Chenge ashikiliwa polisi kwa ajali ya gari iliyosababisha vifo

Sheria zetu nyingi zimechoka hasa. Yaani Chenge na gari yake ni kama vile waligonga ng'ombe wawili kule Bariadi.
 
Anadunda yupo mtaani kapata dhamana na kakana mashitaka yote matatu. Upo hapo?
Siku zote unatakiwa ukane ,hivyo kama huna habari basi hiyo ndivyo ilivyo,unatakiwa ukatae mashtaka , si unaona wahalifu wote wanakataa makosa yao ,maana katika kukataa wale wanaokushitaki wakizubaa tu umetoka na kurudi uraiani ,sasa hapa katika kesi hii ili kupindishwa pindishwa ushahidi itabidi utolewe kiaina , na kama chenge tayari ameshanunua vifo vya hao waliokufa basi hapo dau lake si dogo kwa kila kichwa,halafu kama dereva hajapatikana inaweza ikaifanya hii kesi kuwekwa kiporo kwani ushahidi utakuwa hautimii mpaka dereva wa Bajia apatikane.polisi wakisema bajaji iligongwa kwa nyuma wakati kule inaonekana gari ya Chenge imeumia ubavuni ,ushahidi wa polisi utakuwa wa uongo,
 
Page+3.JPG

Jeneza la mwili wa marehemu Beatrece Costantine mwanamke aliyefariki katika ajali iliyomuhusisha waziri na mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, Andrew Chenge ukiwa ndani ya nyumba yake Kiseke wilayani Ilemela Jijini Mwanza mara baada ya kuwasili kutoka Dar es salaam kwa ndege,mwili huo unatarajiwa kuzikwa kesho saa tisa alasiri.Picha kwa Msaada wa Mdau Mpoki Bukuku
----------
Na Frederick Katulanda,Mwanza
VICTORIA George,mwanamke aliyefariki katika ajali iliyomuhusisha waziri na mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, Andrew Chenge alizikwa juzi mjini hapa, huku jina la Halima likitumiwa katika taratibu zote.

Vicky na mwenzake, Beatrice Constatine walifariki papo hapo baada ya pikipiki ya matairi matatu waliyokuwa wamepanda kugongana na gari aina ya Toyota Hilux iliyokuwa ikiendeshwa na Chenge katika makutano ya Barabara ya Haile Silasie na Karume. Mwili wa Beatrice uliwasili jijini hapa jana kwa ndege ya shiria la Precision tayari kwa mazishi.

Vicky alizikwa Jumatatu majira ya saa 10:00 kwenye makaburi ya Lumala wilayani Ilemela kwa taratibu zote za dini ya Kiislamu. Mwili wake uliwasili saa 5:00 asubuhi ukitokea Dar es salaam.
 
"Siku zote unatakiwa ukane ,hivyo kama huna habari basi hiyo ndivyo ilivyo,unatakiwa ukatae mashtaka , si unaona wahalifu wote wanakataa makosa yao ,maana katika kukataa wale wanaokushitaki wakizubaa tu umetoka na kurudi uraiani ,sasa hapa katika kesi hii ili kupindishwa pindishwa ushahidi itabidi utolewe kiaina , na kama chenge tayari ameshanunua vifo vya hao waliokufa basi hapo dau lake si dogo kwa kila kichwa,halafu kama dereva hajapatikana inaweza ikaifanya hii kesi kuwekwa kiporo kwani ushahidi utakuwa hautimii mpaka dereva wa Bajia apatikane.polisi wakisema bajaji iligongwa kwa nyuma wakati kule inaonekana gari ya Chenge imeumia ubavuni ,ushahidi wa polisi utakuwa wa uongo,"

*************************

Mwiba:

Ingawa kesi za trafiki ni minor ilikuwa sawa kwa Andrea kuyakana mashitaka ili kujiweka on the safe side -- hadi pale 'atakapompanga' hakimu. Bila hivyo kuna danger moja -- hakimu anaweza kumnyima option ya fine na kumsweka ndani hata mwezi mmoja -- ili tu kumuabisha fisadi huyu. hadi a-lodge rufaa yake etc tayari atakuwa ameonja joto la jiwe lupango.

Na ninaamini kabisa mahakimu hawa wameji-tune kiunyama unyama kwa mafisadi kama hawa -- ona jinsi wale wa EPA walivyopata shida kuhusu masharti ya dhamana!
 
