Child Adoption - Hali ikoje Bongo?

IROKOS

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
10,187
7,772
Wana JF hivi hili suala la kuasili mtoto (nadhani ndicho kiswahili chake? i stand to be corrected) au adoption kwa Kiingereza kwa hapa kwetu hali ikoje? sheria/sera (kama zipo) zinasemaje? Je linafanyika? Is it something which is becoming popular nowadays?

Nimeomba mawazo yenu kwa sababu utaratibu huu ni common huko kwa wenzetu kama tulivyoona kwa staa madona kumuasili yule mtoto Banda, na wengine wengi tuu. Hivi kwa kungalia mila zetu na desturi zetu, dini na mambo mengine hii kitu ina changomoto gani?

Nimelileta hili suala hapa jukwaani kwa sababu wote ni mashahidi jinsi watoto wanavyotupwa, kuuwawa na kutelekezwa kwa upande mmoja lakini pia kwa upande wa pili tumeshuhudia jinsi ambavyo ndoa nyingi zilivyo kwenye misukosuko kama siyo kuvunjika kabisa kwa kukosa watoto.

Yaani Wewe unamtupa mtoto wakati wenzio wamemaliza mahospitali na waganga wa jadi kutafuta!! Je Kali kuasili kukiwekwa wazi na watu wakaelewa haiwezi kupunguza hili tatizo kwa kila upande kufaidika?? Samahani kama mada hii ilishawahi kujadiliwa humu kabla sijajiunga.
Naomba kuwasilisha.
 
NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
362
Ukweli ni kuwa bado sio swala "popular" na ambalo sijaliona sana likitokea (i stand to be corrected) hasa kwa mtu wa nje ya nchi ku-adopt mtoto. Inawezekana inatokea lakini si kwa kiwango kikubwa sana.........ila ndani kwa ndani najua wapo ambao huwa wanaasili watoto lakini wengi huwa hawafuati procedures za kisheria zaidi ya "on good will and faith" na makubaliano kati ya anaeasili na wazazi wa mtoto au ndugu zake wa karibu. Nililiona hili kwa mtu ambae alifanya hivyo.

Kwa upande wa kisheria ningekushauri upitie Law of the Child Act ya mwaka 2009 ina provisions juu ya adoption ya mtoto.............Unaweza kuisoma hii sheria hapa http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/21-2009.pdf
 
IROKOS

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
10,187
7,772
Thanks Mkuu for sharing this.

Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,442
2,467
sheria ya adoption ipo sikumbuki cap gani ,mahakama kuu wanafanya sana,masharti ninayojua kwa tanzania anaetaka kuasili awe ni mtanzania, awe ktk ndoa, ridhaa ya mzazi au walezi wa mtoto, awe chini ya miaka kumi na nane yaani mtoto, na pia mzazi wa mtoto au mlezi akiri hajanufaika kwa kuruhusu mwanae kuasiliwa, mwombaji ataandika petition ikiambana na viapo vya mzazi mlezi na pia anaeasili na aonyeshe sababu za kumchukua huyo mtoto na pia lazima aonyeshe uwezo wa kumlea mtoto nk.kw aufupi ndio hivo,.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom