Chenge: Mimi ni nyoka mwenye makengeza msaka pesa

Chenge: Mimi ni nyoka mwenye makengeza msaka pesa

Yaah ndo mfano wa mwanaume mtaftaji... sio kushinda jf kupiga kelele na kulalamika kama mwanamke kutwa nzima. Acheni wanaume watafte pesa, kama mmechagua kushinda kwenye keyboard kutwa nzima, mnalalamikia nini wanaume wenzenu wasaka pesa? Dunia hii nani asiyetaka pesa za kumhakikishia maisha ya kesho.

PASCO (alisema tanzania ni shamba la bibi.)

Chenge ni mwanaume mtafutaji?
Anafanya biashara gani na sisi tuige tupige hela ndefu?
 
Katika hali iliyoniacha mdomo wazi, kwenye kipindi cha watanzania tuzungumze magazeti cha rfa, imesikika kwenye moja ya magazeti Mh. Vijisenti Bwana Endrew Chenge akisisitiza kwamba yeye co mwizi au fisadi kama wengi tunavomwita bali yeye ni nyoka mjanja mwenye makengeza mtafuta pesa, amejitetea kwamba yy anajitahd kutafuta pesa kwa ajili ya wananchi wa bariadi west, tukumbuke pia huyu ktk harakati za chama chake kujivua gamba alishawahi kusema yeye gamba lake limekwamia kiunoni mwenye shoka aende akalimalzie, lakin pia tusisahau kwamba huyu ndie alikua mwenyekiti kamati ya uandishi katiba pendekezwa ambayo inapgiwa chepuo na serikali ya CCM, nakusihi kasome ibr ya 29 ibr ndg 2b, then unganisha na hz kauli za mh.joka vijisent, then ng'amua mwenyewe kupga kura aidha ya hapana au ndio kwa katiba ya Joka Makengeza Msakapesa.. Tafuteni hlo gazeti mimi nipo kijijn mda huu

Haya ndiyo matokeo ya Mkuu wa nchi kuwa MPENDA, NA MLA RUSHWA. Katika ngoma ya Vigodoro ni mchezaji yupi atamwambia mwenzie kuwa yupo UCHI WAKATI WOTE WANACHEZA NGOMA HIYO???
 
Yaani kila anaechangia hapa ni kulalamika tuu. Mpaka Watanzania mtakapoacha kufikiria kwa kutumia ma.sabu.ri ndio nchi hii itanyooka
 
Sasa iliyobaki watanzania wazalendo tupambane na hili Joka, Chenge hajakosea kujiita Joka ni sumu kali kwa taifa hili,hizi dharau zake zina mwisho walikuwepo makamanda hatari waliotishia dunia yote leo hii wako wapi? Hata naye dharau zake zina mwisho......the time will tell.......
Cc: Elli na BAK
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Safi Sana chenge umesema vyema na uko na haki kusema hivyo kwa sababu sisi watanzania Sinai maboya atujui lolote atuna maamzi uchaguzi huu tena tunakwenda kukupa Serikali na uwenda ukawa waziri mkuu vizuri Sana Mzee change chief wa wawa sukuma hongera kuwa nyoka mwenye makengeza unayejua kutafuta Pesa.
 

18th February 15
Chenge: Mimi ni nyoka

Anceth Nyahore
Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge, ‘amefunguka’ kuhusu kashfa inayomkabili ya kupata mgawo wa Sh. bilioni 1.6 kutoka kwenye fedha zilizochotwa kifisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), akisema hastahili kuitwa mwizi, bali anapaswa kuitwa ‘nyoka wa makengeza’.

Amesema anapaswa kuitwa ‘nyoka wa makengeza’ kwa kuwa yeye ni mjanja wa kutafuta fedha kwa ajili ya wananchi wa jimbo lake, ambao wanapaswa kupuuza madai ya wizi yanayoelekezwa kwake, badala yake wamwamini zaidi.

Chenge, ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) mstaafu, alisema hayo wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mahaha kata ya Bunamala, Wilaya Bariadi mkoani Simiyu juzi.

Alisema kwa muda mrefu amekuwa kimya, lakini ameshangazwa na kitendo cha kuandamwa kuhusiana na kashfa ya akaunti hiyo.

“Wanasema Chenge na Escrow…Pale nimeenda kutafuta kwa ajili ya wananchi wa jimbo langu wala sikwenda kubomoa duka. Bali tunatumia akili kutafuta pesa kwa ajili yenu,” alisema Chenge.

Chenge alitoa kauli hiyo wiki chache baada ya kusimama bungeni na kusema amelazimika kufanya hivyo baada ya kumvumilia Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, aliyetaka wabunge wachunguzwe kuhusiana na kashfa ya akaunti hiyo na wa kwanza kuchunguzwa awe Chenge.

Alisema kama Mdee ana ushahidi wa tuhuma anazozielekeza kwake, aupeleke bungeni kama kanuni za Bunge zinavyotaka au tuhuma hizo akaziseme nje ya ukumbi wa Bunge.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ningelipenda Bunge hili liendelee kuwa na heshima yake. Pili, naomba sana hayo wanayoyasema wawe na ujasiri wa kwenda kuyasema nje ya ukumbi huu wa Bunge, wasijifichie katika immunity (kinga) ya Bunge,” alisema Chenge.

Alisema anayo mengi ya kusema, lakini kwa sababu alisimama kuhusu utaratibu, kumtaja yeye kwa jina moja kwa moja, anaomba aweke ushahidi mezani.

Mdee alitoa pendekezo hilo wakati akichangia mjadala kuhusu taarifa ya PAC na ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), bungeni, Januari 30, mwaka huu.

Alisema Chenge amekuwapo katika kashfa mbalimbali za ufisadi, kuanzia ile inayohusu mikataba mibovu.

Kashfa nyingine za ufisadi ambazo alisema Chenge ameshiriki ni pamoja na inayohusu kampuni ya kufua umeme ya Independent Tanzania Limited (IPTL).

Nyingine alisema ni ya hivi karibuni ambayo alipata mgawo wa Sh. bilioni 1.6 zilizochotwa kifisadi katika akaunti hiyo.

“Tuanze kuchunguzana wabunge, tuanze na Chenge,” alisema Mdee.

Kauli hiyo ya Mdee ndiyo iliyoonyesha kumkera Chenge na kulazimika kusimama bungeni siku hiyo na kutoa kauli hizo.

Kwa mujibu wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), fedha zinazodaiwa kuchotwa kutoka akaunti hiyo, ni zaidi ya Sh. bilioni 300 wakati kwa mujibu wa Rais Jakaya Kikwete, ni Sh. bilioni 202.9.

Chenge alitajwa kupata mgawo huo kutoka katika fedha hizo na taarifa maalum ya PAC iliyowasilishwa kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe na Makamu wake, Deo Filikunjombe, bungeni Novemba 26, mwaka huu.

Taarifa hiyo ya PAC, ilimtaja Chenge kupata mgawo wa Sh. bilioni 1.6 kutoka kwenye fedha zilizochotwa kutoka katika akaunti hiyo.

Wengine waliotajwa na taarifa hiyo ya PAC kupata mgawo kutoka katika fedha hizo, ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka (Sh. bilioni 1.6), Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja (Sh. milioni 40.4) na Mbunge mstaafu wa Sumbawanga Mjini (CCM), Paul Kimiti (Sh. milioni 40.4).

Pia wamo aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona (Sh. milioni 40.4); aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk. Enos Bukuku (Sh. milioni 161.7), Jaji Profesa John Ruhangisa (Sh. milioni 404.25), Jaji Aloysius Mujulizi (Sh. milioni 40.4) pamoja na Mkurugenzi mstaafu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), Philip Saliboko (Sh. milioni 40.4).

Wengine ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Emmanuel Ole Naiko (Sh. milioni 40.4), Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Lucy Appollo (Sh. milioni 80.8); Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Dk. Methodius Kilaini (Sh. milioni 80.9); Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa (Sh. milioni 40.4) na Padri Alphonce Twimannye Simon (Sh. milioni 40.4).

Kutokana na taarifa hiyo ya PAC iliyohusu ukaguzi maalum wa malipo yaliyofanyika katika akaunti hiyo, Novemba 29, mwaka jana, Bunge lilipitisha maazimio nane dhidi ya wote waliohusika na kashfa hiyo.

Ukaguzi huo ulifanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Taarifa hiyo ya PAC, ilieleza kuwa mmiliki wa kampuni ya Pan African Power Solutions Ltd (PAP), Harbinder Singh Sethi, mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering & Marketing (VIP), James Rugemalira, walihusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha kufanyika miamala haramu ya fedha katika akaunti hiyo kwenda kwa kampuni hizo.

Wengine waliotajwa na taarifa hiyo ya PAC kuhusika katika kashfa hiyo ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini aliyesimamishwa kazi, Eliakim Maswi na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, aliyejiuzulu.

Prof. Muhongo alitajwa na taarifa hiyo ya PAC kuwa alikuwa dalali kati ya Rugemalira na Sethi kufanikisha uchotwaji wa fedha hizo kutoka katika akaunti hiyo.

Wengine waliotajwa na taarifa hiyo ya PAC kuhusika katika kashfa hiyo, ni pamoja na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema na waliokuwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Hivyo, Bunge likaazimia kuwa Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya ulinzi na usalama viwachukulie hatua stahiki za kisheria kwa mujibu wa sheria za nchi watu wote waliotajwa na taarifa hiyo ya PAC kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya akaunti hiyo na wengine watakaogundulika kuhusika katika vitendo hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya PAC, vitendo vilivyofanywa na watu hao vinaashiria makosa mbalimbali ya jinai, kama vile uzembe, wizi, ubadhirifu, kutakatisha fedha haramu, matumizi mabaya ya madaraka, rushwa na kupokea mali ya wizi.

Tayari Prof. Muhongo na Jaji Werema walikwishajiuzulu nafasi zao serikalini, huku Maswi, ambaye amesimamishwa kazi akiendelea kuchunguzwa.

Pia tayari Prof. Tibaijuka ameshatimuliwa kazi na Rais Kikwete kwa kupokea fedha hizo kupitia akaunti yake binafsi iliyoko benki ya Mkombozi, kinyume cha maadili.

Pia kutokana na kashfa hiyo, Chenge, ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, alijiuzulu nafasi hiyo kutekeleza moja ya maazimio ya Bunge yaliyotaka yeye na waliokuwa wenyeviti wenzake wa kamati za Bunge; Ngeleja (Katiba, Sheria na Utawala) na Victor Mwambalaswa (Nishati na Madini), wavuliwe nyadhifa hizo. Wote walijiuzulu nyadhifa hizo.

Mbali na kujiuzulu, Februari 2, mwaka huu, Baraza la Maadili lilitangaza kuwaita kwa nia ya kuwahoji wabunge hao, akiwamo Prof. Tibaijuka, Ngeleja, Mwambalaswa na Chenge, kutokana na tuhuma za kashfa ya akaunti hiyo zinazowakabili.

Wabunge hao watafika mbele ya Baraza hilo, kuanzia Februari 23, mwaka huu.

Ofisa Habari wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Johanither Barongo, alisema mahojiano hayo yatafanyika kwa wiki tatu na yataongozwa na Jaji mstaafu, Hamisi Msumi na wajumbe wengine wawili, Hilda Gondwe na Celina Wambura.

MIRADI MAENDELEO JIMBONI
Akizungumzia suala la wananchi na miradi ya maendeleo jimboni mwake, Chenge alisema mtaji wa maendeleo ni kila mwananchi kujituma katika kuchangia miradi mbalimbali na kushirikiana na viongozi na serikali kwa manufaa yao.

