Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,668
- 167,614
Huku sasa ni kuwalea wala unga, mwisho wa siku watatubakia wanetu bureeee
Mkuu kisheria ni sahihi. sababu kubwa ni kukiri kwake kosa mapema na kutokusumbua mahakama. Na pia kuomba msamaha kwa kutoa sababu kadhaa wa kadhaa. ikiwemo udogo wa mzigo aliokutwa nao pia ilikua sio biashara..
Mkuu nimekuelewa.
Ila kwa mtindo huu, vita dhidi ya madawa ya kulevya TZ itabaki kuwa historia. Masogange nae alichoropoka hivihivi.
Na ndio maana kapata adhabu ndogo. Ukizingatia kakiri kosa. Ngoja akamatwe tena ndio ataijua mahakama. Amuulize chekaChidy ni mtumiaji wa madawa na syo muuzaji? Mbona Kuna wauzaji wa akamatwa na magunia ya madawa ya kulevya, mbona hatuski wakihukumiwa
Kalipiwa sasa sijui atairudishaje
Hizi mahakama zetu....yaani alitakiqa apumzike jela bila fain
hawezi kosa laki tisa.Hiyo jamaa ni maarufu sana.
Uko sahihi mkuu, ila lazima ukumbuke adhabu hupungua kutokana na sabab zinazomridhisha hakimu. Ila kuachiwa huru bila adhabu haiwezekani..sasa mbona kwenye kifungu cha possession naangalia hapa, alitakiwa kulipa milioni tatu kwa hizo count tatu alizoshitakiwa nazo, miliono moja kila count na ni mandatory kuna neno "shall". ilikuwaje alipe laki tisa kwa count tatu?...
kakosea sana, angeenda jela, ili akitoka aje na verse mpya nyingi,
Unaweza shindwa mkuu maana watu wanaweza kukususa si unajua laki 9 ela ndefu hasa katika mazingira ya kesi na ukizingatia unatakiwa ulipe katika kipindi kifupi (huwa inapatikana kwa haraka kutokana na ndugu kuepuka lawama na fedheha kutoka kwa walimwengu utasema walimtuma)angeshindwa kulipa ningemshangaa.....
Tunalia na kupiga kelele kuhusu madawa ya kulevya, halafu eti mtu anahukumiwa miaka miwili au faini ya shilingi laki tisa? Bora China wananyonga maana huu upuuzi wa madawa ya kulevya hauwezi kuisha kama adhabu zenyewe ndio hizo za kipuuzi.