Chiligati: Acheni kuandika habari za wanachama wa CCM kujiunga CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Naibu katibu mkuu wa CCM John Chiligati ameshutumu tabia ya vyombo vya habari kushupalia suala la wanachama wanaotoka CCM kwenda kujiunga na CDM.
Chiligati ameshauri vyombo vya habari kuandika mambo ya msingi yanayohusu maendeleo ya watanzania na si kila siku kuandika habari za wanaCCM wanaojiunga CDM.
Chiligati alikasirishwa na maswali ya waandishi kumtaka atoe maoni yake kuhusiana na wimbi la wanachama na viongozi wanaojiunga CDM kutokea CCM.
Source:Tanzania daima.
 
chilgat yupo sahihi kabisa, yawapasa waandish wa habari waandike mambo yamaendeleo katika jamii, siyo kila siku cdm na ccm mpaka lini!!?? wajaribu kuzungumza mambo yanayomgusa kila mtanzania kwa upande wake, tunatengeneza nchi siyo chama.
 
Atajijuuu!ye alidhani habari ni zile za viongozi wa CDM kukamwatwa na askari?hiki kimbunga tu anaanza kuweweseka je tsunami inayokuja 2015 si ndo ataanza kuchapana na wahariri?
 
Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu oooh, je Makamo wa rais alipoenda Nachingwea na kuvuna wanachama eti 800 toka CDM Mh. Chiligati alisema chochote? Huyo huyo Chiligati magazeti yalivyomwandika amewasahau wapiga kura wake wa pale NUNJE kambi ya SUKAMAHELA, wakoma wanaomba barabarani na magodolo yao wametapeliwa Chiligati alisema hayo ni magazeti tu. Sasa akubali tu matokea kimbunga bado kinakuja.
 
Magazeti yatauzwaje?
Basi waandike JK safarini kutembeza bakuli la rambirambi make inchi ishadedi.
 
Kwani habari muhimu yeye anazipimaje? Na umuhimu inategemeana kwa nani! Manaake ya muhimu kwake sio ya Muhimu kwetu and vise versa, Wangekuwa wanaandika jinsi wana CDM wanavyo hamia CCM ingekuwa ya muhimu kwake! Shortsitedness!
 
Naibu katibu mkuu wa CCM John Chiligati ameshutumu tabia ya vyombo vya habari kushupalia suala la wanachama wanaotoka CCM kwenda kujiunga na CDM.
Chiligati ameshauri vyombo vya habari kuandika mambo ya msingi yanayohusu maendeleo ya watanzania na si kila siku kuandika habari za wanaCCM wanaojiunga CDM.
Chiligati alikasirishwa na maswali ya waandishi kumtaka atoe maoni yake kuhusiana na wimbi la wanachama na viongozi wanaojiunga CDM kutokea CCM.
Source:Tanzania daima.
Ama kweli mkuki kwa nguruwe.......wamesahau mwenyekti wa chadema mkoa wa Mbeya alipo jiunga na CCM vyombo vyote vya habari vilitangaza takribani wiki nzima mbona hakuzuia...
 
ccm hawakutarajia kabisa haya mabadiliko,tumuulize chiligati mara ya mwisho ccm kufanya mkutano wa hadhara ni lini?
 
Kwani habari muhimu yeye anazipimaje? Na umuhimu inategemeana kwa nani! Manaake ya muhimu kwake sio ya Muhimu kwetu and vise versa, Wangekuwa wanaandika jinsi wana CDM wanavyo hamia CCM ingekuwa ya muhimu kwake! Shortsitedness!
Naona wandishi wa habri wanaanza kupangiwa habari za kuandika kwenye vyombo vyao....
 
Back
Top Bottom