Chenge ashikiliwa polisi kwa ajali ya gari iliyosababisha vifo

21/02/2009 THE INDIAN OCEAN NEWSLETTER n°1256
POLITICS & POWER/BEHIND CLOSED DOORS

Dar es Salaam
Barclays Bank may have decided to close the account of former Attorney General Andrew Chenge who is implicated in a scandal around the sale by British Aerospace of a radar system to Tanzania last year. (...) [57 words] [€1,3]


Mzee huyu ni fataki mkuu kwani vijisenti vinamsumbua
 
Kuhusu insurance inasemekana ilikuwa re-newed isipokuwa tu sticker haikubandikwa.

Gazeti la Kulikoni leo limeandika kuwa kulikuwapo watu wawili waliosikia kishindo na kufika sehemu ya ajali sekunde chache baada ya tukio. Mmoja wa hawa iddi Matuki ambaye ni mlinzi kutoka eneo hilo alisema (haikutajwa alikuwa amamwambia nani) kwamba alikuta Bajaj imegongwa vibaya, maiti moja ikiwa barabarani na nyingine -- iliyokuwa bado hai -- imelaliwa na bajaj, na "....gari ya Chenge lilikuwa limesimamia hatua chache kutoka eneo la tukio na mwenyewe akiwa ndani ya gari akiwasiliana na polisi ambao walifika baada ya ya dakika 45."

Alijuaje kwamba ni Chenge ndiyo alikuwa ndani ya gari (iliyogonga) na pia alijuaje alikuwa anawasiliana na polisi?

Hata hivyo huyu shuhuda Matuki inaonekana anaondoa ile theory ya kwamba huenda Chenge aligonga wafu. Amepangwa?

Lakini bado nina wasiwasi mkubwa -- hasa kwa nini dereva wa Bajaj hajapatikana hadi sasa, au mmiliki wake! Hivi kweli bajaj hii haijulikani kabisa, kwa mfano wapi huwa inapaki jijini hapa? Pakijulikana hapo, si inakuwa rahisi kuulizia wenzake kuhusu hiyo bajaj na nani huiendesha? Na huyo mmiliki, hivi kweli hakuna anayemfahamu kabisa, pamoja na kwamba anamiliki bajaj? Kwa tafsiri yoyote ile ni utata mkubwa!

Isitoshe, hivi hawa marehemu hakuna watu/marafiki etc waliokuwa nao kwenye sehemu ya starehe etc usiku ule kabla ya kukutwa na ajali? Bila shaka watu hawa wasingesita kamwe kujitokeza na kusema "hawa tulikuwa
nao sehemu fulanui..... hadi saa fulani...., na baadaye walituaga na kuondoka na Bajaj etc etc etc!

Inavoonekana hii bajaj na abiria wake ni kama vile waliteremka tu kutoka juu na kugongwa na Chenge!
 
Ah Zak umenifanya nicheke japo nina machungu ati waliteremka kutoka juu na kugongwa na chenge!

Kwa jinsi nyama na damu zilivyotapakaa kwenye gari ya mheshimiwa je eneo la tukio kuna nyama na damu ya binadamu au imeoshwa na mvua?
 
5.JPG
Anaingia na nguo za mjini.

6.JPG

Kaenda kubadilisha anarudi na nguo za shamba.

1.JPG

Mengine mepya hata mwanangu kachanganyikiwa ,sijui kama hapa nitavuka.Naiona jela hiyooo !
 
Toto lake linalipa sema itakuwa aibu kuwa na baba mkwe fisadi tena wa visenti...unaweza kukuta mzee mzima unakuwa Bushoke lohhh!
 
Gazeti la Kulikoni leo limeandika kuwa kulikuwapo watu wawili waliosikia kishindo na kufika sehemu ya ajali sekunde chache baada ya tukio. Mmoja wa hawa iddi Matuki ambaye ni mlinzi kutoka eneo hilo alisema (haikutajwa alikuwa amamwambia nani) kwamba alikuta Bajaj imegongwa vibaya, maiti moja ikiwa barabarani na nyingine -- iliyokuwa bado hai -- imelaliwa na bajaj, na "....gari ya Chenge lilikuwa limesimamia hatua chache kutoka eneo la tukio na mwenyewe akiwa ndani ya gari akiwasiliana na polisi ambao walifika baada ya ya dakika 45."

