Hute
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,537
- 6,483
hakimu LEMA ni hakimu mla rushwa, alishajadiliwa sana hapa kwenye jf. alichofikiria yeye ni hela tu na sio maisha ya chid benz. kwa usalama wake, kama kweli lema ana huruma alitakiwa asimwache huru, ampeleke ndani ili kule ndani aende akawe mbali na mazingira ya madawa, na apewe rehabilitation medication akiwa ndani jela, akirudishwa mtaani lazima ataendelea.Adhabu ndogo sana kwa makosa hayo. Hawawezi kuacha kwa faini ya sh laki tisa.
hakimu LEMA anafikiri amemsaidia, kume amemweka kwenye mazingira ya kufa mapema zaidi. ni sawa na kuruhusu mtoto arudi mtaani ambako kuna simba anaenda kummaliza. angekaa ndani asingemalizwa na simba huyo. hakimu huyu alishalalamikiwa sana kwamba ana rusha, SERIKALI INATAKIWA KUMCHUKULIA HATUA kwasababu hapo haonyeshi kama ana moyo wa kupambana na madawa ya kulevya, anatakiwa kutoa kitu cha funzo kwa wengine na aonyeshe kuwa mahakama ipo pamoja na serikali kupambana na madawa ya kulevya.