Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 189
- 314
Katika miaka ya 1960, Zambia ambayo ni mzalishaji wa tatu wa shaba duniani, ilikabiliwa na changamoto ya mauzo ya nje ya shaba kutokana na vizuizi vilivyowekwa na serikali za kikoloni za nchi jirani. Mwalimu Juliusi Nyerere wa Tanzania aliomba msaada kwa jamii ya kimataifa, nchi za magharibi zilikataa bila ya kusita, ila China, ambayo wakati ule ilikuwa inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi ilikubali kutoa msaada.
Mwaka 1965, aliyekuwa rais wa China Mao Zedong alimwambia Nyerere, “Tutasaidia kujenga reli hiyo hata kama tukilazimika kuacha kujenga reli nyumbani.” Halafu China ilitoa fedha na kupeleka makumi ya elfu ya wahandisi na mafundi wa China kujenga reli hiyo. Walifanya kazi ngumu kwa kushirikiana na wenzao wa Tanzania na Zambia kwa miaka sita, mpaka kukamilisha reli hiyo yenye urefu wa kilomita 1,860.
Mwaka 2024, China, Tanzania, na Zambia zilisaini Mkataba wa Makubaliano kuhusu Mradi wa Uhuishaji wa Reli ya TAZARA, zikiamua kuirekebisha kikamilifu reli hiyo. Mwaka 2025, mradi huo ulianza rasmi, na makampuni ya China yakishirikiana na makampuni ya Tanzania na Zambia yataunganisha reli hiyo na mtandao wa reli wa kikanda, na kuunda mfumo mpya wa “usafirishaji wa reli na bandari” na Bandari ya Dar es Salaam. Mara tu mradi huo utakapokamilika, Reli ya TAZARA inatarajiwa kuongeza mara tatu uwezo wake wa usafirishaji wa kila mwaka.
Baada ya miaka 50, moyo wa Reli ya TAZARA umepata uhai mpya katika ushirikiano wa China na Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, reli nyingine nyingi zilizojengwa na China ikiwemo reli ya SGR inayounganisha Nairobi na Mombasa na reli inayounganisha Addis Ababa na Djibouti, zilizinduliwa barani Afrika. Ushirikiano kati ya China na Afrika unastawi katika nyanja mbalimbali kama vile uchumi wa kidijitali, maendeleo ya kijani, juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na huduma za elimu na afya.
Pendekezo la China la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” linaendana na Ajenda ya Afrika ya 2063. China imeendelea kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 17 mfululizo. China na Afrika zimeinua kiwango cha uhusiano wao kuwa Jumuiya yenye Hatma ya Pamoja katika Enzi Mpya.
Safari ya miaka 50 ya Reli ya TAZARA imeshuhudia uhusiano wa kirafiki wa China na Afrika. Hadi leo, moyo wa reli hiyo wa usawa, kuheshimiana, na kunufaishana bado ni moyo wa ushirikiano wa China na Afrika. Wakati dunia inapokabiliana na mabadiliko makubwa ambayo hajawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita, China itaendelea kushirikiana na nchi za Afrika kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja ya pande hizo mbili