China kujenga standard gauge reli ya TAZARA

....
“Makamu wa Rais wa China alieleza anavyokumbuka jinsi Dkt Salim wakati huo akiwa Umoja wa Mataifa alivyofurahi China kurejesha kiti chake”, mmoja wa wajumbe wa ujumbe huyo alimueleza Mwandishi nje ya mkutano huo wa faragha.
...
Hawa jamaa wanatuona mazuzu sana wallahi! Kwa hiyo kubwa ililofanya Tanzania ni hilo la "kufurahi China kurejeshewa kiti chake".
 
Wapewe fursa maalum katika kuwekeza hapa Tanzania?! Kama watakubaliwa, basi kitakachotokea ni the rising of China East Africa.
 
Alhuda 619, 16/05/2018- Ramadhan.

CHINA KUJENGA STANDARD GAUGE RELI YA TAZARA

Na Mwandishi Wetu

China inajiandaa kwa uwekezaji mkubwa nchini Tanzania.

Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao ametoa ahadi hiyo kwa Dkt. Salim Ahmed Salim Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania uliokuwa nchini China wiki moja iliyopita, huku akimuomba mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM amfikishie Salamu maalum kwa rais wa Tanzania Dkt John Magufuli.

Katika mazungumzo hayo, yaliyohafanyika katika Hoteli ya Regent mjini Beijing nchini humo jumatatu iliyopita, Bwana Li Yuanchao aliyemuwakilisha Rais wa nchi hiyo Xi Jinping, amesema China ina nia kubwa ya kuiinua Tanzania kiuchumi ikikumbuka uhusiano wa kihistoria wa nchi hizi mbili na jitihada kubwa iliyofanywa na Tanzania kuirejesha China katika kiti chake umoja wa Mataifa.

Makamu wa Rais wa China alimwambia Dkt Salim na ujumbe wake kuwa nchi hiyo inaikumbuka na kuithamini zaidi Tanzania katika mataifa ya kiafrika.

“Makamu wa Rais wa China alieleza anavyokumbuka jinsi Dkt Salim wakati huo akiwa Umoja wa Mataifa alivyofurahi China kurejesha kiti chake”, mmoja wa wajumbe wa ujumbe huyo alimueleza Mwandishi nje ya mkutano huo wa faragha.

Amesema katika kuonesha China inavyothamini Tanzania, ujumbe wa Dkt Salim ulipewa mapokezi maalum katika Hoteli Homg Qiao State Guest ambayo ni maalum yenye ulinzi na utulivu mkubwa mjini Shanghai.

Akiwasilisha salamu za Mwenyekiti wa chama cha Kikomunisti cha China, rais Ximping kwa Comrade Salim, makamu huyo wa rais wa China aliuambia ujumbe wa Tanzania kuwa watu wa China wanaipenda Tanzania na kwamba serikali ya watu wa China ingependa kuwekeza kwenye miundombinu na kuonesha haja ya kuichukua tena reli ya TAZARA ili kuiboresha na kuiendesha kibiashara.

“Wanasema wakikubaliwa watang’oa reli iliyopo na watajenga reli mpya ya Standard Gauge kwa ajili hiyo walimuomba Dkt Salim wafikishie salamu hizo kwa Rais wa Tanzania Dkt Johm Magufuli ambaye walitoa mwaliko maalum kwake ahudhurie mkutano wa China na Afrika utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu”, ameeleza mjumbe mwingine.

Aidha amesema katika mazungumzo ya faragha kati ya Makamu wa Rais wa China na Dkt Salim, China imemuomba Rais Magufuli awape fursa maalum katika uwekezaji Tanzania ili China yenye uchumi mkubwa na nguvu duniani ioneshe jinsi inavyothamini udugu na urafiki baina ya mataifa haya mawili.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Dkt Salim uliondoka nchini kuelekea China jumamosi iliyopita na kuwasili siku ya pili kuitikia mwaliko wa chama cha urafiki katika ya Tanzania na China(Tanzania China Frirendship Promotion Association) ambacho Mwenyekiti wake ni Dkt Salim Ahmed Sali.

Jummane iliyopita ujumbe huyo ulihudhuria Kongamano la Serikali za mitaa ambalo pia lililohudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa nchi ya Niger.

Katika Hotuba yake kwenye Kongamano hilo, Dkt Salim alielezea uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na China na uzoefu katika siasa za kimataifa ambapo alisifu msingi imara wa Tanzania ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere katika kupigania haki na usawa duniani ambao uliikutanisha Tanzania na mataifa kama China na mengine ya mfano wake.