“Ndugu zangu, ni bora miradi tunayoileta vijijini mwenu mkaitunza ili tuendelee kuwatumikia kwa muda mrefu…na tufanye kazi ya kuilinda miradi hiyo na kuisimamia miradi yote iliyo ndani ya kata hii,” alisema Chenge.

Mbunge huyo alitembelea maabara ya Shule ya Sekondari Sapiwi kuangalia maendeleo ya ujenzi wake baada ya Mfuko wa Jimbo kutoa mabati 300 kwa ajili ya kuezekea maabara.

Shilingi milioni 36 zimetumika kugharimia ujenzi huo, huku wananchi wakichangia Sh. milioni 10 na Sh. milioni 74 zikihitajika.

Awali, Ofisa Mtendaji wa kata ya Sapiwi, Telen Nhandi, alisema zipo changamoto zinazoikabili kata hiyo ikiwamo upotoshaji wa watu katika michango ya kuchangia maabara, ukame na kusababisha mazao mengi kuanza kuathirika.

Alisema hali hiyo imesababisha baadhi ya wananchi kushindwa kuchangia katika miradi ya maendeleo.


NIPASHE

sasa kama yeye anaiba kwa ajili ya wanajimbo lake anashindwa nini kuchangia hizo 74 mln ziliyobaki kutoka hiyo 1.6 bln kumalizia kujenga maabaara? Huyu mzee ni arrogant wa kutupa!
 
Katika hali iliyoniacha mdomo wazi, kwenye kipindi cha watanzania tuzungumze magazeti cha rfa, imesikika kwenye moja ya magazeti Mh. Vijisenti Bwana Endrew Chenge akisisitiza kwamba yeye co mwizi au fisadi kama wengi tunavomwita bali yeye ni nyoka mjanja mwenye makengeza mtafuta pesa, amejitetea kwamba yy anajitahd kutafuta pesa kwa ajili ya wananchi wa bariadi west, tukumbuke pia huyu ktk harakati za chama chake kujivua gamba alishawahi kusema yeye gamba lake limekwamia kiunoni mwenye shoka aende akalimalzie, lakin pia tusisahau kwamba huyu ndie alikua mwenyekiti kamati ya uandishi katiba pendekezwa ambayo inapgiwa chepuo na serikali ya CCM, nakusihi kasome ibr ya 29 ibr ndg 2b, then unganisha na hz kauli za mh.joka vijisent, then ng'amua mwenyewe kupga kura aidha ya hapana au ndio kwa katiba ya Joka Makengeza Msakapesa.. Tafuteni hlo gazeti mimi nipo kijijn mda huu

watu wegine munasumbuka tu hapo mimi naona hautafa nikiwa nakuomba hoja nyingine. nzokamahenge wewe edelea na mipango yako yakuijega bàriadi sisi tunasema tuko na wewe.
 
Mjinga tu huyu naye,, yaani unaiba hela za umma halafu unajiita mjanja?? Hizo anazoiba ni hela za shangazi zake, bibi zake, mademu zake na za kwake mwenyewe halafu anajiona mjanja,,, hawaoni akina bakhresa, dewji, rostum, nassoro wa superdoll na wengine,, yeye kama mjanja angekuwa mtaani huku halafu akawa anamiliki hizo hela... Unaiba hela za umma/wananchi ambao wamekupa zamana halafu unajiita mjanja?? We ni pumbavu tu na boya fulani hivi... Wajanja wako mtaani huku wanatafuta za halali na si za kuibia wananchi!!!
 
haya sasa kaweka mambo wazi,wale watetezin wake wake tena wamtetee,huyu mzee noma Sana ,ni jizi LA kimataifa.
akiona tu sehemu pamezuubaa anapiga alafu anakaa kando
Mke wake ndio usiseme kwenye kampeni huwa yuko front line,tena Ana jeshi lake LA vijana wake,wanaogopeka bariadi nzima,akisema maliza huyo ,vijana wan an us hug bulimia ipasavyo.
baba anapiga deal kupitia taaluma take,mama yeye anaongoza kikosi cha arthini,wacha kabisa.
 
