Child Custody after Divorce.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Child Custody after Divorce..

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kibunango, Feb 4, 2009.

 1. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Wanabodi, sheria ya Tanzania inasema nini juu ya hili? Ni nani hasa anapaswa kuwa mlezi wa mtoto baada ya talaka?
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa Sheria yetu ya ndoa ya Mwaka 1971. Kama watoto wana umri wa chini ya miaka 7. Watoto watatunzwa na mama ambapo baba atawajibika kutoa matunzo na visitation right.
  Kama wana umri wa zaidi ya miaka saba, wazazi mkubaliane wakae wapi. Msipokubaliana, yaani mkiamua kuwagombea, mahakama itaangalia the best interest ya watoto ikiwepo kuwauliza watoto wenyewe.
  Mmoja ya wazazi akiweka pingamizi la kipato/ulevi au ukatili dhidi ya watoto, mahakama inaweza kuamua kumkabidhi mzazi salama na baba kuwajibika kutoa matunzo.

  Sheria yetu hii inatamka bayana kiwango cha matunzo ni Shilingi Mia moja kwa kila mtoto kwa Mwezi!.

  Pia ni sheria ya mfumo dume kuwa baba tuu ndio mwenye jukumu la kutoa matunzo hata kama baba ni jobless na mama ndio mwenye kipato.

  Wanaharakati wa haki za binaadamu/jinsia/watoto wamepiga kelele sana kuhusu sheria hii kupitwa na wakati mpaka sasa hakuna kilichobadilishwa japo ustawi wa jamii na mahakama vimekuwa vikitoa maamuzi kuongeza kiwango cha matunzo from time to time.
   
 3. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  What? yaani kubadili hii sheria iende na wakati nayo ni big deal... kweli Tanzania tuna uhaba wa wanasheria. Mtoto wa siku hizi ukimpa shilingi mia moja kila siku anaikataa, anataka mia mia mbili kwa siku.
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kwa maneno mengine mtoto baada ya kupita miaka 7 anaweza kurudi kwa baba yake? Kwani sheria ya mwaka 1963 Law of Persons Act inasema kuwa mtoto atakaye zaliwa katika ndoa anakuwa wa baba. Vipi kuhusu sheria za ndoa za dini ya Kiislamu, hazipingani na sheria za Mahakama katika hifadhi ya mtoto?
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wanasheria ufafanuzi zaidi hapa, kama baba ana kipato zaidi ya mama na anaweza thibitisha mtoto akiwa na baba anapata mahitaji muhimu kama shule na matibabu lazima awe na mama hata kama ni chini ya miaka 7.....? na kama mama anachelewesha divorce ili apate pesa za matunzo ya mtoto Mahakama zetu Tanzania zalionaje hilo?

  Masa
   
Loading...