Chid Benzi kawa kama zamani big up kwake

Chid Benzi kawa kama zamani big up kwake

Watanzania wafarijika baada ya kuona muonekano mpya wa chid benzi, you know what? GOD DID.
aache kuweka focus zake sana juu ya muziki wamsaidie afanye mambo mengine ndani ya muziki sio lazima aimbe kwa maana stress za ngoma kutokwenda kwa namna ile ambayo alizoea zikimvaa tena lazima ajikute amerudi tena alikotoka.
 
Hoja ni ileile kuacha unga sio jambo rahisi, hilo ni pambano ambalo limeshaondoka na uhai wa wengi​
Wapo walioacha kabisa na ushahidi tunao hakuna pambano lisilokua na Mshindi, kwa hio ninachokwambia kizingatie na ukielewe vizuri
 
chama cha mapinduzi kimekua kikipambana na vita ya madawa ya kulevya kila siku

huyo msanii wa miondoko ya kufoka MUNGU amsimanie azidi kuimarika
 
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Chid Benz, aliyewahi kuwa mraibu wa dawa za kulevya, anatarajiwa kushiriki katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupinga Biashara na Matumizi ya Dawa za Kulevya Duniani, yatakayofanyika jijini Dodoma tarehe 26 Juni 2026.



Uwepo wa Chid Benz unatarajiwa kuwa mfano hai wa ushindi dhidi ya uraibu, na chachu ya kuhamasisha vijana kuachana na matumizi ya dawa hizo. Kupitia ushuhuda wake wa maisha, atasaidia kuelimisha jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya na umuhimu wa msaada wa kitabibu na kijamii kwa waathirika.
download-1.jpg
 

Attachments

  • download-1.jpg
    download-1.jpg
    7.2 KB · Views: 24
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Chid Benz, aliyewahi kuwa mraibu wa dawa za kulevya, anatarajiwa kushiriki katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupinga Biashara na Matumizi ya Dawa za Kulevya Duniani, yatakayofanyika jijini Dodoma tarehe 26 Juni 2026.

View attachment 3381812

Uwepo wa Chid Benz unatarajiwa kuwa mfano hai wa ushindi dhidi ya uraibu, na chachu ya kuhamasisha vijana kuachana na matumizi ya dawa hizo. Kupitia ushuhuda wake wa maisha, atasaidia kuelimisha jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya na umuhimu wa msaada wa kitabibu na kijamii kwa waathirika.View attachment 3381813
Huyu mbona amepona ghafla sana au wamemtoa damu yote wamemwekea mpya..!
 
Back
Top Bottom