Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Jorghino wa kingereza, back pass laki nane.
 
Wachezaji walioko Injuries na Return Dates kwa leo 24/12/2022

Total injuries = 9
  1. Kepa Arrizabalaga, majeruhi anarudi 27/12/2022
  2. Reece James, majeruhi - 27/12/2022
  3. Wesley Fofana, majeruhi- 08/01/2023
  4. Ben Chilwell majeruhi- 05/01/2023
  5. N'Golo Kante, majeruhi anarudi 04/03/2023
  6. Ruben Loftus-Cheek, majeruhi- 05/01/2023
  7. Carney Chukwuemeka majeruhi- No return date
  8. Armando Broja - majeruhi - no return date
  9. Mason Mount - Tight Calf Muscles - 27/12/2022
Wengine ambao watachelewa kuwepo kwa sababu ya off ya wiki moja baada ya World Cup ni
  1. Hakim Ziyech - Off for one week - 01/01/2023
  2. Mateo Kovacic - Off for one week - 01/01/2023
 
Huyu ndio kiungo wa kununua.

Jamaa yuko versatile sana siyo kama matakataka yaliyojaa pale darajani.
 
Sidhan kama tutalipa hiyo hela kama rb liepzig walikataa summer 80M. Sasa hiv sidhan kama tutamchukua huyu gvardiol,

Ukijumlisha performance ya world cup aah huyu tushamkosa labda tujitoe akili tutoe hiyo 100M ila sioni tukimchukua huyu mtu since tunamaeneo ya kiungo tunahitaj kusaji n kuna uwezekano both jorginho na kante wakaondoka free
 
Chelsea wako katika mazungumzo dhidi ya monaco kwa ajili ya usajil wa beki (lcb) Benoite Badiashile kwa ada ya €35M, Makubaliano bado hayajafikiwa ila inategemewa kufikiwa wiki zijazo.

Machaguo yanayowaniwa kwa ajili ya january/summer ni Gvardiol(Gvardiol personal terms zimeshakuwa agreed tangu summer, ila changamoto iliyobaki makubaliano ya Chelsea na Liepzig.Liepzig kwa sasa wanataka kiasi kikubwa cha pesa )
Evan Ndicka wa Frankfurt
Hincapie wa leverlusen

Source. David Ornstein
 
Huyo Benoite ni beki mzuri kweli?
 
Naona kweli kuna mabadiliko maaana hata tetesi zetu zimekuwa zinaonesha watu tofauti na niwazuri sana
 
Yaaani huyo Rice hata simuelewi
 
Mendy akataa mkataba anataka paundi laki 2 kwa wiki.

Chelsea star Edouard Mendy has rejected a new contract offer because he apparently wants £200,000-per-week. It seems that part of the reason for disenchantment is due to his counterpart Kepa Arrizabalaga
 
Huu

Huu ni mwaka wa 7 tangu nyie misukule mkifurahia ligi inapoanza, lakini tunavyosonga mbele mnapoteana kama misukule
[emoji23][emoji23][emoji23] lembu usiwe unapenda kutumia utani unaofanana na ukweli unapojibizana na hii misukule ya Mateka.
Kuna msukule mmoja uligoma kula siku 3 kisa niliuambia tu kua msimu huu Arsenyani haingii hata kwenye top4.

Baada ya hali yake kua mbaya ndugu zake walikuja kunibembeleza nikaongee na ndugu yao akubali hata kunywa maji, walinitisha kua endapo ndugu yao atapoteza maisha basi nijiandae na kesi ya mauaji itakayo nikabili.

Ule msukule niliukuta katika hali mbaya sana aisee, ila mi niliingia na gea ya kumsifia Arteta na kumhakikishia kua Arsenyani msimu huu anachuka makombe yote kuanzia Epl, Uropa, Uefa, Fa na Carabao tena nikamuhakikishia kua wakimsajili Mudryk pamoja na Joao Felix watachukua mpaka Copa del Rey na La Liga, hapo ndio nikauona msukule unatabasamu na kuomba uletewe uji.

Hawa watu tunatakiwa tuongee nao kwa kutumia akili sana la sivyo tunaweza kusababisha maafa makubwa kwenye jamiii zinazowazunguka.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…