China yaanza kutumia roboti kuongoza magari barabarani

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
443
Reaction score
1,101
China imeanza majaribio ya kutumia roboti kwa ajili ya shughuli za barabarani ikiwa ni pamoja na kuongoza magari. Hata hivyo roboti hao hawana mamlaka ya kumkamata mtu pale anapokosea au kukiuka sheria.

Maroboti hayo yamepelekwa hasa kwenye makutano yenye shughuli nyingi ya barabara katika jiji la Hangzhou, mashariki mwa China.

Roboti hizo zenye urefu wa mita futi 6.2 zinaweza kumtambua mwendesha baiskeli ya umeme asiyevaa kofia ya usalama, kutoa onyo kwa heshima na kusogeza mikono yake ya kimitambo sambamba na taa za kuongozea magari.

Roboti hizo aina ya T2, mwenye uzito wa kilo 98, ametengenezwa na kampuni ya teknolojia ya nchini humo, SUPCON Information, na ni sehemu ya mpango wa majaribio unaolenga kukabidhi baadhi ya majukumu ya mara kwa mara ya maafisa wa polisi wa trafiki kwa roboti.

Mkuu wa Kituo cha Ubunifu wa Mifumo Akili Isiyohitaji Mwendeshaji cha SUPCON, Cao Hui, amesema katika mahojiano kwamba roboti huyo hutumia kamera, rada na mfumo wa kompyuta uliowekwa ndani yake kutambua waendesha baiskeli wasio na kofia za usalama, baiskeli za umeme zinazobeba abiria, magari yanayosimama kuvuka mistari maalumu ya kusimama, pamoja na watembea kwa miguu wanaovuka barabara kinyume na ishara za taa za kuongozea magari.

Roboti hao pia wanaweza kujibu maswali kuhusu maelekezo ya njia, maegesho na sheria za trafiki, huku mfumo wa dharura ukiwaunganisha watumiaji na polisi wa eneo husika. Kampuni ya SUPCON imepeleka roboti 15 katika jiji la Hangzhou tangu mwezi Mei.

1787216108944.png

1787216139801.png
 
View attachment 3653682

View attachment 3653685
Waache wawe na maendeleo hao,sisi serikali yetu juhudi yake kubwa ni kukikandamiza chama kikuu cha upinzani,na kuwafunga viongozi wake.
 
Back
Top Bottom