choma kadi ya ccm kuelekea Uhuru kamili

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
Maisha yetu yamekua magumu haina haja tena kumiliki hizi takataka, na kila mwenye nayo aichome moto ili tuwe wasafi tunapoenda kuanza harakati za kupigania/kudai uhuru wa pili wa watu wa Jamhuri ya Tanganyika.
301672_265200096857214_100001016768117_788943_724941653_n.jpg
 
Duuuh! hii kali!! Hivi hasira hizi zilizojaa kwenye vifua vya watu siku zikitoka nje kuna kitu kitabaki?????
 
Duuuh! hii kali!! Hivi hasira hizi zilizojaa kwenye vifua vya watu siku zikitoka nje kuna kitu kitabaki?????
watu wetu wamechoka sana, kwakweli wanahitaji ukombozi wa pili , wanahitaji kupambana kuondoa mfumo legelege wa ccm ambao umewaletea madhila yote haya.
 
Maisha yetu yamekua magumu haina haja tena kumiliki hizi takataka, na kila mwenye nayo aichome moto ili tuwe wasafi tunapoenda kuanza harakati za kupigania/kudai uhuru wa pili wa watu wa Jamhuri ya Tanganyika.
301672_265200096857214_100001016768117_788943_724941653_n.jpg
nguvumali, hasira za nini?, hasira hasara!.
Kwanza sio ustaarabu kuchoma moto kadi ya chama chochote, huu ni uhuni!.
Pili hata ukiichoma, chama kilichokupatia hiyo kadi, kitaendelea kujivunia uanachama wako maana jina lako linakuwa bado lipo kwenye register ya yao ya wanachama, hivyo the right forum ni ama kujitoa kwa kuwarudishia kadi yao, ama kujiunga na chama kingine kwa kuikabidhi hiyo kadi huko kwingine na hivyo kuwa sio mwanachama wa chako chako.

Angalizo, kwenye siasa, hakuna urafiki wa kudumu wala uadui wa kudumu, wako wengi kama wewe walkiofikiri siasa ni shibe, hivyo walikasirika na wakahama kwa mbwembwe na majigambo kibao, siku ya siku, njaa zikawazidia huko walipo na ni kwa kuendekeza hizo njaa zao, wakarudi walikotoka na sasa ni wapayukaji wakuu huku wakichumia tumbo!.
 
Bahati mbaya mimi sina hiyo kitu ningeichomelea mbali... Hivi zinatolewaga wapi nami nikachukue moja niichomelee mbali?
 
Ngoja mie nikatafute ya kwangu niipige kiberiti!maana hata siijui nilikoitupa!nakumbuka tulipewa na kikwete mwaka 2006 diamond jubilee!tulizichukua coz tulikuwa tunabembelezea mikopo ya vyuo!damn!let i go and find it now!
 
nguvumali, hasira za nini?, hasira hasara!.
Kwanza sio ustaarabu kuchoma moto kadi ya chama chochote, huu ni uhuni!.
Pili hata ukiichoma, chama kilichokupatia hiyo kadi, kitaendelea kujivunia uanachama wako maana jina lako linakuwa bado lipo kwenye register ya yao ya wanachama, hivyo the right forum ni ama kujitoa kwa kuwarudishia kadi yao, ama kujiunga na chama kingine kwa kuikabidhi hiyo kadi huko kwingine na hivyo kuwa sio mwanachama wa chako chako.

Angalizo, kwenye siasa, hakuna urafiki wa kudumu wala uadui wa kudumu, wako wengi kama wewe walkiofikiri siasa ni shibe, hivyo walikasirika na wakahama kwa mbwembwe na majigambo kibao, siku ya siku, njaa zikawazidia huko walipo na ni kwa kuendekeza hizo njaa zao, wakarudi walikotoka na sasa ni wapayukaji wakuu huku wakichumia tumbo!.
Pasco,
ni vyema wakaendelea kujivunia kuwa na jina langu na huenda likawapumbaza na kudhani wanaidadi hiyo ya wanachama , kumbe kinyume chake wengi watakua wametoka.
ni sawa na vile kin Nape wanavyojivunia mtaji wa wanachama milioni 5, huko ni kupumbazika wakati wanaolipia kadi hawazidi 1.7 millioni, waliobakia huwa wanalipiwa kadi na wagombea wanaotaka madaraka, hawa si wanachama hai, ni wachumia tumbo. wanaofikiri kwamba wali na khanga wakati wa uchaguzi ni ufumbuzi wa matatizo yao.
Tunataka watu waanze kutambua kuwa hakuna ukombozi kupitia ccm, njaa zao haziwezi kumalizwa kwa mlo mmoja, tunataka waasi mfumo uliopo ili kurejesha heshima ya Taifa na kuruhusu ustawi mpya wa nchi hii.
 
usiichome kivyakovyako. warudishie kadi yao, ili wapate somo kuwa wanawachama wanawahama. au vinginevyo jiunge nachama kingine na wakabidhi hiyo kadi ya ccm
 
mie na nunua kutoka kwa wananchi kadi moja sukari kilo moja nahitaji kuchemshia nazo chai mpaka ichemke nikipata za kutosha nitaota nazo moto.
 
siungi mkono hoja.
si ustaarabu kuchoma kadi ya chama chochote,kama umewachoka warudishie kadi yao.
hatuichukii ccm kwa sababu ni ccm tunaichukia kwa sababu ilitangulia kutuchukia watanzania,ila ikbadilika na kuwapenda watanzania na mimi narudi ccm kwa hiyo sioni sababu ya kuchoma kadi.
 
La msingi hapa sio kuchoma kadi bali kumuelimisha mwananchi wa kawaida kabisa kujua umuhimu wake siku ya kupiga kura, wananchi wakipata eleimu ya kutosha ya kupiga kura itasaidia sana kuleta mabadiriko bila hata kuchoma hiyo kadi. Maana inashangaza watu wamejiandikisha 19 million then wapiga kura wawe 7 million. Tuanzia hapo sasa kabla ya kupiga hatua nyingine
 
Back
Top Bottom