Enigma
Senior Member
- Feb 29, 2008
- 109
- 62
Mbunge wa Bariadi Magharibi Bw. Andrew Chenge ameanza kuandamwa na tetesi nyingine za mambo ambayo endapo yatamnasa kweli basi itakuwa vigumu kwake hata kuendelea na Ubunge wake.
Vyanzo vya kuaminika vimethibitisha kuwa siku ya Jumanne baada ya kikao cha wabunge wa CCM Bw. Chenge aliomba udhuru wa kurudi ndani ya ukumbi wa Bunge ambao ulikuwa tayari umefungwa. Alifunguliwa na Afisa mmoja wa Bunge ili kwenda kuchukua/kufanya alichotaka kwa dakika chache.
Seti mbili za Kamera ziliweza kumnasa akijongelea eneo la kiti cha Spika na baadhi ya wabunge ambao majina yao yote tunayo na ambao walishiriki kwa namna moja au nyingine katika kuanguka na kuvunjika kwa serikali ya Waziri Mkuu Lowassa.
Mojawapo ya seti za Kamera ni zile za Star TV na zile za Usalama wa Bunge. Inadaiwa nakala za tukio hilo tayari lilikopiwa na "wajanja" kabla ya kutoa taarifa kwa uongozi wa Bunge ambao inasemekana wamechukua nakala originals za tukio hilo ili kupitia na kuona nini kimefanyika.
Kukumbushwa kwa tukio hili kumekuja hasa baada ya mmoja wa wabunge ambao inadaiwa Bw. Chenge aliwatembelea "kupangusa" viti vyao Dr. Harrison kuugua kwa ghafla. Hata hivyo haijulikani kama kuugua kwa Mwakyembe kuna uhusiano wowote ule na "movements" za Chenge siku mbili zilizopita.
Sasa hivi Dr. Mwakyembe anapumzika nyumbani.
Japo yawezekana kuwa jambo hili hili halina lolote lakini mlolongo wa matukio kadhaa katika historia ya Tanzania yamekuwa yakiwafanya watu wengi kuwa na wasiwasi sana kuhusu maisha ya wale wanaoonekana kuwajali na kuwatetea na hivyo tetesi zozote za "mkono wa mtu" zinasumbua kweli.
Kuna kila dalili jambo hili litafahamika masaa machache yajayo kwani inadaiwa kuwa hata kama ni kweli imetokea serikali haiko tayari kuona mmoja wa wabunge anahusishwa na kitu chochote ambacho kimsingi kinaendana na mambo ya uhalifu. Uongozi wa Bunge inadaiwa wanalifuatilia jambo hili kwa kina ili kuwa kujua ukweli ni upi.
Hata hivyo, yaonekana wazi kuna suala zima la chenge, Star TV na Utaalamu mambo leo ambao wengi wanaufikiria ni "ushirikina" kumbe ni sayansi ya kisasa ya kushughulikia watu.