Chenge matatani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chenge matatani

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by sulphadoxine, Jun 24, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  KIKOSI cha wabunge kikiongozwa na Naibu Spika, Job Ndugai, kimesafiri kwenda jijini London, Uingereza, kukutana na Bunge la makabwela la nchi hiyo, ili kuongeza ushawishi na hatimaye mabilioni ya fedha yanayopaswa kurejeshwa nchini kutokana na ununuzi wa kitapeli wa rada, yarejeshwe serikalini.

  Sakata hiyo ya rada ilimlazimu waziri wa zamani wa miundombinu, Andrew Chenge, kujiuzulu nafasi yake serikalini baada ya makachero wa Uingereza kukuta zaidi ya dola milioni 1 (bilioni 1.6) kwenye moja ya akaunti za nje za mwanasiasa huyo.

  Makachero hao walizihusisha pesa hizo na tuhuma za rushwa ya rada huku Chenge mwenyewe akijitapa kuwa pesa hizo ni “vijisenti tu” kwake.

  Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mjini hapa, kikosi kinachoundwa na wabunge wengine takriban wanne, kitakutana na viongozi mbalimbali wa Bunge la Uingereza, ambako ndiko mzozo wa mauzo ya rada ya kijeshi ulikoanzia ukiwa na aliyekuwa Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataita wa Uingereza, Clare Short.
   
 2. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Natumaini watakutana na Clare Short pia. Nakumbuka alikuja Tanzania na akakutana na Mkapa Dodoma ambako alimweleza kinagaubaga kwamba mpango wa kununua rada haukuwa na faida kwa nchi hii maskini kwa wakati ule. Ningekua mshauri wa bunge ningemwambia Ndugai na wenzie ni aibu kujaribu kuwaambia waingereza waipe serikali hizo hela wakati bado hatujawachukulia hatua wahusika katika kashfa hiyo. Hivi jamani huu kweli ni ujinga au ni kitu gani hiki kinacho endelea?
   
 3. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Sijaona huo Utata uliompata Chenge
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  nalifikiri ni mimi tu nimepigwa na upofu wa kupambanua, kumbe siv yo. sijaona mahala ambapo chenge anaelekea kuingizwa matatani
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  nadhani kiswahili yake haijanyoroka.anaongelea matata yaliyopita.kaka siku hizi anapeta,anamalizia kutafuna vijisenti vyake kwa mrija!
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hakutakua na jipya.....ni kama yale ya richmond
   
 7. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Mzee Mwanakijiji, wapelekee hao wabunge wa uingereza barua rejea uliyowaandikia wakati ule..
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Jun 24, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Hakuna Matata!

  What a wonderful phrase

  Hakuna Matata!

  Ain't no passing craze

  It means no worries for the rest of your days

  It's our problem-free philosophy

  Hakuna Matata!

  Hakuna Matata?

  Yeah. It's our motto!

  What's a motto?

  Nothing. What's a-motto with you?

  Those two words will solve all your problems

  That's right. Take Pumbaa here
  Why, when he was a young warthog...

  When I was a young wart hog

  Very nice

  Thanks

  He found his aroma lacked a certain appeal
  He could clear the savannah after every meal

  I'm a sensitive soul though I seem thick-skinned
  And it hurt that my friends never stood downwind
  And oh, the shame
  He was ashamed
  Thought of changin' my name
  What's in a name?
  And I got downhearted
  How did ya feel?
  Everytime that I...

  Hey! Pumbaa! Not in front of the kids!

  Oh. Sorry

  Hakuna Matata! What a wonderful phrase
  Hakuna Matata! Ain't no passing craze

  It means no worries for the rest of your days

  It's our problem-free philosophy
  Hakuna Matata!
  Hakuna Matata! Hakuna matata!
  Hakuna Matata! Hakuna matata!
  Hakuna Matata! Hakuna matata!
  Hakuna Matata! Hakuna--

  It means no worries for the rest of your days

  It's our problem-free philosophy
  Hakuna Matata! (Repeats)

  I say "Hakuna"

  I say "Matata"


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Thread zinazowekwa jukwaa hili huwa ni nzito sana lakini hii nadhani haistahili kuwekwa humu.
   
 10. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Bora wewe pia umeona hili.
   
 11. P

  PascalFlx Member

  #11
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hivi hizo fedha walizifanyeje ameachiwa?, je ameszitolea justification amezipataje au ndo yamekwisha?
   
 12. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 524
  Trophy Points: 280
  Mi nashindwa kuelewa, hao waliohusika na kasha ya rada wana kinga gani, maana hata serikali inaogopa kuwafungulia mashtaka. Kama mbayuwayu wa kikwere yumo kwenye hilo saga si ajiuzulu tu, ili sheria ichukue mkondo wake?
   
 13. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hee! Kwahyo utata kwake ni kukutana na wabunge wa uingereza au? Haisomeki.
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Title haijatulia..
   
 15. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ms anamajibu yote tena kwa ufasaha...
   
 16. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  tuiombee nchi yetu ya amani jamni tuendeleee hivi hivi kudumu na amani na ujimya.tuwaombee walioenda waanikiwe kilichowapeleka hukoooo.amen
   
 17. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
 18. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #18
  Dec 10, 2016
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,546
  Likes Received: 1,599
  Trophy Points: 280
  majibu hakuna, sakata limekwisha kama lile la richmond, eskrow, lugumi, shivacom....
   
Loading...