Kabla ya hapo Dkt Salim alihojiwa na China Global Television Network ambapo siku ya jumanne mchana alitembelea Chuo Kikuu kikongwe cha Peking na kuzungumza na wanafunzi wa nchi za kiafrika wanaosoma Chuoni hapo kisha kukutana na Profesa Liu ambaye ni Mkongwe katika Chuo hicho.

Ukiwa mjini Shanghai ujumbe huo ambao pia ulimjumuisha Balozi wa Tanzania nchini humo Bwana Kairuki, ulitembelea mahali kilipoasisiwa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China mwaka 1921 na kushuhudia picha za waasisi wake 12 wakiwa kwenye kikao wakiongozwa na Mao Ze Dong.

Kama Wachina wanataka kuichukua Railway na kuiendesha kibiashara ni vyema, maana kwa sasa hivi imekaa tu haifanyi kazi. Ni afadhali waichukue waikarabati na wasafirishe abiria na mizigo na serikali za Zambia na JMT zitakua wabia kwa silimia kadhaa
 
Tazara siyo Standard gauge. Ina upana wa 1.067mm.

Standard gauge ina upana wa 1.435mm.

Kitu ambacho hakieleweki hapa ni kama watajenga reli mpya au wataongeza upana wa hii ya sasa.
Wamesema watang'oa hayo mavuma ya reli yaliyopo na kuweka mapya yenye upana wa standard. Kazi hiyo inaweza kufanyika ndani ya miezi 6 na kuwa SGR ya diseal kama ya Kenya kutoka Dar hadi Kapilimposhi. Hatujengi tuta jipya, lililopo linatosha. Tunatumaini JPM atawaruhusu kazi hiyo ianze mara moja. Halafu wamesema wataleta mabehewa na vichwa vya treni na kuviendesha kwa gharama yao wenyewe. Sisi tutapata kodi yetu stahiki katika uendeshaji huo. This is Public Public Paternaship instead of Public Private Paternaship ambayo si nzuri. Hapa public ya Tanzania inashirikiana na public ya China kujenga na kuendesha mradi wa serikali.
 
hii habari kaileta nani? au wale wale CCM from Lumumba? totally politics... Stupid Dogs

Tazara kila siku tunaambiwa ni Standard gauge labda waseme wanakuja kuivalisha viatu vipya four angle
 
TAZARA tayari ni standard gauge. Pia ni uwendawazimu kusema eti watai'goa iliyopo na kujenga ingine, hata kama kweli ingekuwa siyo standard gauge. Acheni kudanganya watu.
Hata mimi nilikuwa najiuliza kuwa SGR ni nini tena? maana iliyopo tayari ni SGR. na kama ni kweli yamesemwa hivyo huko China na watu wakasikiliza na kukubaliana na kuubeba ujumbe, then hee, sijui tunaenda wapi sasa?
 
Wamesema watang'oa hayo mavuma ya reli yaliyopo na kuweka mapya yenye upana wa standard. Kazi hiyo inaweza kufanyika ndani ya miezi 6 na kuwa SGR ya diseal kama ya Kenya kutoka Dar hadi Kapilimposhi. Hatujengi tuta jipya, lililopo linatosha. Tunatumaini JPM atawaruhusu kazi hiyo ianze mara moja. Halafu wamesema wataleta mabehewa na vichwa vya treni na kuviendesha kwa gharama yao wenyewe. Sisi tutapata kodi yetu stahiki katika uendeshaji huo. This is Public Public Paternaship instead of Public Private Paternaship ambayo si nzuri. Hapa public ya Tanzania inashirikiana na public ya China kujenga na kuendesha mradi wa serikali.
Muwe tayari kuandaa majeneza pia.
 
China inajiandaa kwa uwekezaji mkubwa nchini Tanzania.

Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao ametoa ahadi hiyo kwa Dkt. Salim Ahmed Salim Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania uliokuwa nchini China wiki moja iliyopita, huku akimuomba mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM amfikishie Salamu maalum kwa rais wa Tanzania Dkt John Magufuli.

Katika mazungumzo hayo, yaliyohafanyika katika Hoteli ya Regent mjini Beijing nchini humo jumatatu iliyopita, Bwana Li Yuanchao aliyemuwakilisha Rais wa nchi hiyo Xi Jinping, amesema China ina nia kubwa ya kuiinua Tanzania kiuchumi ikikumbuka uhusiano wa kihistoria wa nchi hizi mbili na jitihada kubwa iliyofanywa na Tanzania kuirejesha China katika kiti chake umoja wa Mataifa.

