Wadau naomba kuuliza serikali imeruhusu jamii yetu iathirike na madawa ya kulevya?? Leo mwanamuziki maarufu chidi benz amekutwa na hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin yenye thamani ya takribani milioni 3 na amekiri zaidi ya mara mbili kuwa ni kweli, alikiuwa akitumia madawa hayao na alikuwa mbioni kuacha. Sasa kinachonishangaza ni hukumu aliyopewa, either aliambiwa aende ndani miaka 2, au alipe fidia ya laki 9. Ambayo amelipa; sasa najiuliza hapa wanatoa funzo gani, means wameruhusu watu wauze na kutumia hayo madawa then wakikamatwa walipe fidia tu basi ya tosha..., hapa tunajenga taifa gani ndugu zangu???, huku nyoka wenye makengeza wakijigamba, huku escrow, huku ufisadi kule mauaji ya albino, etc, nchi imekosa muelekeo, tunaelekea wapi??