Chid Benzi ahukumiwa miaka miwili jela

Chid Benzi ahukumiwa miaka miwili jela

Msanii maarufu wa muziki nchini Tanzania,Chid Benz amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au faini ya shilingi laki tisa kutokana na kosa la kukutwa na dawa za kulevya.
====================
11020256_692073264236984_1481213526744442641_n.jpg
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama (Chid Benzi) amehukumiwa kifungo cha miaka mwili jela au kulipa faini ya shingili laki tisa bada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae
Chanzo;ITV Habari.
 
Cha ajabu hata hizo laki tisa utakuta hana....hawa wasanii wetu hawa...uuuuwiiii!!!!!
 
Haya mahaka yetu haya nayo mmh!. Wanafungwa weengine tu.lakini walio iba pesa za uma hawafungwi.wanagoma hata kuhojiwa kwa nini?. Kisingizio cha kijinga kabisa eti kunazuio la .............jibu ulichoulizwa yaani ninahasla.subili kidogo nije.
 
Msanii maarufu wa muziki nchini Tanzania,Chid Benz amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au faini ya shilingi laki tisa kutokana na kosa la kukutwa na dawa za kulevya.

Chanzo;ITV Habari.
ameshalipa faini ameondoka kwa taarifa nilizozipata toka mahakamani leo. ila faini yenyewe laki tisa, alitakiwa kulipa milioni tatu lakini naona alimwona hakimu akapewa laki tisa. ila kihalali, alitakiwa kulipa milioni tatu na ushee au kifungo cha miaka sita sio miwili. ndio hakimu Lema anayesifika kwa rushwa huyo kamwachia dogo.

binafsi ningekuwa hakimu ningemwacha akae ndani tu ili asirudi mtaani akaendelee kubuya unga kwasababu akiwa gerezani angekosa madawa na angetibiwa.
 
Cha ajabu hata hizo laki tisa utakuta hana....hawa wasanii wetu hawa...uuuuwiiii!!!!!
ameshalipa na amesepa mzee, kwa taarifa zenye uhakika nilizonazo sasahivi hapa.
 
Hizi mahakama zetu....yaani alitakiqa apumzike jela bila fain
 
Daah! wangemuweka ndani hata mwezi tu.
 
Kweli Vita ya madawa ya kulevya ni ngumu sana.
 
Hii kesi kwa sisi tunaojuwa sheria ilishaamuliwa nje ya mahakama kilichofanyika leo ni utekelezaji wa makubaliano yalioafikiwa.
1.Laki tisa walikubaliana na hakimu
2.chid alitafuta wa kumlipia na kwenye makubaliano alikwepo
"Eti uhuru wa mahakama labda sayari ya mass sio tz
 
Cheza na hakimu Waliyalande Lema wewe! Alishachukua mchongo wake mapema kama Jaji Werema na Escrow
 
ameshalipa faini ameondoka kwa taarifa nilizozipata toka mahakamani leo. ila faini yenyewe laki tisa, alitakiwa kulipa milioni tatu lakini naona alimwona hakimu akapewa laki tisa. ila kihalali, alitakiwa kulipa milioni tatu na ushee au kifungo cha miaka sita sio miwili. ndio hakimu Lema anayesifika kwa rushwa huyo kamwachia dogo.

binafsi ningekuwa hakimu ningemwacha akae ndani tu ili asirudi mtaani akaendelee kubuya unga kwasababu akiwa gerezani angekosa madawa na angetibiwa.

Kwa hiyo kwa hesabu za haraka Hakimu kala zaidi ya 2,100,000.
 
Msanii maarufu wa muziki nchini Tanzania,Chid Benz amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au faini ya shilingi laki tisa kutokana na kosa la kukutwa na dawa za kulevya.

Chanzo;ITV Habari.
Adhabu ndogo sana kwa makosa hayo. Hawawezi kuacha kwa faini ya sh laki tisa.
 
Kweli Vita ya madawa ya kulevya ni ngumu sana.

Chidy ni mtumiaji wa madawa na syo muuzaji? Mbona Kuna wauzaji wa akamatwa na magunia ya madawa ya kulevya, mbona hatuski wakihukumiwa
 
Hukumu ya wagonga nyundo hainaga fine, may be cort huasume kuwa hawawezi kulipa. Hata chenge kwakuua alitozwa fine! Nchi Hii kuwaa maarufu ! Ukishindwa jukwaani hata jf kuwa maarufu tuu
 
Back
Top Bottom