dickchiller
JF-Expert Member
- Apr 30, 2012
- 1,847
- 3,151
mzee Salim Ahmed Salim yupo vizuri sana kwenye masuala ya kimataifa. nadhani hawezi leta deal fake
TAZARA upana wake sio wa SGR ule ni upana wa Cape gauge ambayo inatumika sana nchi za kusini mwa Afrika ndo mana ikapewa hilo jina la Cape gauge.. Tazara sio standard gauge google vitu vingine vipo wazi kabisa reli kutumika hizo nchi zote haimaanishi ndo standard gauge.....standard gauge ina vipimo vyake na hio cape gauge ina vipimo vyakeNadhani watu wengi humu hawaelewi SGR nini? TAZARA ni SGR walitujengea Wachina miaka hiyo ilianza kujengwa 1969-1976 ambayo ina umbali wa Km 1896 Dar hadi Kapiri Mposhi Zambia. Ndio maana train inaweza kutoka Bandari ya Port Elizabeth South Africa hadi Tanzania bila kubadili mabehewa. Hii reli yetu ya TRL sio Standard gauge hii mostly iko East Africa hasa Kenya, Uganda na Tanzania. wa-Kenya wamejenga Standard gauge railway hivi karibuni. Sio kwamba Standard gauge ni ile rail yenye Umeme. Standard Gauge ni ule Upana wa Kimataifa unaozingatia SI unit za Kimataifa.
Mkuu iliyopo kwa sasa mbona nayo ni SGR!Alhuda 619, 16/05/2018- Ramadhan.
CHINA KUJENGA STANDARD GAUGE RELI YA TAZARA
Na Mwandishi Wetu
China inajiandaa kwa uwekezaji mkubwa nchini Tanzania.
Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao ametoa ahadi hiyo kwa Dkt. Salim Ahmed Salim Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania uliokuwa nchini China wiki moja iliyopita, huku akimuomba mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM amfikishie Salamu maalum kwa rais wa Tanzania Dkt John Magufuli.
Katika mazungumzo hayo, yaliyohafanyika katika Hoteli ya Regent mjini Beijing nchini humo jumatatu iliyopita, Bwana Li Yuanchao aliyemuwakilisha Rais wa nchi hiyo Xi Jinping, amesema China ina nia kubwa ya kuiinua Tanzania kiuchumi ikikumbuka uhusiano wa kihistoria wa nchi hizi mbili na jitihada kubwa iliyofanywa na Tanzania kuirejesha China katika kiti chake umoja wa Mataifa.
Makamu wa Rais wa China alimwambia Dkt Salim na ujumbe wake kuwa nchi hiyo inaikumbuka na kuithamini zaidi Tanzania katika mataifa ya kiafrika.
“Makamu wa Rais wa China alieleza anavyokumbuka jinsi Dkt Salim wakati huo akiwa Umoja wa Mataifa alivyofurahi China kurejesha kiti chake”, mmoja wa wajumbe wa ujumbe huyo alimueleza Mwandishi nje ya mkutano huo wa faragha.
Amesema katika kuonesha China inavyothamini Tanzania, ujumbe wa Dkt Salim ulipewa mapokezi maalum katika Hoteli Homg Qiao State Guest ambayo ni maalum yenye ulinzi na utulivu mkubwa mjini Shanghai.
Akiwasilisha salamu za Mwenyekiti wa chama cha Kikomunisti cha China, rais Ximping kwa Comrade Salim, makamu huyo wa rais wa China aliuambia ujumbe wa Tanzania kuwa watu wa China wanaipenda Tanzania na kwamba serikali ya watu wa China ingependa kuwekeza kwenye miundombinu na kuonesha haja ya kuichukua tena reli ya TAZARA ili kuiboresha na kuiendesha kibiashara.
“Wanasema wakikubaliwa watang’oa reli iliyopo na watajenga reli mpya ya Standard Gauge kwa ajili hiyo walimuomba Dkt Salim wafikishie salamu hizo kwa Rais wa Tanzania Dkt Johm Magufuli ambaye walitoa mwaliko maalum kwake ahudhurie mkutano wa China na Afrika utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu”, ameeleza mjumbe mwingine.
Aidha amesema katika mazungumzo ya faragha kati ya Makamu wa Rais wa China na Dkt Salim, China imemuomba Rais Magufuli awape fursa maalum katika uwekezaji Tanzania ili China yenye uchumi mkubwa na nguvu duniani ioneshe jinsi inavyothamini udugu na urafiki baina ya mataifa haya mawili.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Dkt Salim uliondoka nchini kuelekea China jumamosi iliyopita na kuwasili siku ya pili kuitikia mwaliko wa chama cha urafiki katika ya Tanzania na China(Tanzania China Frirendship Promotion Association) ambacho Mwenyekiti wake ni Dkt Salim Ahmed Sali.
Jummane iliyopita ujumbe huyo ulihudhuria Kongamano la Serikali za mitaa ambalo pia lililohudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa nchi ya Niger.
Katika Hotuba yake kwenye Kongamano hilo, Dkt Salim alielezea uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na China na uzoefu katika siasa za kimataifa ambapo alisifu msingi imara wa Tanzania ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere katika kupigania haki na usawa duniani ambao uliikutanisha Tanzania na mataifa kama China na mengine ya mfano wake.
Kabla ya hapo Dkt Salim alihojiwa na China Global Television Network ambapo siku ya jumanne mchana alitembelea Chuo Kikuu kikongwe cha Peking na kuzungumza na wanafunzi wa nchi za kiafrika wanaosoma Chuoni hapo kisha kukutana na Profesa Liu ambaye ni Mkongwe katika Chuo hicho.
Ukiwa mjini Shanghai ujumbe huo ambao pia ulimjumuisha Balozi wa Tanzania nchini humo Bwana Kairuki, ulitembelea mahali kilipoasisiwa Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China mwaka 1921 na kushuhudia picha za waasisi wake 12 wakiwa kwenye kikao wakiongozwa na Mao Ze Dong.
Sio SGRMkuu iliyopo kwa sasa mbona nayo ni SGR!
Nadhani watu wengi humu hawaelewi SGR nini? TAZARA ni SGR walitujengea Wachina miaka hiyo ilianza kujengwa 1969-1976 ambayo ina umbali wa Km 1896 Dar hadi Kapiri Mposhi Zambia. Ndio maana train inaweza kutoka Bandari ya Port Elizabeth South Africa hadi Tanzania bila kubadili mabehewa. Hii reli yetu ya TRL sio Standard gauge hii mostly iko East Africa hasa Kenya, Uganda na Tanzania. wa-Kenya wamejenga Standard gauge railway hivi karibuni. Sio kwamba Standard gauge ni ile rail yenye Umeme. Standard Gauge ni ule Upana wa Kimataifa unaozingatia SI unit za Kimataifa.
AhsanteMkuu reli ya Tazara si SGR.
Imezidi upana wa reli ya TRC kwa 6.7cm tu.
Upana wa SGR ni kama nilivyoonyesha kwenye post yangu.