A
Anonymous
Guest
Wilaya ya Chemba imegeuka kitovu cha malalamiko makubwa baada ya walimu na watumishi wa Idara ya Elimu Msingi wilayani humo kuibuka na tuhuma nzito dhidi ya Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi, Bw. Josephat Ambilikile.
Wakiwa wamechoshwa na kile wanachoita utendaji mbovu, matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa fedha za Serikali, walimu hao wameamua kuvunja ukimya na kufichua kile kinachoendelea ndani ya Idara hiyo muhimu.
Kwa mujibu wa malalamiko yao, Ambilikile anadaiwa kutumia vibaya nafasi yake kwa vitendo vinavyoashiria ufisadi, upendeleo, unyanyasaji na udhalilishaji wa watumishi. Walimu wanasema, badala ya kuongoza kwa weledi na maadili ya kazi, kiongozi huyo amekuwa chanzo cha mgawanyiko, kuua ari ya walimu na kudidimiza maendeleo ya elimu katika wilaya ya Chemba.
Moja ya tuhuma nzito zilizotolewa ni za ubadhirifu wa fedha za matumizi mengineyo (OC), ambapo Ambilikile anadaiwa kuzitumia akaunti za watumishi kama njia ya kuficha matumizi binafsi. Aidha, inadaiwa kwamba Juni 2025, kati ya shilingi milioni 42 zilizotolewa kwa ajili ya posho za uhamisho wa walimu, shilingi milioni 8 zilielekezwa moja kwa moja kwenye matumizi binafsi ya kiongozi huyo. Hali hii imewafanya walimu waendelee kutaabika huku haki yao ikiendelea kuporwa.
Tuhuma nyingine zenye uzito ni zile za fedha za mitihani ya Taifa, ambapo inadaiwa Ambilikile amekuwa akipunguza stahiki za walimu waliokuwa wakisimamia mitihani na kisha kutengeneza madai hewa ili kujinufaisha. Walimu wanasema hali hiyo imesababisha kero kubwa, kwa kuwa kazi ngumu na ya kitaaluma imekuwa haina tija kwao kutokana na ulaji wa viongozi.
Miradi ya maendeleo nayo haijanusurika. Inadaiwa fedha za miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule ya Sankwaleto pamoja na mradi wa SWASH katika shule ya Sori zimehodhiwa na kiongozi huyo, na matokeo yake miradi hiyo imetekelezwa chini ya kiwango au kutokwenda kwa kasi iliyotarajiwa. Kwa maneno ya walimu, fedha za Serikali zimepoteza thamani kutokana na kushindwa kutumika kama zilivyokusudiwa.
Mbali na fedha, walimu wamelalamikia unyanyasaji na matumizi mabaya ya madaraka. Wanasema Ambilikile amekuwa akiwatisha na kuwatenga wale wanaoonekana kutomuunga mkono, huku wengine wakipata upendeleo kutokana na uhusiano wa kimapenzi alionao nao. Tuhuma hizo zimeelezwa wazi kwamba zimeharibu maadili ya kazi na kuleta mgawanyiko miongoni mwa walimu, hali inayokwamisha mshikamano wa taasisi hiyo.
Aidha, walimu wanasema wamelazimishwa mara kwa mara kuchangia fedha kinyume cha taratibu. Mfano halisi ni shilingi 90,000 zilizochukuliwa kutoka shule zote kwa ajili ya michezo ya UMITASHUMTA, kiasi ambacho kimefikia jumla ya zaidi ya shilingi milioni 10. Wanasema mchango huo ulikuwa wa lazima na waliolazimishwa kutekeleza maagizo wakiwa na hofu ya kudhalilishwa au kutishiwa.
Kiburi na dharau navyo ni sehemu ya malalamiko. Walimu wanadai kwamba kiongozi huyo amekuwa anawasema vibaya viongozi wake hapo wilayani hadharani, akionesha wazi tabia ya dharau na kutoshirikiana na viongozi wake. Hali hiyo imesababisha Idara kukosa mikakati madhubuti ya kuinua ufaulu wa wanafunzi, jambo linaloendelea kuiweka Chemba nafasi ya mwisho kimkoa kwa matokeo ya kitaaluma.
Kiongozi huyo pia anatuhumiwa kutumia vibaya rasilimali za Serikali, ikiwemo mafuta ya magari ya ofisi ambayo huelekezwa kwenye gari lake binafsi. Aidha, anatuhumiwa kutumia kampuni yake binafsi iitwayo URL General Trading Limited kujipatia zabuni ya matengenezo ya magari ya Halmashauri, jambo lililotokea hasa alipokuwa akikaimu nafasi ya Mkurugenzi. Hili limeibua hofu kubwa ya mgongano wa kimaslahi na matumizi mabaya ya nafasi za uongozi.