Last edited by a moderator:
Taarifa kutoka kwenye mazishi ya Beatrice huko Mwanza zinaeleza kuwa kaka wa marehemu aitwaye Cosntantine, amewaeleza waombolezaji kuwa Chenge alikuwa pamoja na marehemu hao maisha Club wakikata kinywaji. Anasema awali, Chenge alimpigia simu dada yake na kumtaka wakutane hapo na dada huyo aliamua kwenda na rafiki yake. kwa mujibu wa maelezo ya Costantine, kulitokea kutoelewana na dada yake na rafiki yake wakaamua kuondoka na kibajaj lakini Chenge aliingia kwenye gari lake na kuanza kuwafukuza.
Kwenye mazishi chenge aliwkilishwa na rafiki yake kipenzi Clementi mabina, ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza. Mabina aliwasilisha rambirambi ya Sh lakini tano kutoka kwa Chenge na kueleza kuwa Change alipanga kuhudhuria mazishi lakini ameshindwa kutokana na kukabiliwa na kesi.
Akiwasilisha salamu za Chenge mabina alisema anaitaka familia kuwa na subira wakati huu na kuacha kusikiliza tetesi za mitaani kuhusiana na ajali hiyo kwani yeye hakukusudia kuwagonga waliokuwa kwenye bajaj
 
Hizo ndizo habari za awali kuwa walikuwa wanafukuzwa na nadhani katika ile michezo ya kijinga ya kuwatishia na kuwapiga mkwara. Kwa gari linalokwenda kwenye mwendo wa 80KM/h nadhani ni mchezo wa kijinga.
 
Kuhani,
Nadhani Kiswahili hakijaweza ku catch up na kiingereza...
Hii "kweli si kweli" ndo plea taking -- yaani " guilty or not guilty"
Bado ungejibu " guilty?" unajua ambacho kingefuatia ni kusomewa facts of the case na baadae sentence ...jela.Sidhani Chenge anataka kwenda jela upesi hivyo!

WomenofSubstanc,

Ni kweli lugha yetu haitoshelezi mahitaji ya mawasiliano ya kitaalam na ndio maana hata sheria zinaandikwa Kiingereza. Lakini hata maneno guilty/not guilty nayo tabu?

Hatuwezi kusoma shitaka kwa Kiswahili sahihi, tutaweza kuandika sheria na hukumu kwa Kiingereza cha watu?

Kuhani, unashtakiwa kwa kosa la kusababisha....kweli, si kweli? KWELI, NASHITAKIWA!

Chenge, unashitakiwa kwa kosa la kusababisha ajali... Je, unakiri kosa, au hukiri?

Chenge, unashitakiwa kwa kosa la kusababisha ajali... Ikirari (plea) yako ni nini, una hatia, au huna hatia?

Chenge, unashitakiwa kwa kosa la kusababisha ajali...Je, unakana shitaka, au hukani?

Kigumu nini hapo?
 
Nimesoma magazeti mengi sana yanayoripoti habari za Chenge na ajali hii yenye utata, sijasoma mahali popote panapoonesha kwamba Chenge amesomewa shitaka la kuendesha gari ambalo bima yake imekwisha muda wake tangu mwaka 2007. Wameonesha makosa ya kugonga na kuua tu. Au kosa hili wameliruka? Au nimesoma vibaya!
Wadau hili nalo limekaaje?
 
Hilo hakushitakiwa nalo ,maana inategemea yule anaekwenda kukushitaki au kukufungulia kesi ,pemgine jamaa hakuzibandika ,sasa ,pengine hilo polisi wameona haliwahusu au halihusiani na vifo au ni jepesi na wako wengi ambao wanaendesha bila ya kuwa na bima ,hapo huwa ndipo wanapopatia mlo wa siku,hivyo wakianza kuwakamata kamata watakosa ulaji lazima mambo mengine uwe unatumia akili ili usije baadae ukapoteza uwekezaji. Hapo inaonyesha polisi wa usalama wamewekeza :D
 
kufuatana na taarifa za magazeti ya leo, inasemekana bima ya 2008 ilonekana ndani ya gari! na ya 2008 -2010 (ya miaka 3) imeonyeshwa kwa polisi ilikatwa NIC. SIJUI SIKU HIZI MTU ANAWEZA KUKATA BIMA YA GARI YA MIAKA MINGAPI NIC. ninavyofahamu bima huwa ni ya mwaka moja moja au chini ya hapo ikitegemea matumizi ya gari.

kwa bingo sio jambo la ajabu kukata bima baada ya kupata ajali.

macinkus
 
"Hizo ndizo habari za awali kuwa walikuwa wanafukuzwa na nadhani katika ile michezo ya kijinga ya kuwatishia na kuwapiga mkwara. Kwa gari linalokwenda kwenye mwendo wa 80KM/h nadhani ni mchezo wa kijinga."
__________________

MKJJ: Pengine haukuwa "mchezo wa kijinga" na ilikuwa ni dhamira ya kumwonyesha huyo dada wa Constantine kwamba Andrea -- bingwa wa radar, Meremeta etc -- siyo mtu wa kukataliwa na "changu doa" kama huyo!

