Chenge: Mimi ni nyoka mwenye makengeza msaka pesa

Chenge: Mimi ni nyoka mwenye makengeza msaka pesa

Mkono mwenyewe alikuwa anachaji laki moja kwa one hr as consultation fee mwaka 2009 haijalishi ni kampuni au individual.
kazi ya Mkono ilikuwa ni nini? na alifanya kwa nani?
 
Yaah ndo mfano wa mwanaume mtaftaji... sio kushinda jf kupiga kelele na kulalamika kama mwanamke kutwa nzima. Acheni wanaume watafte pesa, kama mmechagua kushinda kwenye keyboard kutwa nzima, mnalalamikia nini wanaume wenzenu wasaka pesa? Dunia hii nani asiyetaka pesa za kumhakikishia maisha ya kesho.

PASCO (alisema tanzania ni shamba la bibi.)

We utakuwa ni jambazi si bure.Mko tayari kutoa maisha ya watu ili mpate Pesa!.Unajua hasara ambazo taifa limepata
kwa huyo unayemsifia, kutuingiza kwenye mikataba ya hovyo?.
 
Hatimaye Andrew Chenge amefunguka na kudai kuwa yeye ni mjanja wa kutafuta pesa hivyo hatishiki kwa maneno yanayosemwa juu yake.

Ameenda mbele zaidi na kujifananisha na nyoka mjanja mwenye makengeza ambaye ni hodari katika kuvizia fursa zilizoko mbele yake.

Chenge amekuwa na kashfa nyingi sana za ukwapuaji wa fedha za umma kupitia njia za ujanja ujanja hasa kwa kutumia nafasi zake za madaraka. Ifahamike kuwa kila kashfa kubwa ya wizi wa fedha za umma huwa yumo.

Je, ni kusema kuwa Chenge ameshindikana au siku ipo inakuja atajutia ufisadi wake?

Chanzo: Uchambuzi wa magazeti 18.02.2015

Huyu ndie mkuu wa maadili kwenye chama chetu cha ccm
 
huyo ndio Mzee vijisent na nyoka msaka noti
hii inamaanisha hata msemeje yeye bado ni jogoo ndani ya ccm na hakuna wakumfanya chochote
 
Mh. Chenge anatuumiza vichwa akiwa na makengeza tu je akiwa na vichwa

nyoka.jpg
 
huyo ndio Mzee vijisent na nyoka msaka noti
hii inamaanisha hata msemeje yeye bado ni jogoo ndani ya ccm na hakuna wakumfanya chochote
 
Yataisha tukimpata kiongozi bora uchaguzi mkuu 2015
 
Andrew Chenge vijisenti, joka macho makengeza, fisadi, hujumun, dhuluma ni matokeo ya ujinga wengi kuendelea kuchagua CCM, yaani wewe kwa akili yako unaamini propaganda za form four leaver na katibu wake msanii msanii anayepita kushirikiana na wananchi kulalamika dhidi ya mwenyekiti wa chama chake.

sisi wajinga ndio maana chenge bado yupo hai, sisi wapumbavu ndio maana chenge bado anashika nyazifa, sisi wapuuzi ndio maana chenge bado anatutungia sheria na kutuwakilisha bungeni.

kubwa kuliko yote sisi tutaopiga kura NDIO kwa hilo LIKATIBA alilohariri huyu JOKA MAKENGEZA CHENGE, sisi mbwa ikipita hii
 
joka litakalolala mavumbini one day na kuyaacha mabilioni ya umma lililoyaiba watu wanyonge. huko jehanam joka hili litajibu kuhusu wizi wake wote kwa majoka menzie ya huko!
 
