China kujenga standard gauge reli ya TAZARA

Sri Lanka sasa hivi wanalia baada China kuwekeza sana nchini humor wakashindwa kulipa hivyo China wakajitwalia bandari kwa miaka 100 had I pesa yao irudi
wacha uongo lisome vizuri sakata la Sri Lanka, India na China.
 
Sri Lanka sasa hivi wanalia baada China kuwekeza sana nchini humor wakashindwa kulipa hivyo China wakajitwalia bandari kwa miaka 100 had I pesa yao irudi
Na huenda wanafanya the same Pakistan, Myanmar, Vanuatu, Jibuti! Miradi ya Uchina ni mashaka sana.
 
Mimi nadhani haitakuwa vibaya Rais wetu akienda China,na hata Urusi.Hizi nchi zimekaa vizuri,they are dependable, tofauti na matapeli ya nchi za Magharabi.
 
Mchina ataparekebisha pamoja na maeneo mengine korofi ili kuwezesha mwendo kasi wa treni za SGR.
Mimi nimefanya kazi TAZARA ktk train ya Abiria miaka ya themanini. Nakumbuka mara kibao tulikua tunawafaulisha abiria. Watu wanatembea umbali fulani sababu kila mwezi magari ya mizigo yakikua yanaanguka
 
Wamesema watang'oa hayo mavuma ya reli yaliyopo na kuweka mapya yenye upana wa standard. Kazi hiyo inaweza kufanyika ndani ya miezi 6 na kuwa SGR ya diseal kama ya Kenya kutoka Dar hadi Kapilimposhi. Hatujengi tuta jipya, lililopo linatosha. Tunatumaini JPM atawaruhusu kazi hiyo ianze mara moja. Halafu wamesema wataleta mabehewa na vichwa vya treni na kuviendesha kwa gharama yao wenyewe. Sisi tutapata kodi yetu stahiki katika uendeshaji huo. This is Public Public Paternaship instead of Public Private Paternaship ambayo si nzuri. Hapa public ya Tanzania inashirikiana na public ya China kujenga na kuendesha mradi wa serikali.
Hawa jamaa ni nguvu kazi hii reli waliijenga kwa miaka mita
TAZARA tayari ni standard gauge. Pia ni uwendawazimu kusema eti watai'goa iliyopo na kujenga ingine, hata kama kweli ingekuwa siyo standard gauge. Acheni kudanganya watu.
Mkuu unavijua vipimo vya reli ama unapenda kufurahisha umma. TAZARA ni CAPE GAUGE na siyo Standard. Haijafikia huko TAZARA NI 3FT 6in standard gauge ni 4ft 8.5 in
 
“Wanasema wakikubaliwa watang’oa reli iliyopo na watajenga reli mpya ya Standard Gauge kwa ajili hiyo walimuomba Dkt Salim wafikishie salamu hizo kwa Rais wa Tanzania Dkt Johm Magufuli ambaye walitoa mwaliko maalum kwake ahudhurie mkutano wa China na Afrika utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu”, ameeleza mjumbe mwingine.

Aidha amesema katika mazungumzo ya faragha kati ya Makamu wa Rais wa China na Dkt Salim, China imemuomba Rais Magufuli awape fursa maalum katika uwekezaji Tanzania ili China yenye uchumi mkubwa na nguvu duniani ioneshe jinsi inavyothamini udugu na urafiki baina ya mataifa haya mawili.
waje tu wajenge hiyo SGR tusafirishe mizigo ya kusini mwa Afrika tujenge uchumi wa nchi zetu na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara
 
Ninavyokumbuka Mimi Tazara ni Cape gauge railway ambayo inatumika sana nchi za kuzini mwa Afrika (Zambia, Zimbabwe, Botswana na R South Africa)... Sasa Kama wanataka kuing'oa na kulaza njia mpya no wazo jengine ambalo halina maana (kwa maoni yangu) kwani hâta huko nchi ziloendelea wana reli nyembamba n'a wanaweka vituo vya kubadilisha ili reli zinotofautiana zinabadilishana ......


Alhuda 619, 16/05/2018- Ramadhan.

CHINA KUJENGA STANDARD GAUGE RELI YA TAZARA

Na Mwandishi Wetu

China inajiandaa kwa uwekezaji mkubwa nchini Tanzania.

Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao ametoa ahadi hiyo kwa Dkt. Salim Ahmed Salim Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania uliokuwa nchini China wiki moja iliyopita, huku akimuomba mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM amfikishie Salamu maalum kwa rais wa Tanzania Dkt John Magufuli.

Katika mazungumzo hayo, yaliyohafanyika katika Hoteli ya Regent mjini Beijing nchini humo jumatatu iliyopita, Bwana Li Yuanchao aliyemuwakilisha Rais wa nchi hiyo Xi Jinping, amesema China ina nia kubwa ya kuiinua Tanzania kiuchumi ikikumbuka uhusiano wa kihistoria wa nchi hizi mbili na jitihada kubwa iliyofanywa na Tanzania kuirejesha China katika kiti chake umoja wa Mataifa.