Hivi kweli tukoje? Mtu amegonga. Badala ya kuhangaika kuokoa maisha ya majeruhi tunakimbilia kujilinda? Juhudi gani zilifanywa kujaribu kuwaokoa waliopata ajali? Ati polisi walikuja baada ya dakika 45! Dakika 45 ambapo mtu anapoteza damu. Pengine simple first aid ingeweza kuwaokoa. Hivi lini tutaanza kuona roho za binadamu wenzetu zina thamani?

Amandla..........
 
Last edited:
Vicky wa ajali ya Chenge azikwa kama Halima

Na Frederick Katulanda, Mwanza

VICTORIA George, mwanamke aliyefariki katika ajali iliyomuhusisha waziri na mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, Andrew Chenge alizikwa juzi mjini hapa, huku jina la Halima likitumiwa katika taratibu zote.


Vicky na mwenzake, Beatrice Constatine walifariki papo hapo baada ya pikipiki ya matairi matatu waliyokuwa wamepanda kugongana na gari aina ya Toyota Hilux iliyokuwa ikiendeshwa na Chenge katika makutano ya Barabara ya Haile Silasie na Karume. Mwili wa Beatrice uliwasili jijini hapa jana kwa ndege ya shiria la Precision tayari kwa mazishi.


Vicky alizikwa Jumatatu majira ya saa 10:00 kwenye makaburi ya Lumala wilayani Ilemela kwa taratibu zote za dini ya Kiislamu. Mwili wake uliwasili saa 5:00 asubuhi ukitokea Dar es salaam.


Habari kutoka kwa ndugu zake zinaeleza kuwa muhudumu huyo wa zamani wa Hoteli ya Mwanza alipachikwa jina hilo baada ya kuigiza tamthiliya akitumia jina la Vicky.


"Baada ya hapo alijulikana kama Vicky na hata alipoajiriwa Hoteli ya Mwanza alitumia jina la Vicky kwa sababu alibadili dini baada ya kuzaa na Mkristo anayeitwa Innocent," alisema mmoja wa ndugu zake.


"Lakini hapa mwishoni alionekana kurudia kwenye dini yake ya Kiislamu na ndio maana amezikwa kwa taratibu zote za Kiislamu."


Vicky amekuwa gumzo katika ajali hiyo baada ya mama yake kudai kuwa Chenge alikuwa akifahamiana vizuri na mwanamke huyo, kiasi kwamba wakati ambao Vicky, ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye casino ya hoteli hiyo, hakwenda kazini, mheshimiwa huyo alimpigia simu ili aende kumuhudumia.


Chenge amekiri kumfahamu Vicky, lakini amekana kuwa na mahusiano yoyote na msichana huyo.


Awali, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa Vicky na Beatrice walikuwa wakielekea Zanzibar ambako msichana huyo angefunga ndoa, lakini mama yake alikanusha madai hayo akisema kuwa alishaenda visiwani humo na kwamba angerejea Mwanza asubuhi ya siku ambayo alifariki.


Habari zaidi kutoka kwa baadhi ndugu wa karibu wa Vicky zinaeleza kuwa Chenge amegharamikia usafiri wa ndege kwa mwili wa marehemu wote wawili.


Katika kuchangia gharama hizo za safari Chenge amegharamikia gharama za kusafirisha mwili pamoja na tiketi mbili za ndege kwa ndugu wawili walioambatana na mwili wa marehemu kutoka Dar es salaam kuja Mwanza, lakini kwa upande wa mwili wa Beatrece pia amegharamikia tiketi tatu za basi kwa ajili ya ndugu wengine kuja Mwanza kwa mazishi.


Kaka wa Marehemu alipoulizwa alikataa kutoa maelezo yoyote kuthibitisha ama kukubali na kusema mengine ni masuala ya familia.


Katika hatua nyingine, mwili wa Beatrice unatarajiwa kuzikwa leo saa 9:00 alasiri.


Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa marehemu kaka wa marehemu na msemaji waamilia Andrew Constantine alisema mara baada ya kuwasili mwili huo waliamua kuufikishia nyumbani moja kwa moja kungoja maziko.


Alisema baada ya kuwasili kwa mwili huo ndugu na jamaa wamekubaliana kuwa maziko yatakuwa leo ili kutoa nafasi ya wanafamilia wengine na ndugu wengine kuwasili jijini Mwanza

Source: Mwananchi
 
Uta define vipi kuendesha gari kizembe?

Mimi nilifikiri wataweka pia kuendesha gari kwa speed kubwa (80km/h) kinyume na barabara husika?