Makamu wa Rais wa China alimwambia Dkt Salim na ujumbe wake kuwa nchi hiyo inaikumbuka na kuithamini zaidi Tanzania katika mataifa ya kiafrika.

“Makamu wa Rais wa China alieleza anavyokumbuka jinsi Dkt Salim wakati huo akiwa Umoja wa Mataifa alivyofurahi China kurejesha kiti chake”, mmoja wa wajumbe wa ujumbe huyo alimueleza Mwandishi nje ya mkutano huo wa faragha.

Amesema katika kuonesha China inavyothamini Tanzania, ujumbe wa Dkt Salim ulipewa mapokezi maalum katika Hoteli Homg Qiao State Guest ambayo ni maalum yenye ulinzi na utulivu mkubwa mjini Shanghai.

Akiwasilisha salamu za Mwenyekiti wa chama cha Kikomunisti cha China, rais Ximping kwa Comrade Salim, makamu huyo wa rais wa China aliuambia ujumbe wa Tanzania kuwa watu wa China wanaipenda Tanzania na kwamba serikali ya watu wa China ingependa kuwekeza kwenye miundombinu na kuonesha haja ya kuichukua tena reli ya TAZARA ili kuiboresha na kuiendesha kibiashara.

“Wanasema wakikubaliwa watang’oa reli iliyopo na watajenga reli mpya ya Standard Gauge kwa ajili hiyo walimuomba Dkt Salim wafikishie salamu hizo kwa Rais wa Tanzania Dkt Johm Magufuli ambaye walitoa mwaliko maalum kwake ahudhurie mkutano wa China na Afrika utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu”, ameeleza mjumbe mwingine.

Aidha amesema katika mazungumzo ya faragha kati ya Makamu wa Rais wa China na Dkt Salim, China imemuomba Rais Magufuli awape fursa maalum katika uwekezaji Tanzania ili China yenye uchumi mkubwa na nguvu duniani ioneshe jinsi inavyothamini udugu na urafiki baina ya mataifa haya mawili.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Dkt Salim uliondoka nchini kuelekea China jumamosi iliyopita na kuwasili siku ya pili kuitikia mwaliko wa chama cha urafiki katika ya Tanzania na China(Tanzania China Frirendship Promotion Association) ambacho Mwenyekiti wake ni Dkt Salim Ahmed Sali.

Jummane iliyopita ujumbe huyo ulihudhuria Kongamano la Serikali za mitaa ambalo pia lililohudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa nchi ya Niger.

Katika Hotuba yake kwenye Kongamano hilo, Dkt Salim alielezea uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na China na uzoefu katika siasa za kimataifa ambapo alisifu msingi imara wa Tanzania ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere katika kupigania haki na usawa duniani ambao uliikutanisha Tanzania na mataifa kama China na mengine ya mfano wake.

Kabla ya hapo Dkt Salim alihojiwa na China Global Television Network ambapo siku ya jumanne mchana alitembelea Chuo Kikuu kikongwe cha Peking na kuzungumza na wanafunzi wa nchi za kiafrika wanaosoma Chuoni hapo kisha kukutana na Profesa Liu ambaye ni Mkongwe katika Chuo hicho.

Ukiwa mjini Shanghai ujumbe huo ambao pia ulimjumuisha Balozi wa Tanzania nchini humo Bwana Kairuki, ulitembelea mahali kilipoasisiwa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China mwaka 1921 na kushuhudia picha za waasisi wake 12 wakiwa kwenye kikao wakiongozwa na Mao Ze Dong.
 
Mchina na wenzake wote wa bara la Asia ni wakatili sana. Wanatafuta mahali pa kusitiri raia wao hawa. Hivi ni mbongo gani analipwa ml.5 kwa mwezi kwenye hizi kampuni za Kichina?
Hii miradi mingine hatuitaki sasa, kama vimiradi 4 vimesimamisha stahiki za watumishi kwa miaka kadhaa je, hii miradi mingine hii?
 
Ndo na sisi tujipange tuwe na makampuni yetu kwani hata wewe ukiwa na kampuni upate tenda hapo Kenya utashindwa kuwabeba watu wa nchini kwako? Tusilalamike tujifunze
 
Back
Top Bottom