Chid Benzi ahukumiwa miaka miwili jela

Chid Benzi ahukumiwa miaka miwili jela

Angepelekwa jela kabisa iwe fundisho kwa wengine.




UKIKOHOA WIKI MBILI ZAIDI NI DALILI ZA AWALI ZA

KIFUA KIKUU NENDA KAPIME

STOP TB
 
Madawa ya kulevya afunge miaka 2 au faini!!!!!!!:A S embarassed:
 
Madawa ya kulevya afunge miaka 2 au faini!!!!!!!:A S embarassed:

With our corrupt system chochote chaweza tokea kwanza kesi imesonga fasta tofauti na nyingine maana watu wanasota miaka mahabusu hukumu hazifiki yeye fasta na yupo mitaani now...
This country bhana
 
hakimu LEMA ni hakimu mla rushwa, alishajadiliwa sana hapa kwenye jf. alichofikiria yeye ni hela tu na sio maisha ya chid benz. kwa usalama wake, kama kweli lema ana huruma alitakiwa asimwache huru, ampeleke ndani ili kule ndani aende akawe mbali na mazingira ya madawa, na apewe rehabilitation medication akiwa ndani jela, akirudishwa mtaani lazima ataendelea.

hakimu LEMA anafikiri amemsaidia, kume amemweka kwenye mazingira ya kufa mapema zaidi. ni sawa na kuruhusu mtoto arudi mtaani ambako kuna simba anaenda kummaliza. angekaa ndani asingemalizwa na simba huyo. hakimu huyu alishalalamikiwa sana kwamba ana rusha, SERIKALI INATAKIWA KUMCHUKULIA HATUA kwasababu hapo haonyeshi kama ana moyo wa kupambana na madawa ya kulevya, anatakiwa kutoa kitu cha funzo kwa wengine na aonyeshe kuwa mahakama ipo pamoja na serikali kupambana na madawa ya kulevya.

gerezan ataharibka zaid,kama hjui gerezan wanakla bangi mda wote
 
Kalipa faini ya shs 900,000 na sasa ameachiwa huru.

Kulipa faini ni jambo la busara? Maana asipokata rufaa na kushinda ina maana katiba hamruhusu kugombea uongozi wowote wa nchi hii?

Thamani ya madawa ya kulevya au bangi huwa inapatikanaje?
 
Huyo ni mtumiaji mkuu. Mi naona wale ma drug dillers ndo wadhibitiwe kwa sheria kali sana.

Ukithibiti watumiaji, hao drug dealers watakosa soko la kuuzia hayo madawa. Lakini ukiwaacha watumiaji, drug dealers watatafuta njia ya kuwafikia watumiaji hata kama watauza madawa kwa gharama kubwa zaidi.
 
Huku sasa ni kuwalea wala unga, mwisho wa siku watatubakia wanetu bureeee

alafu sijui hizo hela za faini huwa zinaenda wapi??/ na hayo madawa wakiyakamata wanayapeleka wapi???
 
Sisi tukikamatwa marungu yanaanzia eneo la tukio mpaka kituoni...na huko unarushiwa sero mpaka afande akukumbuke umeshamaliza miezi miwili...lakini wenzetu...wanapelekwa kama mabibi harusi..na wanatoka kama walienda picnic...dah!!..maisha haya bwana..
 
Sheria za nchi hii hovyo sana,MTU kukutwa na unga laivu faini laki 9 tu??? kumbe ndo maana biashara imeshamiri sana bongo
 
Sheria zingine zimepitwa na wakati,
Hilo ni kosa kubwa lakini faini yake ni sawa na bure tu!
Kwa faini kama hizi madawa hayawezi kuisha daima.
 
hapo alishaenda kumwona akapanga na hakimu kuwa alete fungu lake, aje akubali kosa ili alipe faini aende zake. hakimu huyu ni mla rushwa kuliko ajabu. huwezi kumwachia mtumiaji wa madawa aende mtaani akaendelee kutumia madawa.


Una lako jambo wewe,,,,
 
Huyu alikuwa mpumbafu toka mwanzo...kiasi kile cha bange kilikuwa kina attract fine tu
 
Back
Top Bottom