Choicevariable,
Suala la uongozi bora siyo jambo jepesi jepesi! Wachina wanakuja kufanya huo uwekezaji siyo kwa sababu wana huruma Hapana, ni kwa sababu wameona fursa ipo ya kupiga pesa, wameangalia mbali. Kwanza wameshajiridhisha kuwa Africa hata baada ya miaka Hamsini watakuwa bado wamelala. Wanajua kuwa wao ili waendelee wanahitaji first world Technology ambayo kila siku wanaiba na kukopy na kugombana na Westerners. Huku Afrika kuna vilema wa akili kama Tanzania, Congo DRC, Zambia, Zimbabwe nk nk; walizima ndiyo watapata raw materials na strategic metals na rare earths za kawaida kukompete na Westerners. Wao yaani wachina wanaita Soft Diplomacy, nyie mnawasifia ati hawa ndiyo rafiki. Wao wana plan ya 50 to 100 years.
Sasa kwani wewe unafikiri wao wanakuzidi wapi? Only one issue, DICIPLINE, sheria zao zinafuatwa ingawa ni draconian Zaidi ya zile za JPM; hamana utani kwenye uongozi wa kampuni au kwenye rushwa serikali au kampuni, adhabu ni kifo au kufungwa maisha hata uwe nani ingawa rushwa china bado ipo. Hapa kwetu hamna discipline hiyo. China kiongozi anaachishwa kazi au anafungwa kwa jela kwa kuwa na kimada. Discipline. Hivi Tanzania kuna kiongozi gani ana discipline? Kila shirika ni rushwa na rushwa adhabu yake ni Rais kusema STUPID.
Sasa hivi China ndiyo katawala Construction Industry yote ya Tanzania au Afrika, miradi hii ina faida kubwa lakini haina impact kwa Maendeleo ya long term kwa sababu faida yote na fedha za kigeni zinaenda nje yaani China. mradi mmoja wa Barabara unawapa faida USD 82 million, hiyo yote inaishia China siyo Tanzania. Sasa kwa nini MECCO wasipate hizo pesa ni kwa sababu viongozi waliua MECCO ili wapate rushwa kutoka kwa wageni kama wahindi, wachina na waarabu. Hawa ndiyo kipenzi tangu awamu ya pili. Sasa jiulize China makampuni yao waliyaua? Sisi tuna maEngineer kama wachina unashangaa Engineer wetu either hawana kazi au hawaaminiwi. Mchina haajiri Engineer wa kibongo. Anawaajiri wakwake na wakikosea anachapa viboko kama farasi au punda. Sisi tunaweza? Tunaweza lakini ukiwa na viongozi ambao nao hawana discipline nchi itakuwaje, ni kuwa sheria hazitafuatwa. Hata Katiba iwe imetungwaje haitafuatwa. Vyombo vya usalama na Idara zake Pamoja na mihimili ya nchi haina discipline. Sisi ni kama Wanyama hatuna conscience ya kujua lipi jema au baya.