Mjinga tu huyu naye,, yaani unaiba hela za umma halafu unajiita mjanja?? Hizo anazoiba ni hela za shangazi zake, bibi zake, mademu zake na za kwake mwenyewe halafu anajiona mjanja,,, hawaoni akina bakhresa, dewji, rostum, nassoro wa superdoll na wengine,, yeye kama mjanja angekuwa mtaani huku halafu akawa anamiliki hizo hela... Unaiba hela za umma/wananchi ambao wamekupa zamana halafu unajiita mjanja?? We ni pumbavu tu na boya fulani hivi... Wajanja wako mtaani huku wanatafuta za halali na si za kuibia wananchi!!!

kwa hii kauli ya change ingekuwa nchi ambazo zinafuata maadili yaani jamaa sasa hivi angekuwa anahojiwa na mpelelezi mkuu wa taifa hili,
from there wangemzuia korokoroni ili uchunguzibqa kina ufanyike.
yaani jizi linaiba pesa za umma Leo,kesho rais anasema pesa sio za umma,kesho kutwa jizi linajitojeza na kusema yeye ni mwizi ,tena lenye kengeza alafu watu wanashangilia.hata viombo vya usalama vinamtii Kama Nabii wa majizi
bungeni mama wa watu kampa cheo cha kamati ya budget kwa sababu anajua kucheza na loose money .Hii ndio bongo bana.
 
Endelea kutoa mapovu na kulalama ka malaya alokosa bia ila ukweli ni kuwa wakati kutwa nzima uko jf unapiga soga ka sho.ga mwanaume mwenzio yuko anasaka noti kupitia taaluma yake ya sheria. Kwa mwendo huu jiandae kugongewa wife au we kuliwa tigo.

Mkuu punguza ukali kidogo,,, tatizo hapa sio kutafuta hela kwa kutumia taaluma,, tatizo ni hela ambazo zinatokana na wizi wa mali ya umma/wananchi,, ulishasikia kuna mtu anamlalamikia bakhressa au dewji kuwa ni wezi??? Au ulishasikia dk gharib bilal,dk shein wanalalamikiwa kuwa ni wezi??? Taaluma kila mtu anayo na inamsaidia kujipatia riziki na sio kuitumia taalum yako kuibia au kudhulumu watu.. ukizingatia huyu chenge anatumikia umma ambao umempa dhamana,, hili si suala la kulichekea hata kidogo maana kila aliyepewa dhamana akifanya hivyo tutakuwa wapi kama taifa?? Angeutumia uanasheria wake kama wengine akina prof safari, tundu lissu nk
huwezi kujiita mjanja kwa kuibia watu wako waliokupa dhamana na wewe ukiwa raia wa nchi husika ni sawa na kujiibia mwenyewe na kuibia familia yako....
 
Yaah ndo mfano wa mwanaume mtaftaji... sio kushinda jf kupiga kelele na kulalamika kama mwanamke kutwa nzima. Acheni wanaume watafte pesa, kama mmechagua kushinda kwenye keyboard kutwa nzima, mnalalamikia nini wanaume wenzenu wasaka pesa? Dunia hii nani asiyetaka pesa za kumhakikishia maisha ya kesho.

PASCO (alisema tanzania ni shamba la bibi.)

Utukome wewe wanawake wanapiga kelele gani s
Tena ushindwe na ulegee kiunoni kwenda chini alaaa
 
Wala haitii hasira tena.
Huyu jamaa apewe tu uraisi.
Maybe anaweza kwenda next level na kuibia nchi zingine na kuleta TZ.
 
yeye ndio ATM ya chama nani wa kumfukuza?
 
Kuna wakati ni rahisi sana kuidanganya nafsi sababu hakuna tofauti inayoonekana kwa matendo tunayofanya....Anayedhani amesimama aangalie asianguke tu. Itakuwa aibu sana
 
Back
Top Bottom