Mzee wa Visenti atashinda hii case au kuambiwa alipe fidia.

Ila dunia hii matatizo yakikuanza hayatoki kirahisi.

Swadakta! Hii ni sawa na kula nyama ya Binadamu.

Bwana Andrea ana kazi ngumu mno na asidhani hata kama itaisha kwa kuonekana hana hatia au akiamriwa alipe faini itamsaidia sana.

Mimi najua kama binadamu lazima kuna kitu kitazidi kumkereketa moyoni. Kwani haiwezekani mazingira ya ajali ile na mtiririko wa matukio yaliyojitikeza mpaka 'kujileta kwake mahakamani' hii ni sinema.

Chenge mrudie mola wako ndugu yangu dunia hii ina mwisho kaka na damu ina thamani sana.

Lakini Jamani Mungu kweli ana Shani yake...huyu bwana alisemwa sana kwenye mambo ya kesi zile za ufisadi na kutumia madaraka yake vibaya pamoja na kukutwa na vile tujisenti. Leo katokea kwengine....the worst traffic offence iliyopelekea kuua.

duh! ama kweli'Kabla hujafa hujaumbika
 
"......Bwana Andrea ana kazi ngumu mno na asidhani hata kama itaisha kwa kuonekana hana hatia au akiamriwa alipe faini itamsaidia sana.

Mimi najua kama binadamu lazima kuna kitu kitazidi kumkereketa moyoni. Kwani haiwezekani mazingira ya ajali ile na mtiririko wa matukio yaliyojitikeza mpaka 'kujileta kwake mahakamani' hii ni sinema.

Chenge mrudie mola wako ndugu yangu dunia hii ina mwisho kaka na damu ina thamani sana.

Lakini Jamani Mungu kweli ana Shani yake...huyu bwana alisemwa sana kwenye mambo ya kesi zile za ufisadi na kutumia madaraka yake vibaya pamoja na kukutwa na vile tujisenti. Leo katokea kwengine....the worst traffic offence iliyopelekea kuua.

duh! ama kweli'Kabla hujafa hujaumbika....."


*****************************

Kingwele: Kwa kutubu, naona Bwana Andrea angefanya kitu kimoja: Angetoa zile hela za radar zilizoko ktk akaunti yake kule Jersey na kuwagawia masikini wa nchi hii. Hapo angeeleweka na Bwa Mola angalau angemsamehe.
 
Hivi, hizi Bajaj zina safety features gani? Seatbelts? Airbags? Side impact bars?
Unaweza kuta this particular one kilikuwa hakina hata reflecters. Hata mtu ukiwa sober, usiku unaweza usikione hiki.

Kwanini zinasajiliwa na kuruhusiwa kubeba abiria?

Mabalaa mengine waTZ TUNAJITAKIA WENYEWE!!!!!!!!!!!!

Mkuu,
This is interesting question!Ulishaona bajaj? Kama umewahi kuiona... hebu tuambie hata kama ina safety/seat belts au airbags.. ajali kama hii ya Chenge hivi vitu vingesaidia nini maana hivyo vibajaj vyenyewe ni kama toy tu.. vinaonekana very delicate na hivyo kukiwa na impact inaenda moja kwa moja kwa waliomo ndani.
The only safety measure I see ni kama vitakatazwa kuendeshwa mahali penye magari na sijui itakuwa wapi.
 
Mkuu,
This is interesting question!Ulishaona bajaj? Kama umewahi kuiona... hebu tuambie hata kama ina safety/seat belts au airbags.. ajali kama hii ya Chenge hivi vitu vingesaidia nini maana hivyo vibajaj vyenyewe ni kama toy tu.. vinaonekana very delicate na hivyo kukiwa na impact inaenda moja kwa moja kwa waliomo ndani.
The only safety measure I see ni kama vitakatazwa kuendeshwa mahali penye magari na sijui itakuwa wapi.

Mimi kwakweli mwanzoni mheshimiwa Mwiba aliposema sehemu ya ajali hakuna damu nilifikiri anatania.Lakini sasa naanza kupatwa na wasiwasi ya kwamba hiii ajali ni ya kupangwa.

Japo inawezekana lakini duuuuu.
Kwanza wasichana wametoka mbali harafu aliyewagonga anawafahamu ,pili bongo hatuna vitaburisho na dereva wa bajaj alilala mbele lakini wakati huo huo majina na sehemu wanapotoka hao mabinti yalifahamika papohapo.