Chenge kujifananisha na nyoka imekumaliza katika siasa ya kiungwana.Lakini kujinadi kama nyoka hatari mwenye makengeza ni kuonyesha umwamba wako na kuwaonya watawala na CCM kuwa hukamatiki kwani uliwapuputisha Vieleele Nape na aliye kuwa katibu mkuu wa CCM Mukama waliposhindwa kukuvua gamba.Ila hivi kweli wewe ni mwanasheria uliobobea wa Havard mbona hakuna hata kesi mmoja yenye mashiko kushinda kwa maslahi ya Taifa wakati ukiwa mwanasheria mkuu?Au hao wazungu ni black mamba na wewe ni kifutu?
 
Hii inaonesha kuwa nchi hii woga umeisha. Inakuwaje mtu anasimama bele ya kadamnas na kujidai kuwa anaiba kwa niaba yao? Iweje watu wafurahie mtu kuiba kwa niaba yao? Sijawahi kusikia kuwa mahakama imemuachia mwizi kisa kaiba kwa ajili ya watoto wake. Inabidi tujitathmini kwa haya.
 
Ameenda mbele zaidi na kujifananisha na nyoka mjanja mwenye makengeza ambaye ni hodari katika kuvizia fursa zilizoko mbele yake.

Chenge amekuwa na kashfa nyingi sana za ukwapuaji wa fedha za umma kupitia njia za ujanja ujanja hasa kwa kutumia nafasi zake za madaraka. Ifahamike kuwa kila kashfa kubwa ya wizi wa fedha za umma huwa yumo.

Je, ni kusema kuwa Chenge ameshindikana au siku ipo inakuja atajutia ufisadi wake?

Chanzo: Uchambuzi wa magazeti 18.02.2015

Hapo kwenye red ndio pamenigusa, kumbe kuna nyoka wa aina hiyo eeeh.
 
Yaah ndo mfano wa mwanaume mtaftaji... sio kushinda jf kupiga kelele na kulalamika kama mwanamke kutwa nzima. Acheni wanaume watafte pesa, kama mmechagua kushinda kwenye keyboard kutwa nzima, mnalalamikia nini wanaume wenzenu wasaka pesa? Dunia hii nani asiyetaka pesa za kumhakikishia maisha ya kesho.

PASCO (alisema tanzania ni shamba la bibi.)

Uaminifukazi ongea vizuri na NJAA yako; kwa faida yako tu UK wa 22-23 wa Katiba inayopendekezwa Oktoba, 2014 na nukuu " Kanuni za uongozi wa umma 29-(1) Kiongozi wa umma, akiwa katika kazi za ofisi au kazi binafsi au wakati amejumuika na watu wengine, atahakikisha kwamba mwenendo wake: (a) hauruhusu kutokea mgongano wa maslahi binafsi na maslahi ya utumishi wa umma; (b) hauruhusu hadhi ya ofisi anayofanyia kazi; kwa njaa zako Uaminifukazi huyu bwana wako unayemtetea kwa kutuibia fedha zetu amejiandikia Katiba itakayomlinda ili aendelee kutuibia tu..........:rockon:jiangalie wewe na kizazi chako huna mkataba wa kudumu na Mwenyezi Mungu wewe na mimi tutaondoka lakini vizazi vyetu vitaendelea kuishi kwa tabu na utaendelea kupata laana mpaka siku ya mwisho wakati ukiwa kaburini.
 
Soon tutasikia tena NYOKA MAKENGEZA KAPIGA DILI LINGINE TENA
 
Mtazamo wangu labda utawashangaza
kwa hili
mie namkubali na kumuunga mkono 100%
Kwa manake hajasema uwongo.
kwa sababu angedanganya angesakamwa
haya kasema ukweli bado mwamsakama.
HAPO NDIPO TULIPOFIKA.
Maneno maneno hayasaidii piga kazi upate rizki.
Je? ni mtanzania gani asiyepiga deal?
kama kweli yupo huyo ni zobanangai.
Tuache wivu wa ''kike'' tupige ''deal'' ''kazi''
Kwa sasa hivi TZ,haki,halali = na kiini macho
Amkeni----Mbaya kuuwa.
 
Back
Top Bottom