Athari za utendaji huu mbovu zimekuwa kubwa. Walimu wanasema ari ya kazi imeshuka kwa kiwango kikubwa, kwani wengi wao wamedhalilishwa, kunyanyaswa na kunyimwa stahiki zao. Ufaulu wa wanafunzi nao umeshuka, huku Wilaya ya Chemba ikiendelea kuburuza mkia katika matokeo ya kitaaluma ndani ya mkoa. Wanaongeza kwamba vitendo vya aina hii vimeibua rushwa, mgawanyiko na chuki miongoni mwa walimu, hali inayohatarisha mustakabali wa elimu kwa watoto wa Chemba.
Lakini kilichoibua mshangao zaidi ni madai kwamba mtandao wa viongozi mbalimbali umeundwa ili kumlinda Ambilikile asichukuliwe hatua.
Walimu wanawamtuhumu Afisa Elimu Mkoa, Bw. Kayombo na wengineo kuwa kumlindaji mwovu huyo, wakidai kwamba wamekuwa wakipokea mgao wa fedha za mitihani na fedha zingine. Bw. Kayombo kabla ya hapo amewahi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Wizara ya Tamisemi kabla ya kupelekwa Dodoma baada ya kuharibu mambo kule wizarani.
Aidha, wanamtaja Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Elimu TAMISEMI, Mama Suzan Nusu, kuwa anapokea zawadi na fedha kutoka kwa Ambilikile ili kuendeleza ulinzi dhidi yake.
Huyo Mama Nusu aligombea ubunge Ukerewe mwaka huu lakini kura zake hazikutosha, lakini fedha za uchaguzi huo aliyezikusanya ni Ambilikile kutoka kwa maafisa Elimu wote wa msingi wilayani humo wakati wa shughuli ya Umiseta iliyofanyika mkoani Iringa.
Hali hiyo imewafanya walimu wahisi kukosa msaada hata kutoka kwa ngazi za juu zaidi za uongozi.
Si hivyo tu. Walimu wanasema hata Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Wizara ya Tamisemi Dkt. Emanuel Seleman Shindika ameshindwa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya malalamiko haya, jambo linaloonesha uzembe au kulindwa kwa makusudi. Hali hii imesababisha hisia kwamba mtandao wa kulindana umekuwa kikwazo cha kurejesha heshima ya taaluma na fedha za umma.
Walimu wa Chemba sasa wanapaza sauti kwa Serikali na taasisi za uwajibikaji kuchukua hatua za haraka.
Wanapendekeza uchunguzi wa kina ufanywe na TAKUKURU na vyombo vya dola ili kuhakikisha fedha za umma zinalindwa na waliohusika wanachukuliwa hatua kali za kisheria. Aidha, wanataka Ofisi ya Rais – TAMISEMI ichukue hatua ikiwemo kumhamisha au kumuondoa kabisa kiongozi huyo, kwa kuwa amekaa muda mrefu katika wilaya hiyo na kuunda mtandao wenye ushawishi wa kumlinda.
Kwa mujibu wa walimu, hatua kali pia zichukuliwe dhidi ya viongozi wote wanaotajwa kumlinda, akiwemo Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma, Mkurugenzi Msaidizi wa Idaraya Elimu Tamisemi, Mama Nusu na hata Mkurugenzi wa Idara ya Elimu Tamisemi Dkt Shindika, kwa kuwa wote wameshindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo wakumdhibiti Ambilikile aliyeshindikana.
Wanahitimisha kwa kusisitiza kwamba walimu wa Chemba wamechoshwa, na sasa wanataka uongozi mpya wenye maadili, uwajibikaji na ubunifu. Wanasema bila mabadiliko, elimu ya watoto wa Chemba itaendelea kudidimia na fedha za umma kuendelea kupotea. Serikali inasubiriwa kwa hamu kuchukua hatua ili kurejesha imani ya walimu, wanafunzi na jamii kwa ujumla.
Bw. Ambilikile alipopigiwa simu kwaajili ya kupata habari ya upande wake alipokea simu na kusikiliza tuhuma hizo na kusema yuko bize aachwe kwanza azifanyie kazi. Alipotafutwa baadaye simu yake ilikuwa inaita tu pasipo kupokelewa.