Makamu wa Rais wa China alimwambia Dkt Salim na ujumbe wake kuwa nchi hiyo inaikumbuka na kuithamini zaidi Tanzania katika mataifa ya kiafrika.

“Makamu wa Rais wa China alieleza anavyokumbuka jinsi Dkt Salim wakati huo akiwa Umoja wa Mataifa alivyofurahi China kurejesha kiti chake”, mmoja wa wajumbe wa ujumbe huyo alimueleza Mwandishi nje ya mkutano huo wa faragha.

Amesema katika kuonesha China inavyothamini Tanzania, ujumbe wa Dkt Salim ulipewa mapokezi maalum katika Hoteli Homg Qiao State Guest ambayo ni maalum yenye ulinzi na utulivu mkubwa mjini Shanghai.

Akiwasilisha salamu za Mwenyekiti wa chama cha Kikomunisti cha China, rais Ximping kwa Comrade Salim, makamu huyo wa rais wa China aliuambia ujumbe wa Tanzania kuwa watu wa China wanaipenda Tanzania na kwamba serikali ya watu wa China ingependa kuwekeza kwenye miundombinu na kuonesha haja ya kuichukua tena reli ya TAZARA ili kuiboresha na kuiendesha kibiashara.

“Wanasema wakikubaliwa watang’oa reli iliyopo na watajenga reli mpya ya Standard Gauge kwa ajili hiyo walimuomba Dkt Salim wafikishie salamu hizo kwa Rais wa Tanzania Dkt Johm Magufuli ambaye walitoa mwaliko maalum kwake ahudhurie mkutano wa China na Afrika utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu”, ameeleza mjumbe mwingine.

Aidha amesema katika mazungumzo ya faragha kati ya Makamu wa Rais wa China na Dkt Salim, China imemuomba Rais Magufuli awape fursa maalum katika uwekezaji Tanzania ili China yenye uchumi mkubwa na nguvu duniani ioneshe jinsi inavyothamini udugu na urafiki baina ya mataifa haya mawili.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Dkt Salim uliondoka nchini kuelekea China jumamosi iliyopita na kuwasili siku ya pili kuitikia mwaliko wa chama cha urafiki katika ya Tanzania na China(Tanzania China Frirendship Promotion Association) ambacho Mwenyekiti wake ni Dkt Salim Ahmed Sali.

Jummane iliyopita ujumbe huyo ulihudhuria Kongamano la Serikali za mitaa ambalo pia lililohudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa nchi ya Niger.

Katika Hotuba yake kwenye Kongamano hilo, Dkt Salim alielezea uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na China na uzoefu katika siasa za kimataifa ambapo alisifu msingi imara wa Tanzania ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere katika kupigania haki na usawa duniani ambao uliikutanisha Tanzania na mataifa kama China na mengine ya mfano wake.

Kabla ya hapo Dkt Salim alihojiwa na China Global Television Network ambapo siku ya jumanne mchana alitembelea Chuo Kikuu kikongwe cha Peking na kuzungumza na wanafunzi wa nchi za kiafrika wanaosoma Chuoni hapo kisha kukutana na Profesa Liu ambaye ni Mkongwe katika Chuo hicho.

Ukiwa mjini Shanghai ujumbe huo ambao pia ulimjumuisha Balozi wa Tanzania nchini humo Bwana Kairuki, ulitembelea mahali kilipoasisiwa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China mwaka 1921 na kushuhudia picha za waasisi wake 12 wakiwa kwenye kikao wakiongozwa na Mao Ze Dong.
 
Sri Lanka sasa hivi wanalia baada China kuwekeza sana nchini humor wakashindwa kulipa hivyo China wakajitwalia bandari kwa miaka 100 had I pesa yao irudi
sawa tu, waje tuwa kodishe... ili tupumue angalau.... kama jasho lituvuje wote mpaka wajukuu walio tumboni
 
hili joto hasira... kama kula walikula wote... kama kupanda walipanda wote na kuvuna pia
 
Tazara siyo Standard gauge. Ina upana wa 1.067mm.

Standard gauge ina upana wa 1.435mm.

Kitu ambacho hakieleweki hapa ni kama watajenga reli mpya au wataongeza upana wa hii ya sasa.
Nadhani watu wengi humu hawaelewi SGR nini? TAZARA ni SGR walitujengea Wachina miaka hiyo ilianza kujengwa 1969-1976 ambayo ina umbali wa Km 1896 Dar hadi Kapiri Mposhi Zambia. Ndio maana train inaweza kutoka Bandari ya Port Elizabeth South Africa hadi Tanzania bila kubadili mabehewa. Hii reli yetu ya TRL sio Standard gauge hii mostly iko East Africa hasa Kenya, Uganda na Tanzania. wa-Kenya wamejenga Standard gauge railway hivi karibuni. Sio kwamba Standard gauge ni ile rail yenye Umeme. Standard Gauge ni ule Upana wa Kimataifa unaozingatia SI unit za Kimataifa.
 
Back
Top Bottom