Unless Chenge alikuwa nao sehemu na alikuwa anawafuatilia kwa nyuma ama walikuwa wanaelekea nyumbani ,lakini tofauti na hapo duuuu hii itakuwa kwa kiasi kikubwa ni ya kupanga.
 
Wanasheria wa Bongo wanatia huruma walivyomsomea shitaka Chenge.

Chenge, kosa la kwanza unashitakiwa kwa kuendesha kizembe na kusababisha.......kweli, si kweli?
Mimi ningejibu: Kweli, nashitakiwa!

Kuhani,
Nadhani Kiswahili hakijaweza ku catch up na kiingereza...
Hii "kweli si kweli" ndo plea taking -- yaani " guilty or not guilty"
Bado ungejibu " guilty?" unajua ambacho kingefuatia ni kusomewa facts of the case na baadae sentence ...jela.Sidhani Chenge anataka kwenda jela upesi hivyo!
 
5.JPG
Anaingia na nguo za mjini.

6.JPG

Kaenda kubadilisha anarudi na nguo za shamba.

1.JPG



INAONEKANA CHENGE ALIMUAMBIA USINITIE AIBU NA VISURUALI VYAKO (INAONEKA MZEE MKOLONI SANA).

kusema ukweli mtoto wake mzuri, alafu amependeza na hiyo suruali MASHALAHHHHH

embu fikiria umetoka nae disco alafu umeshusha kwao, kabla hajaingia getini anakukiss alafu ana kuambia bye bye, ukiwa unataka kuingia ndani ya taxi mliyokuja nayo anatokea vijisenti, anakuuliza mungwana umetoka wapi na binti yangu, lo......
 
Huyu ndiyo mrembo hapo juu ''' WHY IT HAS TO BE IMMA ONLY HATA MTOTO WA MKULU NAYE IMMA....

Madina Chenge




Legal Officer
Not yet admitted.

Practise Areas:

Litigation & Commercial Law.

Brief biography:

Born in Dar Es Salaam on March 31,1984.

Education:

LL.B, University of West Minister - London
MA, Regent Business School - London

Work experience :

Intern/Legal Officer at IMMMA, 2007 - 2009; Legal Officer at IMMMA, 2009 to date.

Member: none at the moment

Languages: English and Swahili.

Email: chenge@immma.co.tz
 
Huyu ndiyo mrembo hapo juu ''' WHY IT HAS TO BE IMMA ONLY HATA MTOTO WA MKULU NAYE IMMA....

Madina Chenge




Legal Officer
Not yet admitted.

Practise Areas:

Litigation & Commercial Law.

Brief biography:

Born in Dar Es Salaam on March 31,1984.

Education:

LL.B, University of West Minister - London
MA, Regent Business School - London

Work experience :

Intern/Legal Officer at IMMMA, 2007 - 2009; Legal Officer at IMMMA, 2009 to date.

Member: none at the moment

Languages: English and Swahili.

Email: chenge@immma.co.tz

wazungu wanasema nikune mgongo wangu na mimi nitakukuna wa kwako....
masha kwa mwajiri ridhiwani na kikwete kamuajiri masha..

wanasheria ni watu corrupt sana duniani, na kesi zingine zinahitaji kujuana ili kushinda

lakini hafadhali kampeleka binti yake shule, maana yake mitoto mingine hayendi shule na wakati baba zao wana hela za kuwalipia
 
Mkuu Mtu Kwao, hapa tunafikiri pamoja, ni utata mtupu. Wajuana na sio wanafahamiana kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, ikapotoshwa walikuwa wakienda Zanzibar mmoja kufunga ndoa kumbe walishatoka huko na walikuwepo hapo dar, wamegongwa saa kumi usiku na mtu anayejuana na mmoja wao, bajaji imegongwa kwa nyuma kosa ambalo huenda kwa mgongaji moja kwa moja.

Hapana hawa kweli walikuwa wakivinjari pamoja, wakatofautiana, kina dada wakatoka mbio na kuikuta hiyo bajaji, mzee wa vijisenti akawafuata huku amefura na kuwabamiza kwa nyuma, inawezekana sana, tunahitaji kupata wataalamu wa Scotland Yard, hawa wetu wameshaanza kuiharibu kesi, wanaunda tume, muuaji anasindikizwa kama mfalme, anaelekeza!
 
Back
Top Bottom