Hasara roho! Pesa makaratasiWewe ni muuzaji wa duka, mteja anakuja na shilingi elfu Kumi (10,000/-) feki anataka Mkate wa shilingi 2,000/- ...wewe bila kujua unaipokea lakini unagundua hauna change ya kumpa mteja unaamua kuomba change kwa jirani yako na hiyo hiyo 10,000 feki kisha unamrudishia mteja shilingi elfu nane (8,000/-) na mkate, baadae jirani anakuja kukuambia ile pesa uliyompa ni feki unaamua kuichukua na kumpa shilingi 10,000/- halali. Je, utakuwa umepata hasara ya shilingi ngapi?
A. 12,000
B. 18,000
C. 10,000
D. 20,000
E. 8,000
F. 2,000
Jaribu
ELEZEA JIBU LAKO KWA KINA
BashiteHasara jumla sh 20,000
Sh 2,000 bei ya mkate, sh 8,000 chenji kwa mteja na sh 10,000 kumlipa jirani
Shukran!Bashite
na 10000 halali ulompa jirani je??hasara ni 10,000 ,ambayo 8,000 umempa huyo tapeli na 2,000 ni ya mkate
baada ya dk chache umetoa elfu kumi halali kumpa jirani yako!!!!!........??C-10,000
Umemrudishia mteja 8,000 na mkate umempa wenye thamani ya 2,000
Katika elfu kumi halali uliyompa jirani, elfu mbili ipo katika ile change iliyobaki, na wewe umeongezea elfu nane yako tu.baada ya dk chache umetoa elfu kumi halali kumpa jirani yako!!!!!........??
Wacha maneno weka muziki...umezunguuka sana.ile 10000 inayozunguka mda wote toka kwa mteja kuja kwako mpka kwa jirani ni fake...kwa hyo itoe kwny mahesabu..yn tupa kapuni..
inshu imeanzia hapa...
jirani yako alikupa change ya sh10000 tena halali. sasa tayr una 10000 halali,,, katika hela ile alokupa jirani unampa mteja sh 8000 na mkate wake wa 2000...yani imepotea kama ilivo,,,, inamana hapo wew dukan hujaingiza kitu......isipokuwa umepoteza 10000 kwa kumpa mteja 8000 na mkate juu.......atakua anajisifu sana huko aliko mana nisawa na kusema umempa vyote hvo bureee............haya tuendelee
baada ya kama dk 5 jirani anakustua,,, oyaa hela ulonipa ni fake,,, bs kwa mara nyngne tena unaamua kuchukua 10000 yako nzuri kabisa na kumpa jirani.
HITIMISHO
8000 Ulompa mteja+2000 ya mkate+10000 ulompa jirani-10000 fake=20000.
umepata hasara ya sh 20000.
mlatinoh king
Hahaaaaa!Wacha maneno weka muziki...umezunguuka sana.
Watu wengine kueleweshwa kitu huwa awahitaji maelezo mengi.
Unawachanganya..
Jibu ni D. 20,000/-Wewe ni muuzaji wa duka, mteja anakuja na shilingi elfu Kumi (10,000/-) feki anataka Mkate wa shilingi 2,000/- ...wewe bila kujua unaipokea lakini unagundua hauna change ya kumpa mteja unaamua kuomba change kwa jirani yako na hiyo hiyo 10,000 feki kisha unamrudishia mteja shilingi elfu nane (8,000/-) na mkate, baadae jirani anakuja kukuambia ile pesa uliyompa ni feki unaamua kuichukua na kumpa shilingi 10,000/- halali. Je, utakuwa umepata hasara ya shilingi ngapi?
A. 12,000
B. 18,000
C. 10,000
D. 20,000
E. 8,000
F. 2,000
Jaribu
ELEZEA JIBU LAKO KWA KINA