Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,608
Mkurugenzi wa kampuni ya roboti nchini China amezindua mpango wa kwanza duniani wa “roboti mjamzito” – kifaa kitakachokuwa na tumbo la uzazi la kisayansi na kuuzwa kwa takribani dola 14,000. Bei hii ni ndogo mno ukilinganisha na gharama ya kupata mama mbadala (surrogate) binadamu, ambayo huanzia kati ya dola 100,000 hadi 200,000. Mkurugenzi huyo wa teknolojia anadai kuwa kampuni yake inaweza kuwa tayari na mfano wa kwanza wa mauzo mapema mwaka ujao
China imewekeza kwa kiwango kikubwa katika teknolojia ya roboti, na sasa ni moja ya viongozi wakuu duniani katika matumizi ya mashine viwandani. Lakini wakati huohuo, taifa linakabiliana na changamoto kubwa ya kupungua kwa kiwango cha uzazi. Wanawake wengi wanachelewa kuzaa au kuamua kutopata watoto kabisa, na wenza wengine wakikumbwa na matatizo ya uzazi. Kulingana na ripoti ya The Lancet, kiwango cha ugumba kilipanda kutoka asilimia 12 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 18 mwaka 2020 – yaani takribani wanandoa 1 kati ya 5.6 wanapata shida ya kupata mtoto.
Kwa kuwa surrogacy (kupata mama mbadala) ni marufuku nchini China, pamoja na mabadiliko ya kijamii kuhusu kuzaa, taifa linahofia uchumi kudorora, nguvu kazi kupungua, na jamii yenye wazee wengi kupita kiasi. Hali hii imechochea mawazo ya kutengeneza roboti wa kubeba mimba.
Kwa mujibu wa Chosun Biz, wiki iliyopita Dr. Zhang Qifeng, mwanzilishi wa kampuni ya Kaiwa Technology iliyoko Guangzhou, alieleza kuhusu uvumbuzi wake. Qifeng, mwenye shahada ya uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Nanyang Technological University nchini Singapore, alisema roboti huyo ataweza kubeba mimba kwa miezi 9 hadi 10 na kumpa mtoto virutubisho kupitia kitovu bandia. Wazo hili linafanana na jaribio lililofanyika mwaka 2017 ambapo wana-kondoo walilelewa kupitia “mfuko wa kibaolojia” (biobag).