Lakini maelezo ya Mpita Njia yanaleta maswali mapya -- kwamba Andrea hakusema ukweli pale alipotamka kwamba kumfahamu kwake Vicky ni kule Mwanza tu akimhudumia katika Hoteli, na si zaidi ya hapo. Kwa nini alidanganya -- hakusema walikuwa pamoja masaa machache kabla.
 
kufuatana na taarifa za magazeti ya leo, inasemekana bima ya 2008 ilonekana ndani ya gari! na ya 2008 -2010 (ya miaka 3) imeonyeshwa kwa polisi ilikatwa NIC. SIJUI SIKU HIZI MTU ANAWEZA KUKATA BIMA YA GARI YA MIAKA MINGAPI NIC. ninavyofahamu bima huwa ni ya mwaka moja moja au chini ya hapo ikitegemea matumizi ya gari.

kwa bingo sio jambo la ajabu kukata bima baada ya kupata ajali.

macinkus

Nilidhni maajabu yaliisha enzi za mitume, kumbe bado inaendelea!
 
Taarifa kutoka kwenye mazishi ya Beatrice huko Mwanza zinaeleza kuwa kaka wa marehemu aitwaye Cosntantine, amewaeleza waombolezaji kuwa Chenge alikuwa pamoja na marehemu hao maisha Club wakikata kinywaji. Anasema awali, Chenge alimpigia simu dada yake na kumtaka wakutane hapo na dada huyo aliamua kwenda na rafiki yake. kwa mujibu wa maelezo ya Costantine, kulitokea kutoelewana na dada yake na rafiki yake wakaamua kuondoka na kibajaj lakini Chenge aliingia kwenye gari lake na kuanza kuwafukuza.
Kwenye mazishi chenge aliwkilishwa na rafiki yake kipenzi Clementi mabina, ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza. Mabina aliwasilisha rambirambi ya Sh lakini tano kutoka kwa Chenge na kueleza kuwa Change alipanga kuhudhuria mazishi lakini ameshindwa kutokana na kukabiliwa na kesi.
Akiwasilisha salamu za Chenge mabina alisema anaitaka familia kuwa na subira wakati huu na kuacha kusikiliza tetesi za mitaani kuhusiana na ajali hiyo kwani yeye hakukusudia kuwagonga waliokuwa kwenye bajaj

Dada wa Bw, Constantine ni Beatrice Constantine.
Chenge alimpigia simu kumwomba wakutane Maisha Club na dada yake huyo (Beatrice) aliamua kwenda na rafiki yake.

Sasa mbona ni kama Chenge alikuwa karibu sana na huyu Beatrice ambaye siye tuliyeambiwa kuwa anafahamiana na Chenge? au ilikuwaje?
 
Mimi bado ninajiuliza kwa nini hawa mabinti walifariki? Kwa jinsi simu za mkonononi zilivyojaa, kwa nini hakuna aliyetafuta msaada wa hospitali? Bila shaka mtuhumiwa alikuwa na uwezo wa kupigia simu hizo hospitali kama zipo! Kama hazipo, tunafanya nini kuhakikisha kuwa pale panapotokea ajali majeruhi wanapatiwa huduma haraka iwezekanavyo? Hizi idadi za vifo za kutisha kila panapotokea ajali kweli hazitustui? Badala ya kukazania tu kuwakamata wanaosababisha hizo ajali juhudi nazo zifanywe kuhakikisha kuwa maisha ya wenzetu yanaokolewa. Watu wanakufa kwa sababu hakuna anayejua kufunga tourniquet kuzuia damu kupotea? Hao polisi wanapopata taarifa ya ajali, je wanawasiliana na hospitali ili watume watu wa huduma ya kwanza? Kama tunashindwa kabisa basi kwa nini hao mapolisi wa traffic wasiongezewe basic training ya first aid? Hii biashara ya kwamba ajali maana yake kifo ni lazima itafutiwe ufumbuzi.

Amandla..........
 
WomenofSubstanc,

Ni kweli lugha yetu haitoshelezi mahitaji ya mawasiliano ya kitaalam na ndio maana hata sheria zinaandikwa Kiingereza. Lakini hata maneno guilty/not guilty nayo tabu?

Hatuwezi kusoma shitaka kwa Kiswahili sahihi, tutaweza kuandika sheria na hukumu kwa Kiingereza cha watu?

Kuhani, unashtakiwa kwa kosa la kusababisha....kweli, si kweli? KWELI, NASHITAKIWA!

Chenge, unashitakiwa kwa kosa la kusababisha ajali... Je, unakiri kosa, au hukiri?

Chenge, unashitakiwa kwa kosa la kusababisha ajali... Ikirari (plea) yako ni nini, una hatia, au huna hatia?

Chenge, unashitakiwa kwa kosa la kusababisha ajali...Je, unakana shitaka, au hukani?

Kigumu nini hapo?

Kuhani,
We acha tu Tanzania zaidi ya uijuavyo!
 
Back
Top Bottom