Chenai upo wapi my love?

Chenai upo wapi my love?

Episode 8,

Nipo na sued homeboy wangu niliyekuwa naishi nae India vasant Bihar..
Tunakutana baada ya miaka 16 kupita tangu nirudi toka India.

Nikamuuliza sued habari za watu niliowaacha nyuma yangu kule India..

Sued akapiga ile juice fundo la nguvu halafu akanambiya ni long story mwandende...

kwanza akaanza na habari zake,, kwamba ametoka south,, alifata biashara fulani,,lakini kuna watanzania wenzetu walimdhulumu pesa zake zote,,

Hata kufika kukosa hata nauli ya kumfikisha Tanzania.

Ilibidi aweke rehani laptop mbovu ili iwe Kama dhamana ya kumfikissha Tanzania,

Kufika Lusaka nadhani yule kondactor aliishtukia ile laptop mbovu,,

Ikabidi alazimishe kupewa nauli.
Sued alishukuru sana kwa jinsi nilivyomsaidia nauli..

Mwandende,,

Aliniita,,akanambiya ulipoondoka India na mm haikupita mwaka mmoja nikarudi zangu Tanzania.

Siku moja alipiga simu msichana mmoja akajitambulisha anaitwa chenai,

Akajitambulisha ni girlfriend wako,,

tukamwambiya mwandende kasafiri yupo Tanzania.

Duu nikamwambiya mlishaharibu kila kitu,,

Akasema alilazimisha apajuwe nyumbani ili apate uhakika zaidi kama ni kwl umesafiri.

Siku amekuja chenai ,,na kugunduwa kama upo Tanzania,

Chenai alipiga kelele za kilio hata kukaribia kujaza wahindi pale ndani.

Nilijisikia vibaya sana kumwacha chenai katika hali ile.

Nikauliza kuhusu hamidu,,

akasema hamidu alipata ajali mbaya ya gari akafa papo hapo..

Nikakumbuka utabiri wa rajesh kwamba hamidu kivuli alikuwa hakioni na ataishia hapo India.

Nikauliza kuhusu Saidi,, akanambiya nae yupo jela kafungwa miaka mingi ,,

aligombana na mnigeria mmoja ikafikia kumchoma kisu yule jamaa na kufa papo hapo.

Pia nikakumbuka utabiri wa rajesh,,

alisema saidi atapata matatizo
makubwa sn India.

Kwakweli nilijisikia vibaya sana kusikia habari zile.

Nikatoa noti ya $ 100 ,,2 nikampa sued,,
tukaingia tena kwenye bus safari Tanzania..

Hii ni true story ya maisha yangu ya kutafuta inchini India.

Mwisho.
Nipo hapa mwanangu mwandende
 
Episode 1.

Bado naikumbuka siku ya kwanza kufika India,,
Moyo wangu ulikuwa na hofu na wasiwasi na huko niendako.

Naikumbuka siku niliyoishiwa pesa za matumizi na kunifanya niwe street boy katika jiji la new delh.

Miaka 21 toka sasa,,lakini naikumbuka kila mtaa na eneo lote la new delh,,
kuanzia Karol Bagh,palika bazaar,pahar ganj ,,vasant vihar ,conut place.nk.

Bado naikumbuka sura nzuri sana ya mrembo chenai my love.

Where are you?


Hapa dar nilikuwa naishi mitaa fulani ya down town,,

Kipindi hicho watu wakitoka majuu,,basi wanatutia hamasa na tamaa ya kufika ng' ambo.
Yupo brother mmoja wa mtaani,,ilikuwa akirudi yupo powa sana,,
Kuanzia pamba ,,pesa kibao,,mademu kumgombania ni kawaida sana,

Kipindi hicho nina umri wa kama 20 hivi..
Basi niliamua kuzichanga pesa ,,mwishowe na Mimi mwandende nikawa kwenye emirates nakwea pipa ,,

Safari yangu ilianzia Nairobi,,kupitia Dubai,,then sahara international airport Mumbai..

Nakumbuka nilikuwa na jamaa zangu watanzania 3 ambao ndy walikuwa wanaongoza safari nzima.

