Chenge, StarTV na Utaalam wa kisasa

Wewe Kitila, utakuwa kiongozi wa Tanzania bila ya kwenda Bagamoyo? Vipi mkuu unafikiri ni bure? Wakuu kina Zitto wanahitaji kukufunda mkuu,

Yaani bila sangoma na songi songi itakuwaje huwezi kuwa hata katibu tarafa vipi mkuu chi yako unakuwa kama mgeni?

Ndiyo maana uchaguzi mkuu 2005 masangoma wa dunia nzima walijaa Dodoma
 
Labda hizo Camera za usalama lakini hilo la Star Tv mmmh ukumbi wa bunge ukifungwa waandishi wote na zana zao wanatoka iweje hizo camera za Star Tv zikabaki open kama CCTV camera?

Masatu na wengine, kwa taarifa ni kwamba siku hiyo ilikuwa kuna kikao cha CCM na inapokua hivyo wapiga picha wa TV binafsi wanatakiwa kuondoa kamera zao na kinapoisha wanaweza kuzifunga na kuunga vinasa sauti vyao kwa ajili ya kikao cha siku inayofuata, ili asubuhi kunapokaguliwa na kufanywa usafi wasiguse kitu. Sasa walipoingia juu ya ukumbi wakiwa kazini wakaona watu wanaingia ndani ya ukumbi baada ya waheshimiwa wote kutoka, ndipo wakamuona mzee wa vijisenti akisindikizwa na ofisa mmoja wa Bunge. Mwanga haukua mkali maana hawakuwasha taa bali walitegemea mwanga wa taa za juu ya ukumbi. Kutokana na mwanga kuwa mdogo, taarifa rasmi zinasema camera za usalama za bunge zinaonyesha watu lakini bila kuonyesha sura halisi na kinachofanyika ni utaalamu wa juu zaidi kuweza kubaini ni kina nani hasa.

Kwa wale wanaolihusisha suala hili na imani za ushirikina wanaweza kufanya makosa makubwa sawa na waliohusisha ugonjwa wa Amina Chifupa na ushirikina hadi mambo yalipoharibika ndio wakampeleka Lugalo. Ushirikina unaweza kuwapo lakini isiwe jambo la msingi kwa sasa. Jambo la msingi kwanza ni kuangalia mambo ya kitaalamu zaidi, kujua ni kemikali za aina gani zilizomwagwa katika viti vya waheshimiwa hao, ili hatua za haraka na za kitaalamu zaidi zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kusafisha eneo husika na kuwafanyia vipimo vya kisasa kabisa wahusika wakuu akiwamo Dk. Mwakyembe na jirani zake pale ndani ya ukumbi. Spika kwake nadhani hakuna madhara kwa kuwa kiti cha Spika kinaweza kubadilishwa na kipo cha akiba lakini kwa wabunge ni vigumu kubadilisha kwa haraka. Na kama hakikubadilishwa basi wote wawili Naibu Spika na Spika watalazimika nao kufanyiwa uchunguzi wa afya zao kwani Jumatano ambayo ni siku moja baada ya tukio la aina yake kutokea, Spika hakukalia kiti na Bunge liliongozwa na Naibu SPika. Habari rasmi zinasema hadi sasa uchunguzi wa kina unaendelea na kamera zote zinapitiwa kwa sasa kuweza kubaini kilichotokea.

Kama nilivyosema awali suala la ushirikina hapa si mahala pake wanaoamini waendelee kuamini na wasioamini wabaki na imani zao za kidini japo katika dini zote uchawi unatajwa na hata hao watu wa mataifa yaliyoendelea ni washirikina lakini kuna majukwaa yao ya ushirikina si JF labda kama wataanzisha sehemu maalumu na sii hii ya Jukwaa la SIasa. Inasikitisha maana hata wana usalama wanaofuatilia suala hili baadhi wanahusisha na ushirikina hata kabla ya kumaliza kazi yao. Inadaiwa kwamba polisi waliokua wakienda kulinda nyumbani kwa Chenge kuna wakati wanapotea nyumba. Polisi mmoja Dar es Salaam anasema kuna wakati mwingine (si mara zote) wanaachwa na gari nyumbani kwa Chenge na gari linapoondoka wakiangalia nyumba hawaioni wanazunguka na kurudi kituoni na anapokwenda askari mwingine mambo yanakua yale yale hadi asubuhi. Hii inasikitisha maana wapelelezi wanatakiwa wajiepushe kwanza na ushirikina kuweza kufanya uchunguzi wa masuala nyeti.
 
Hayo ya Chenge ni makubwa, kama unazama na maji yamefika shingoni unaweza kufanya vituko. Kama story ni ya kweli hiki kitakuwa kituko na aibu na wala usitegemee kwamba kitashughulikiwa.
 
Mkuu Halisi shukrani kwa data zako mzee,

kina Masatu na KM wanabisha makusudi lakini hapa kuna swala moja la msingi sana.Cha muhimu ni kuweka ushirikina kwanza pembeni na kudeal na swala hili kitaalamu.Lakini hata hivyo ni muhimu pia kwa wanaoamini kwa masangoma kufanya hivyo pia,kwani kuna ndungu yangu mmoja naye katika mambo haya ya ubunge alienda kuchinga kuku mweusi makaburini usiku wa manane.Ni swala ambalo nalifahamu kabisa.So kudismiss ushirikina kwa siasa zetu za kiswahili sipendi hasa.

Anyway mambo yatakuwa wazi kadiri muda unavyosogea,kwani ilianza kama tetesi tu na sasa inazidi kudhihirika kuwa kun kitu kimefanyika.
 
Labda hizo Camera za usalama lakini hilo la Star Tv mmmh ukumbi wa bunge ukifungwa waandishi wote na zana zao wanatoka iweje hizo camera za Star Tv zikabaki open kama CCTV camera?

I smell something very fishy kwenye bandiko hili....

Kweli...Lakini isivumishwe sana!! haina maana!!
Ila ONYO kwa Chenge...angalia usiendeshwe sana na hao wano kuendesha!!
Ni upumbavu!!!....Kama ni akili basi fanya haraka tuone!!
 
Je ikiwa ni kweli alirudi na akapangusa viti hivyo na ikathibitika,sheria gani itakayo mbana?
 
Jamani mwacheni Chenge Vijisenti wetu, alikuwa ni msukule/mzuka wake ulioingia kwenye Madhabahu ya Serikali kumwaga uchafu wa kisayansi.

Maana huu Msukule ulisahau kuwa kuna kamera za ulinzi 24 hours, labda alikuwa amelewa pombe au bangi, fanyeni vipimo vya damu!
 
UDAKU......

mkulu kuhani mkuu usinichokonoe nakunipatia sababu ya kuanza kunusa uchafu ambao naamini wengi wenu humu mnaufukia kwa maandishi ya kistaarabu jamvini. mimi ni inzi sijali wapi nitanusa next
 
Naamini kila kitu kitawekwa wazi baada ya uchunguzi wao. Lakini Mh. Mwakyembe alidai hali hiyo ilikuwa ni kawaida kutokana na Blood Pressure, huenda ilishawahi kumtokea. Pamoja na hayo hiyo isiwe sababu ya ku-dismiss hayo yanayoongelewa hapa maana MAFISADI this time wanataka kuzidi kuonyesha UMMA kuwa wao hawawezeki. Siku yaja na wala haiko mbali kwa MAFISADI kukiona cha Mtema Kuni.
 
sema wewe halisi nikisema miye inzi watasema nimezidi uchafu
 
Nafikiri kutokana na haya siasa za tanzania kwa wale wataalamu wa mambo ya jamii wanaweza kutoa PhD kibao. Hapa siyo mambo ya kutembea na vitabu vya akina OBAMA na mwenzake.

Lakini kikubwa sana nafikiri ingetakiwa wamfanyie Chenge uchunguzi ikibidi waingereza warudi hili waangalie maswala ya kemikali.

Nafikiri pia Wabunge wafanye proposal ya kukaguliwa wakati wanaingia Bungeni naona maisha yao yako hatarini.
 
Je ikiwa ni kweli alirudi na akapangusa viti hivyo na ikathibitika,sheria gani itakayo mbana?

Malila,

je pia ni kwa utaratibu/kanuni gani zilimruhusu "kupangusa" viti vya weniwe (sio chake) including kile cha Spika?

NB: 1. Ilisemwa kuwa ALISAHAU kitu ndani,sio KUPANGUSA.
2. Kazi ya KUPANGUSA ni ya wahudumu wa Bunge.

Hivyo kwa swali lako hilo Chenge ana mwaswali 1,000,000+ ya kujibu.
 
Masatu na wengine, kwa taarifa ni kwamba siku hiyo ilikuwa kuna kikao cha CCM na inapokua hivyo wapiga picha wa TV binafsi wanatakiwa kuondoa kamera zao na kinapoisha wanaweza kuzifunga na kuunga vinasa sauti vyao kwa ajili ya kikao cha siku inayofuata, ili asubuhi kunapokaguliwa na kufanywa usafi wasiguse kitu. Sasa walipoingia juu ya ukumbi wakiwa kazini wakaona watu wanaingia ndani ya ukumbi baada ya waheshimiwa wote kutoka, ndipo wakamuona mzee wa vijisenti akisindikizwa na ofisa mmoja wa Bunge. Mwanga haukua mkali maana hawakuwasha taa bali walitegemea mwanga wa taa za juu ya ukumbi. Kutokana na mwanga kuwa mdogo, taarifa rasmi zinasema camera za usalama za bunge zinaonyesha watu lakini bila kuonyesha sura halisi na kinachofanyika ni utaalamu wa juu zaidi kuweza kubaini ni kina nani hasa.

Taarifa za nani hizo?

Mbona wanaosemwa wamesema hawataki kujulikana wamesema?

Anonymous sources zinapunguza credibility ya habari.

Mtu akisema "jina tunalo" au "taarifa za kuaminika zinasema" hiyo haina maana nikuamini kwa sababu tu umesema. Taarifa kama hizo zinaendana na tabloid journalism, au Kiswahili, udaku.

Kuna namna ya kutumia anonymous sources katika jinsi ambayo inaliwajibisha gazeti kama tukikuta ni habari za uongo. Wanaweza kusema kitu kama "taarifa hizi zimedhihirishwa kutoka kwa Kiongozi ambae ametaka jina lake lisitajwe." Hapo tunajua gazeti kwa nini imeficha jina, na tunajua gazeti limejiweka nyuma ya hii stori, kwamba wanatuahidi wamedhihirisha huyu anonymous. Tukikuta ni uongo, ni gazeti ndilo responsible na haliwezi kujisafisha kwa kutupa mpira kwa mtu baki ambae hajulikani!

Kwa sababu hawafundishi hivi vitu Nyegezi na UDSM, ngoja tupelekane shule hapa hapa.
 
"Ni kweli, Matatizo ya Ufisadi yamemwingiza Chenge kwenyeUshirikina"
Nalazimika kuchangia kutokana na attitude ya kupenda shorcut ya Pundit na Kuhani Mkuu ya kuita kila kitu wasichokijua kuwa "udaku". Hawaelewi kuwa huku Bongo wanasiasa, viongozi wa dini, timu za mpira n.k. hujipanga uchi wa mnyama wakiomba vyeo na ushindi Mlingotini, Bagamoyo na sehemu zingine zenye "mafundi" wa asili. Hivyo si kitu cha kuwashangaza hawa wenzetu, sijui wanaishi Ulaya, kwa Chenge, Msukuma, aliyekulia katika mazingira ya ushirikina ya kuua vizee vyenye macho mekundu, kuwanyunyizia Wabunge wenzake "nyuklia" za Kisukuma ili asiandamwe na sakata la rada na vijisenti. Mimi niko Dodoma na waandishi wa habari wenzangu ambao tumeshuhudia tukio hilo! Mzee wa vijisenti kamimina vibuyu viwili vizima kwenye meza na kiti cha Spika, Naibu Spika, na wabunge machachari akina Ole Sendeka, Anne Kilango, Mwakyembe, Manyanya, Selelii, Mnyaa, Slaa, Mwambalaswa, Zitto, Mkumba na wengineo. Hili ni suala very serious ambalo lazima Bunge lilifanyie uchunguzi wa kina. Vibuyu vya Chenge vinaweza kuwa na pilipili ya Kiafghanistan yenye madhara ya muda mrefu. Tayari tunaambiwa mmoja wa vinara wa Richmond anaumwa! Inawezekana kabisa inatokana na ndumba za Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Chenge! Acheni mzaha, nchi imekwisha! Lazaros
 
Kuhani.. nchi zilizoendelea zinalinda sources pia... si kweli kwamba watu wakiandika habari basi hadi majina yao yajulikane. Umesahau skendo ya Watergate? Na zipo nyingi kila kukicha ambapo vyanzo vya habari vinalindwa sana... au umesahamu mambo ya Valerie Plamer..?

Ukiona watu tunaandika kwa uhakika ni kwa sababu sources hizo ni impeccable... tatizo ni kwamba wakati mwingine u kiitaja source ni rahisi sana kwa wajanja kufanya elimination na kujua source ni nani...
 
Angalau sasa watu watakoma kidogo kumfuata fuata Chenge. Kila siku makelele tu ambayo hayana msingi wowote. Tulieni tujenge nchi ndugu zangu na kuacha majungu. CCM hakuna mafisadi wowote na huyu Chenge anasingiziwa tu.
 
Taarifa za nani hizo?

Mbona wanaosemwa wamesema hawataki kujulikana wamesema?

Anonymous sources zinapunguza credibility ya habari, ndio maana media za nchi zilizoendelea haziandikai habari hivyo.

Mtu akisema "jina tunalo" au "taarifa za kuaminika zinasema" hiyo haina maana nikuamini kwa sababu tu umesema. Taarifa kama hizo zinaendana na tabloid journalism, au Kiswahili, udaku.

Kuna namna ya kutumia anonymous sources katika jinsi ambayo inaliwajibisha gazeti kama tukikuta ni habari za uongo. Wanaweza kusema kitu kama "taarifa hizi zimedhihirishwa kutoka kwa Kiongozi ambae ametaka jina lake lisitajwe." Hapo tunajua gazeti kwa nini imeficha jina, na tunajua gazeti limejiweka nyuma ya hii stori, kwamba wanatuahidi wamedhihirisha huyu anonymous. Tukikuta ni uongo, ni gazeti ndilo responsible na haliwezi kujisafisha kwa kutupa mpira kwa mtu baki ambae hajulikani!

Kwa sababu hawafundishi hivi vitu Nyegezi na UDSM, ngoja tupelekane shule hapa hapa.

weye kuhani saa nyingine unakuwa kana mgema aliyesifiwa...... habari ni habari, mtoa habari anasababu zake za kutotaka kujulikana. time is the mother of all truths. tui la kwanza na la pili na hata lile la tatu la nazi limeshaenguliwa kwenye habari na wanaforum wameshalishwa. uchambuzi wako wa machicha yaliyobakia hautokufikisha mbali...... kwa uelevu uliokwisha onesha hapa ni bora hayo machicha uyatengenezee kashata tu. nd'o maana nyani wa ngabu saa nyingine huwaambia weye na pundit wako, uchambuzi wenu mwingine huwa ni ubishi ulio pumba. ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiip natoweka. hewala.
 
Mkuu kuhani naomba uchaguzi ujao njoo ukakae tanzania ukayaone. Halafu ujaribu tu kugombea nafasi yoyote.
 
Back
Top Bottom