Kiungani
JF-Expert Member
- Feb 2, 2007
- 274
- 71
Awali ulisema hivi;
Na sasa unasema hivi;
Hii nayo inahitaji rocket scientist?
Masatu, rejea mtundiko wako hapo juu ukijibu mtundiko wa Enigma.
Bila kuchagua upande, ni vizuri uelewe tu namna jengo la bunge linavyofanya kazi.
Wabunge na wageni wana muda maalum wa kuingia kwenye ukumbi mkuu wa mijadala wa bunge. Wafanyakazi wa bunge (si wote) na waandishi (pia si wote), wanaruhusiwa kuwa maeneo kadhaa ya ukumbi mkuu hata kama huo si muda wa wabunge na wageni kuwepo. Waandishi wengi huwa wanakuwa kwenye media room inayoangalia ukumbi kwa chini, aidha wakimalizia reports zao au wakikamilisha kutuma reports kwenye vituo vyao vya kazi. Ni nadra sana kuwakuta wabunge ndani ya ukumbi baada ya milango mikuu kufungwa, ila ni rahisi sana kuwaona waandishi na wapiga picha katika maeneo ya juu yanayozunguka ukumbi (siyo ndani ya ukumbi wenyewe) hadi usiku sana.
Kinachoshangaza ni kwa nini (kama kweli) Chenge aliachiwa akaingia peke yake? Kawaida wabunge wakisahau vitu ndani, na inatokea mara nyingi sana, aidha ataingia mbunge na ushers au ataingia usher na kumletea mbunge vitu alivyosahau. Nimeona pia mara kadhaa wabunge wakiwatuma madereva kurudi na kuchukua vitu walivyosahau ndani, na ni ushers ambao huingia na kuleta.
Nadhani hiyo ya Chenge (kama ni kweli) itakuwa tu ni 'za mwizi ni arobaini..' kama hata watu wa TV walikuwa hawajamaliza kazi zao na cameras zilikuwa bado ON. Security cameras ziko ON masaa 24, na labda 'mtu' alipitiwa kwa hilo.