Hawa jamaa nilikutana nao Nairobi ktk mipango ya kutafuta viza ya India.

Maana kipindi hicho hapa bongo hakukuwa na mambo mengi ya wajanja wa kutoa viza.

Ilikuwa kila kitu basi lazima upite Nairobi.


Mimi nilikuwa bado mdogo sana,,wala sina ndugu huko,,wala jamaa zaidi ya watanzania wenzangu wanaoishi huko ambao siwajuwi.

Tulifika Mumbai asubuhi salama,
pale tukakutana na watanzania wachache,,
Usiku tukapanda train tukaenda new delh ambapo ndy niliishi kwa dhiki na shida hadi kukutana na mtoto wa kishua chenai..

Itaendelea ,,
Khumbu?
 
Daahh huu Uzi kumbe ulihamishiwa huku mode hawajatutendea haki kabisa yaani


Nilikuwa natafuta Sana .. mkuu Hilo jina la chenai linamaana gani nimelipenda Sana Lina sound poa Kama linaasili ya asia hivi
 
Episode 6.

Tupo palika bazaar ,,,tupo kwenye utabiri wa rajesh,,
Mdosi kutoka Tamil akitubashiria hatma ya maisha yetu pale India.

Basi baada ya Mimi kutabiriwa mafanikio,,

Ikafika zamu ya sued,,nae akachanga karata kama kawaida,,
Akaziweka chini ,,kasuku akachaguwa moja akampa rajesh mtabiri,

Hapo rajesh akamuangalia sued halafu akashika mkono wake wa kulia akamwambiya na wewe utakwenda nyumbani tena soon.
Utapata mafanikio..

Hamidu nae akachukuwa karata,, akazichanga,,akaziweka chini.

Kasuku akachukuwa moja akampa rajesh mtabiri,,akaiangalia ile karata,,

Akamshika mkono hamidu halafu ghafla akauachia kwa nguvu sana.
Kama ameunguzwa na kitu..

Ni Kama vile afanyavyo mtu aliyeunguzwa na kitu.
Akasema ni kama vile sikuoni,,ila hakuna tatizo..
Ila hutofika nyumbani,, utaishia hapa hapa India.
Basi tukacheka,,kimasihara kama kumdhihaki rajesh mtabiri..

Ikaja zamu ya saidi nae akachanga karata,,halafu akaziweka chini,,tena kasuku akachukuwa moja
Akampa rajesh mtabiri.

Akamshika mkono saidi,, rajesh akasema wewe utapata matatizo makubwa sana hapa India..

Duu!! Ulikuwa ni utabiri fikirishi sana,,

lakini tuliupuuzia kama upuuzi
mwingine,
Tulifikiria pengine ni mambo ya kiongo kama wafanyavyo watabiri wengine matapeli

Mungu mkubwa nilipata passport yangu kutoka kwa police,, na mambo yangu yalirejea kama kawaida kufanya mishenishe za biashara..

Ikawa chenai tunawasiliana kwa usiku tu,,au week end moja moja nakutana nae sehem,,

Maana ni kipindi sasa mama yake amesharejea toka Zimbabwe.yupo hapo new delh.

Kwahyo muda mwingi nilikuwa busy,,

hivyo ilimfanya chenai kuchanganyikiwa zaidi na mwandende boy.

Ikawa simu mfululizo hadi kero,,Kama unavyojuwa simu tulikuwa tunashare na Mwenye nyumba,,

Kwa hyo muda mwingi yeye akipiga simu huwa wanapokea huko,,sisi yunakuwa town.

Phone calling!!!!!
Chenai

Hello,,

.sorry

Can I speak to mwandende plz?


"No no,,baadme mwandende abi neihe "

Abi school jaega"

Akimaanisha now mwandende hayupo amekwenda shule.

Basi simu kila wakati hata sometimes tunaongea habari zetu za mapenzi ktk simu bila kujuwa kumbe yupo Binti mmoja wa Mwenye nyumba anaitwa sapna anafuatilia maongezi yetu.

