ndani mzee Kibandiko kidogo aruke juu
kwa furaha kwani alielewa Rhoda alitaka
kumueleza moja kwa moja Beka kwamba
alimpenda .
“ Huyu binti leo lazima nimpe hela ya
matumizi, ngoja nisikilize anachotaka
kumuambia huyu domo zege wangu, ” mzee
huyo aliyekuwa akimuita majina ya ajabu
mwanaye aliwaza .
“ Sikiliza Beka , hivi tangu unifahamu
umeshawahi kuniona nahangaika na
wavulana hapa mtaani?” Rhoda alimuuliza .
beka: “ Sijawahi!”
Rhoda aliendelea kuchombeza:“ Unajua kwa nini sina taimu nao ?”
beka:“ Mimi sijui bwana!”
Kufuatia kuambiwa hivyo , Rhoda alimueleza
Beka kwamba chaguo lake alikuwa yeye na
kwamba alikuwa akimpenda sana kwa
sababu nyingi .
Rhoda hakutaka kumpa beka nafasi ya
kuzungumza kabla ya kumaliza,
alimuambia kwanza alikuwa handsome boy,
mpole , mtanashati , alipenda kujisomea.
Aliendelea kummwagia sifa kwamba ukiacha
sifa hizo , hakuwa bize na mambo ya
wasichana kama wenzake , alipenda
kumsaidia mama yake kazi za nyumbani na
alikuwa na macho mazuri .
Kule ndani kila Rhoda alipommwagia sifa
Beka , mzee kibandikoa alitikisa kichwa kwani
aliamini asingeweza kuchomoa na kujisemea
moyoni kwamba kama angemjibu tofauti
msichana huyo siku hiyo angemtimua pale
nyumbani .
“ Kwa hatua aliyofikia huyu binti Beka
asipomuelewa, kwanza atakula bakora
zakutosha kisha namtimua hapa nyumbani ,
sitaki ujinga mimi ,” mzee huyo aliwaza .
“ Beka , ” Rhoda alimwita Beka aliyekuwa
ameduwaa kwa muda baada ya kumwagiwa
misifa kibao. Je, beka ataingia line baada ya sifa hizo??
ITAENDELEA HAPA HAPA

WABALLA Inc miss nuru Lmntrix
 
Back
Top Bottom