Ilitokea siku moja natoka ndani napita pale kwa Mwenye nyumba kuna jambo fulani la kumwambiya.

Nikakutana na Binti mmoja kama 20 hivi,,,nilikuja kujuwa baadae jina lake anaitwa sapna.

Ambaye ni mtoto yule mama,,nikamsalimia,,akajibu kwa aibu sana.

Then nikamuuliza yule mama akawa hayupo.
Nikamwambiya nitakuja baadae.

Yule binti akanambiya.
You must be mwandende.

Nikajibu

Yes,,iam the one.

Akanambiya ..

Your voice is so family to me.

Nikashangaa sana,,

I used to hear you on the phone with your girl friend talking.

I wish to see her one day..

She is so luck to have you.

Duu..
Nilitetemeka kwa hofu jinsi huyu binti alivyonitamkia,,

Halafu sikuwahi kumdhania chochote,,
Kumbe huyu Binti anatusikiliza maongezi yetu?

Halafu inaonyesha amependa sana sound yangu through phone.
Hii ni hatari sana hii.

Ghafla akaingiia muhindi mmoja Mzee wa makamo kiasi,, ambaye tunakaa wote flat moja,,
Ni Jirani yetu.

Basi alituangalia Jicho Kali sana hata nikahisi kuna kitu zaidi ya utazamaji wake.

Wahindi ni watu wanafki sana,,pia hawapendi kuona mwanamke yeyote muhindi awe karibu na mwanaume mwafrica.
Kwa jinsi alivyotuangalia yule jamaa nikahisi ni tatizo.

Nikarudi zangu ndani kwangu nikaendelea na shughuli zng,,

Siku ,,week zinakatika huku nikiendelea na ukaribu wa yule mtoto wa kihindi sapna..

Na yeye nilipogunduwa anasikiliza maongezi yetu,,

Basi nizidi kuweka sound za kimahaba zaidi,,

nikazidi kumteka sapna,,hata kwao wakaanza kuhisi jambo mbaya kwangu mm na yeye.

Siku moja yupo ndani usiku hapo home,,

walivamia wahindi pale flat na magongo wakiongozwa na mkuu wa kitongozi,

Wakiwalazimisha homeboys wangu tufunguwe mlango,,wana shida na mm,,

Wale jamaa hawakujuwa kosa na sababu ya mm kutafutwa na wale wahindi zaidi ya 10 na magongo ya ctiket mkononi..

Tukaomba aitwe Mwenye nyumba tujuwe sababu ya kwann mm natakiwa nje na wahindi,,nihojiwe kwann natembea na Binti yao,,

maana yake kinachofatia ni kupigwa magongo ya cricket mwilini.

Yule mama kumbe alishalishwa sumu kwamba natembea na spna Binti yake,

Akiongea kwa uchungu wanitoe mm na tuhame mle flat.

Basi ilitokea purukushani pale tufunguwe mlango na sisi hatutaki,,

Itaendelea.
Wahindi kweli makuππa
 
Daahh huu Uzi kumbe ulihamishiwa huku mode hawajatutendea haki kabisa yaani


Nilikuwa natafuta Sana .. mkuu Hilo jina la chenai linamaana gani nimelipenda Sana Lina sound poa Kama linaasili ya asia hivi
Duu,,mkuu mm maana yake sijuwi,,
Wala sikuwahi kumuuliza.

Lakini mkuu haya majina watu wanayatoa kwenye vitabu na mitandao.

Siku hizi mambo ya majina ya asili imekuwa ngumu sana kuyaona.

Yamebaki family names pekee.
 
Wahindi kweli makuππa
Wahindi ni hatari mkuu,,
Kwa ramli hata kwa ushirikina.

Yule tembo na ubabe wake wote lakini wahindi wanamfanyisha kazi za mashambani,

Mfano kubeba Magogo,
Kulima nk.

Mtu anafuga nyoka yule black mamba,,

Halafu anamkodisha kwa watu either nyumbani au shambani kupambana na panya waharibifu.

Akimaliza kazi ,,anachukuwa joka lake.

Hata sijuwi wahindi wana dawa gani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom